PINDA : Mshahara wa RAIS unatakiwa kujadiliwa na kupitiswa na BUNGE ila sijaliona hilo

amakyasya

JF-Expert Member
Jun 26, 2013
3,480
907
Wana JF:

Leo bungeni akijibu swali la papo kwa papo la mheshimiwa Mnyaa aliyeuliza '' Ni lini bunge lilikaa kujadili na kupitisha mshahara na posho za rais kama katiba inavyotaka? Waziri mkuu Pinda alishindwa kujibu na aliishia kusema hajui ni kwa nini hajawahi kuona pia suala hilo likiletwa bungeni japo katiba inataka iwe hivyo. Na pia akasema labda kuna sheria nyingine inayoruhusu lisijadilwe bungeni japo pia hakujua ni sheria gani. Kiujumla majibu yake katika hili yalikuwa ni ya kubahatisha ama kukisia tu bila uhakika wowote.

Je, kama waziri mkuu ambaye ni kiongozi mkuu wa shughuli za serikali bungeni hajui suala nyeti kama hili, inatoa tafsiri gani kwa wananchi wa kawaida?
 
Wananchi wakawaida tunapata picha kuwa viongozi wengi wa serikali ya CCM hawana majibu fasaha matatizo ya nchi yetu maana hata Rais Kikwete aliwahi kusema hajui kwa nini watanzania ni masikini.
 
Wananchi wakawaida tunapata picha kuwa viongozi wengi wa serikali ya CCM hawana majibu fasaha matatizo ya nchi yetu maana hata Rais Kikwete aliwahi kusema hajui kwa nini watanzania ni masikini.
Mkuu kiukweli ni majibu ya kusikitisha kuyasikia kutoka kwa viongozi wakubwa wa nchi.
 
Katiba peke yake haiwezi kutoa majibu ya mawsali yote zipo pia sheria na taratibu zinazoongoza maswala haya.
 
Katiba peke yake haiwezi kutoa majibu ya mawsali yote zipo pia sheria na taratibu zinazoongoza maswala haya.
Pinda kashindwa hebu msaide kuitaja hiyo sheria ambayo imeondoa suala la mshahara wa rais na pm kupitishwa bungeni kama katiba inavyotaka.
 
Katiba peke yake haiwezi kutoa majibu ya mawsali yote zipo pia sheria na taratibu zinazoongoza maswala haya.

kwa sababu na ufisadi wenu...katiba inasema bunge litajadili na kupitisha, mshahara wa Rais, iweje nyie mnalipana kisirisiri!.ufisadi ni sera ya ccm
 
kwa sababu na ufisadi wenu...katiba inasema bunge litajadili na kupitisha, mshahara wa Rais, iweje nyie mnalipana kisirisiri!.ufisadi ni sera ya ccm

Wanajitengenezea mazingira ya ufisadi tu hawataki uwazi wanapenda mambo ya mafichoni ndo maana wanashindwa kujibu maswali wakibanwa ili waeleze ukweli. Hawana kumbukumbu maana mambo yao mengi ni ya kuchakachua zaidi.
 
Magamba wengi wako bungeni kupiga makofi na kugonga mabenchi hapo AG angeingilia atoe ufafanuzi wa kina
 
Back
Top Bottom