Pinda: "muda wa kufanya kampeni bado"

Ustaadh

JF-Expert Member
Oct 25, 2009
413
19
Mh. Pinda unachofanya si kampeni?
.....................................................................
Sitta, Kapuya mambo safi

WANANCHI wa Urambo mkoani Tabora wamemhakikishia Waziri Mkuu, Mizengo Pinda watawachagua Samuel Sitta na Profesa Juma Kapuya kuendelea kuwa wabunge wao.

Wananchi wametoa msimamo huo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mirambo mjini Urambo.

Wameyasema hayo baada ya Pinda kuwauliza kama wako tayari kumchagua Sitta kuwa Mbunge wao tena katika uchaguzi utakaofanyika baadaye mwaka huu.

Wangapi wako tayari kumchagua spika Sitta? Alihoji Pinda na kujibiwa na wananchi wote tuko tayari kumchagua Sitta, Pinda pia aliuliza tena na Kapuya je? Wananchi tuko tayari kumchagua tena.

Waziri Mkuu amewataka wananchi hao wawe makini na watu wanaojitokeza na kugawa pikipiki, baiskeli fedha kwa kisingizio chochote kile kwani lengo lao ni kampeni za kisiasa ambazo sheria hairuhusu kwa sasa.

Wakishawaletea waambieni hizo pikipiki na baiskeli tunazipenda, lakini kwa sasa hatuko tayari kupokea, Bunge likishavunjwa Julai 23, ndio uje na zawadi zako tutakutambua rasmi, Pinda aliwaambia wananchi hao.

Alisema hata baada ya muda wa kampeni kufika ikitokea mtu akiwa anapita kwenye vikundi vya wananchi huku akigawa fedha, wana CCM kwa kanuni mpya zilizopitishwa na Bunge itabidi wamuulize hizo fedha nani kakupa.

Tutakapojua mtu aliyekupa hizo fedha, itabidi tena tukae chini na kujiuliza je amekupa kwa nia njema? Au ana siri nyingine moyoni, alisema Pinda na kueleza kuwa sheria hiyo kwa sasa ipo kwa Rais kusubiri kutiwa saini.

Pinda aliwaambia wananchi hao kuwa ingawa spika Sitta ndiye anayeongoza mijadala ya kutekeleza miradi ya maendeleo, lakini hana uwezo wa kulipendelea jimbo lake la Urambo Mashariki.

Alisema pia kuwa Serikali itafanya juu chini kushirikiana na Spika Sitta ambaye ni Mbunge wa Urambo Mashariki na Profesa Juma Kapuya wa Urambo Magharibi ili kuwaletea wananchi wa Urambo maendeleo.

Waziri aliyasema hayo mjini hapa jana alipokuwa anazungumza na wakazi wa Wilaya ya Urambo akiwa katika ziara ya siku moja ya kutembelea wilaya hiyo.

Msidhani kwa kuwa ni Spika anaweza kuipendelea Urambo. Yeye pale ni kama mfungwa hawezi kufanya lolote lile zaidi ya kusimamia kanuni na taratibu za Bunge tu.

Zaidi zaidi anachoweza kufanya ni kudandia, akitokea mbunge anatetea mradi wake halafu Spika Sitta akaona urambo inaweza kunufaika na mradi huo basi utamsikia anasema barabara hii ni muhimu kwa maana inapita pia Urambo alisema Pinda.

Aliwaambia wana Urambo kuwa amekuwa akifanya kazi kwa karibu zaidi na spika Sitta kuhakikisha kuwa nchi inapata maendeleo na kuondoa umasikini kwa wananchi.

Alisema kama ilivyo katika mikoa mingi nchini wananchi katika Wilaya ya Urambo wanaishi katika umasikini kutokana na pato lao kwa mwaka kuwa takribani Sh 300,000 kwa mwaka.

Bado hali si nzuri ukichukua Sh 300,000 ukaigawa kwa mwezi halafu ukaigawa ni Sh ngapi kwa siku utaona hali si nzuri sana. Alisema Pinda.

Chanzo: Habari leo
 
nadhani wa kulaumiwa ni wananchi wetu wenyewe; watu wetu wana mitazamo mifupi sana kuhusu future zao na wala hawataki kuwauliza viongozi wao maswali magumu. Utadhani viongozi ni watu maalum sana waliozaliwa kuwa watawala tu badala ya kutambua kuwa viongozi wale wapo pale kwa sababu ni sisi tuliowaweka pale.
 
Tatizo Tanzania ni elimu ya uraia hasa vijijini.Lakini kwa Sitta mimi nadhani ni vyema tu akarudi tena bungeni.Ila huyo Prof huyo mhhh...
 
Back
Top Bottom