Elections 2010 Pinda na Dr. Slaa wanapogonga kwa furaha

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
733
Hehehe hapa kwa kweli Dr. Slaa umetusaliti Watanzania mbona kimya na kwa gonga hii na Mh. Pinda ina maana serikali ya JK so far umeikubali yetu macho...

slaa_pinda.jpg
 
Hebu ipeni maneno picha hiyo mie nadhani Dr. Slaa anamuambi "mkuu kule Mpanda mjini lazima tuchukue nyie si mko huku hamtaweza kuchakachua na Pinda anajibu hahahahaha Slaa bwana nyie chukueni tu hata kama ni nyumbani kwangu...."
 
Mimi ninamtazamo tofauti: Slaa anamwambia Pinda, bahati yako sikuweka mgombea kwako, usingelikuwepo hapa! Pinda anasema, aisee ungelikuwepo bungeni mara hii, ungelitusambaratishaje?

Kusema kweli picha hii inaonyesha ukomavu wa siasa. Wapo wanaomchukulia Slaa kama adui. Hawa ni majambazi! Wapo wanaomchukulia Slaa kuwa ni mpinzani, hawa ni wanasiasa. Wapo wanasiasa wanaocheka na Slaa, hawa ni wanasiasa wa kweli. Wapo wanaomchukulia kila mwanasiasa ni ndugu, hawa ni wa Tanzania.....
 
Pia wala hakusema kuwa amemkataa Kikwete check hotuba ya kampeni ya Marando wakati alipokuwa anawania Uspika
 
slaa anamwambia pinda , nyie sio watu wazuri mmemchakachua mpaka SITTA.ha ha ha ha
 
yeah! Siasa siyo vita but tofauti ipo ktk sera na njia za kufikia 'common goals'
 
Tanzania ni yetu sote bila kujali itikadi ya vyama vyetu. Hakuna haja ya kuwa maadui kama binadamu; lakini kisera tunatofautiana.
 
MKUU MIMI NAKUUNGA MKONO KAMA SIO MIGUU YOTE MIWILI, NINA UHAKIKA DR SLAA NI MZALENDO WA KWELI, HAWEZI KUTUSALITI WATANZANIA, ILA HICHI KIMYA HATA MIMI, KINANITIA MASHAKA, SISI WENGINE HUKU MTAANI WATU BADO WAMETUNUNIA, SASA WAO WANAKWENDA KUCHEKA NA HAWA MAFEDHULI! BASI TUNAOMBA KUSIKIA TAMKO LA CHADEMA ILI MIOYO YETU ITULIE.

KWA KWELI HAFADHALI MPENDAZOE NIMEMUELEWA, AMEFANYA KILE WANANCHI WANAKITALAJIA, SASA KWA NINI CHAMA MAKINI KAMA CHADEMA HAKIJATOA TAMKO LAKE KAMA CHAMA? DEMOKRASIA YA KWELI NI PAMOJA NA KUHOJI NA KUDADISI, HAPA NAOMBA MAELEZO KUTOKA CHADEMA

:A S angry:
 
Me nadhani anaogopa kuwaomba radhi watz kwa nukuu za uongo ambazo amekuwa akingizwa mkenge na wanausalama wake.
Ajitokeze hadharani tunamsubiri.
 
Slaa anasema 'Tanzania yetu sote, fungu la chadema limeongezeka safari hii, tutakula na kusaza, vipi nyie ccm?"

Pinda anajibu "usijali wewe ccm chama kubwa, kama ruzuku ni ndogo, tutafanya ufisadi tu, tuko pamojaaaaa"

wanagonga wamefurahiiiii :A S angry:
 
Pinda anasema bwana safari hii umetupiga sawa sawa, kama sio kutumia mbinu za ziada tungeenda na maji.
 
Hapo Mh. Pinda anakubali kuwa mwaka huu wa uchaguzi CHADEMA chini ya Dr. Slaa iliiendesha mchakamchaka chama kikongwe cha SISIEMU.
 
Pinda kicheko chake hakitoki moyoni lakini cha Dr. Slaa chatoka moyoni kabisaaaaaaaaaaa...........................Dr. Slaa ana mapenzi ya kweli na nchi lakini hawa CCM wao ni mlo tu upo mbele lakini siyo kulitumikia taifa kwa manufaa ya vizazi vijavyo.................................
 
Back
Top Bottom