Pinda: Mshaurini JK kuhusu mishahara ya wabunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda: Mshaurini JK kuhusu mishahara ya wabunge

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by fangfangjt, Apr 2, 2011.

 1. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Pinda: Mshaurini JK kuhusu mishahara ya wabunge

  Said Powa
  WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, ameiagiza Tume mpya ya Utumishi wa Bunge kumshauri Rais kuhusu malipo ya mishahara ya wabunge baada ya bunge kuvunjwa na Rais kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu.

  Akizindua tume hiyo jijini Dar es Salaam jana Pinda alisema katika bunge la tisa uzoefu unaonyesha kwamba kuna tatizo kuhusu uhalali wa mishahara na posho za wabunge baada ya bunge kuvunjwa.

  Alifafanua kwamba wananchi na wabunge wanataka kujua kama kweli upo uhalali wa wabunge kuendelea kulipwa baada ya bunge kuvunjwa na Rais. Pinda alisema kutokana na hali hiyo ilifahamika kwamba baada ya Rais kuvunja bunge na kutangazwa kwenye gazeti la Serikali, ndiyo ukomo wa muda wa mbunge, kwa mantiki hiyo ndiyo ukomo wa malipo ya mishahara na posho zote zinazolipwa kwa wabunge.

  “Moja ya jukumu la kamati hii ni kumshauri Rais kuhusu malipo ya mishahara na posho na stahili zingine za Wabunge kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu. Natumaini kamati italifanyia kazi suala hili ili lieleweke vizuri kwa waheshimiwa Wabunge,” Alisema Pinda. Pinda alisema bajeti ya ofisi ya bunge imekua ikioboreshwa ili kuiwezesha sekretarieti ya bunge kutoka Sh26.5 billioni 2006/2007 hadi kufikia Sh70.5 billioni mwaka wa fedha 2009/2010.

  “Suala la kupokea mishahara na posho kwa Wabunge wakati Rais ameshavunja bunge, lilileta maneno mengi na sintofahamu kwa wananchi na hata wabunge wenyewe mwaka jana,”alisema Pinda.

  Hii ni mara ya kwanza kwa tume inayomaliza muda wake kufanya makabidhiano rasmi na tume mpya, hata hivyo mwenyekiti aliyemaliza muda wake Samweli Sitta, hakuwepo kwa maelezo kuwa yuko nnje ya nchi kikazi na nafasi yake ilichukuliwa na mwenyekiti wa sasa ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume iliyomaliza mudawake Anne Makinda.

  Naye mwakilishi wa Katibu wa Bunge, Eliakimu Mrema, alisema kuna tatizo la uhaba wa watumishi hasa ukizingatia ongezeko la wabunge na kufanya ikama ya watumishi kutoendana na ongezeko la wabunge ambao kwa sasa wamefikia 357 ikilinganishwa na ikama ya watumishi 251 wa sasa na kupunguza ufanisi wa kazi.

  Akitoa mfano Mrema alisema Bunge la Zambia lenye wabunge 260 tu, lakini linahudumiwa na watumishi zaidi ya 500.
   
 2. m

  mzambia JF-Expert Member

  #2
  Apr 3, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 882
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35

 3. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #3
  Apr 3, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Pinda anapotaka Tume ya Utumishi imshauri Rais yeye anafanya kazi gani? Pia inatushangaza kuwa mishahara ya wabunge tangu walipoanza kulipwa kumbe hapakuwa na utaratibu. Leo baba (Pinda) anamshauri mtoto (tume) aende kwa baba mkubwa (rais) ili amshauri, hapo kuna mantiki kweli.

  Pinda aache usanii, nchi hii tumeshaielewa wala hakuna sababu ya kujitetea kuwa hamkuwa mnafahamu utaratibu.
   
Loading...