Pinda na kauli zake zilizopinda (Hatma ya nchi yetu)

Ochu

JF-Expert Member
May 13, 2008
976
47
kauli za waziri mkuu pinda zinatia njia panda hatama ya nchi yetu.
kauli ya kuwa meremeta ni suala la usalama wa taifa haliwezi kujadiliwa bungeni wakati kampuni imesajiliwa visiwa vya uingereza na wakurugenzi ni wazungu inatisha. je usalama wa taifa umebinafsishwa? inatisha!!
kauli kuwa waliochota hela za EPA hawawezi kushtakiwa kwa sababu ya uwezo wao kifedha inatisha zaidi. je sheria za jinai ni kwa ajili ya maskini tu?
na hili la zanzibar si nchi sio geni watu walikuwa wanajua lakini kulizungumza kama kiongozi wa ngazi ya juu ya nchi inahitaji umakini kidogo si kuropoka tu. huyu jamaa kweli ni mwanasheria au tunadanganywa?
je tatizo ni hana washauri au ni mkurupukaji?
je kama huyu ndie anaemshauri rais wetu tutegemee nini?
kazi ipo
 
Last edited:
kauli za waziri mkuu pinda zinatia njia panda hatama ya nchi yetu.
kauli ya kuwa meremeta ni suala la usalama wa taifa haliwezi kujadiliwa bungeni wakati kampuni imesajiliwa visiwa vya uingereza na wakurugenzi ni wazungu inatisha. je usalama wa taifa umebinafsishwa? inatisha!!
kauli kuwa waliochota hela za EPA hawawezi kushtakiwa kwa sababu ya uwezo wao kifedha inatisha zaidi. je sheria za jinai ni kwa ajili ya maskini tu?
na hili la zanzibar si nchi sio geni watu walikuwa wanajua lakini kulizungumza kama kiongozi wa ngazi ya juu ya nchi inahitaji umakini kidogo si kuropoka tu. huyu jamaa kweli ni mwanasheria au tunadanganywa?
je tatizo ni hana washauri au ni mkurupukaji?
je kama huyu ndie anaemshauri rais wetu tutegemee nini?
kazi ipo

je kama kweli huyu ndie mshauri wa raisi tutegemee nini?
 
Kwa Hiyo Nchi Yetu Ina Bahati Mbaya Na Mawaziri Wakuu Tunaowapata?
hii ni zaidi ya bahati mbaya. ni hatari sana kuwa na kiongozi wa ngazi ya juu serikalini msema hovyo
 
Wapinzani Bungeni wajipanga kumkabili Pinda

KAMBI ya Upinzani Bungeni imepanga kumbana Waziri Mkuu, Mizengo Pinda hadi ajiuzulu pamoja na serikali yake, baada ya kuwa na uthibitisho kuwa amevunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo aliapa kuwa atailinda wakati anapewa wadhifa huo.

Wapinzani hao hawakuishia hapo, pia wamemgeukia Rais Jakaya Kikwete wakimlaumu kuwa naye anafanya vitendo vya kuvunja umoja wa kitaifa pamoja na kwenda kinyume na mambo ambayo aliliahidi taifa wakati anaingia madarakani.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Msemaji wa Kambi ya Upinzani na Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed alisema kuwa wanamtaka Pinda kutoa maelezo ya kuliridhisha bunge juu ya wapi alipopata madaraka ya kwenda kinyume na katiba kwa kuwaagiza wananchi wajichukulie sheria mkononi kuwaua wale wanaowatuhumu kuhusika na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino).

Alisema kuwa kambi ya upinzani ilikuwa na wasiwasi juu ya ukweli wa habari hiyo iliyotolewa kwa mara ya kwanza na gazeti hili, lakini jana walipata uthibitisho kutoka ofisi yake kuwa ni ya ukweli.

"Tumeshtushwa na hili kwani ni kinyume kabisa na misingi ya katiba yetu. Waziri Mkuu kuhamasisha wananchi kuchukua sheria mkononi, ni kitendo cha kulaaniwa," alisema Hamadi wakati akifafanua juu ya kauli hiyo aliyoitoa Pinda alipokuwa kwenye ziara Kanda ya Ziwa, hivi karibuni.

Mbunge wa Karatu (Chadema), Dk Wilbrod Slaa alisema hawakutarajia matamshi ya hatari namna hiyo yangeweza kutamkwa na kiongozi mkubwa serikalini.

Hata hivyo, alikataa kuweka wazi mikakati ambayo kambi hiyo ya upinzani itaitumia kufanikisha mpango huo kwa maelezo kwamba, ni sawa na askari wanaoenda vitani kuweka hadharani mbinu zao za kivita.

"Kwa kawaida asakari wanaoenda vitani hawawezi kuweka wazi mikakati yao," alisema Dk Slaa na kuongeza kuwa serikali inaashiria kupoteza mwelekeo wa kupambana na mauaji ya kikatili ya albino.

Awali Hamad alisema kambi hiyo inalaani vikali mamaalumu cha vyombo vya usalama kitakachoshirikiana na asasi zisizo za kiserikali, jeshi la kimataifa (Interpol) na wananchi wenguine, ili kuweka mikakati itakayomaliza kabisa tatizo hilo.

Wakizungumzia juu ya kauli iliyodaiwa kutolewa na Rais Kikwete wakati akiwa kwenye ziara kisiwani Pemba, kwamba siku zote wanachagua chama kisichokuwa na serikali na hivyo itawachukua miaka mingi, hadi wao kuwa na serikali; walisema inavunja umoja wa kitaifa.

Alibainisha kuwa kauli hiyo ni kinyume na ahadi aliyoitoa wakati akihutubia bunge kwa mara ya kwanza kuwa atahakikisha anamaliza mpasuko wa kisiasa visiwani Zanzibar.

Dk Slaa aliielezea kauli hiyo kuwa inawezekana alijisahau au hana washauri wazuri au hakua na nia thabiti ya kuupatia ufumbuzi mgogoro wa kisiasa unaoendelea kwa muda mrefu Zanzibar.

Alisema wapinzani wanamshauri rais kuwa kauli hiyo ni ya hatari kwa umoja wa kitaifa, kwa sababu ina mbegu ya ubaguzi na inatonesha vidonda vya machungu waliyo nayo wakazi wa Pemba ya kuuliwa kwa wenzao zaidi ya 20 katika utawala wa serikali ya awamu ya tatu.

Katika hatua nyingine, wabunge hao wa upinzani walidai kuwa pamoja na umoja uliokuwa umeundwa na vyama vyao kusambaratika, wao bado wataendelea kuwa na mshikamano.

Lakini wakasisitiza kuwa wataendelea kuwashauri viongozi wao wasawazishe tofauti zao na kuendelea kuwa na ushirikiano, hasa ikizingatiwa kuwa muswada wa vyama vya siasa ambao upo katika hatua za mwisho kabla haujawasilishwa bungeni, una kipengele kinachowezesha vyama kuunda ushirika unaweza kukusanya nguvu za pamoja ili kushinda kwenye chaguzi mbalimbali.

Pia kambi hiyo ya upinzani iliahidi kuwa itaupinga kwa kauli moja muswada wa wanayamapori, unaotarajia kuwasilishwa kwenye mkutano huu wa 14 wa bunge unaoendelea hapa, kwa maelezo kuwa umezingatia zaidi maslahi ya wageni na kupuuza watanzania.
 
Meremeta kama ni suala la usalama wa Taifa na haiwezi kushitakiwa sasa tuamini nchi imeuzwa au ipo njia panda. Ni jambo ambalo Bunge letu tukufu lilivalie njuga ili ikweli ufahamike isije kuwana la vigogo ambao wanaogopa kuumbuka.
 
Back
Top Bottom