Pinda: Mimi sio mcha Mungu

Mbalinga

JF-Expert Member
Apr 9, 2010
1,714
1,370
Wana jamii,

Jana Mh Pinda alipokuwa anajibu hoja ya Mh Mlata alianza kwa kusema kuwa "Mimi sio mcha Mungu, isipokuwa ni muumini wa kawaida tu". Hivi kauli kama hii ina maana gani?
 
Wana jamii, Jana Mh Pinda alipokuwa anajibu hoja ya Mh Mlata alianza kwa kusema kuwa "Mimi sio mcha Mungu, isipokuwa ni muumini wa kawaida tu". Hivi kauli kama hii ina maana gani?
Mtu hunena yale yaujazayo moyo wake. Amekiri kuwa yeye si mcha mungu na ndiyo maana hajali watu wanapokufa kwa umaskini na mgomo wa madaktari. kuna tofauti kati ya mcha mungu na muumini wa kawaida.

Mcha mungu humwogopa sana mungu, kwani ndiye mlinzi wake, na wakati wote anamhofu mungu kwani anajua wakati wa kuishi duniani ni mfupi na ataondoka wakati wowote. Mtu huyo madaraka yake au mali si kitu anachokithamini zaidi ya ubinadamu na utu.

Muumini wa kawaida kama Pinda yeye kwake mungu ni ziada tu. anaweza akawa na mganga wa kumlinda, kwake mali, heshima, cheo ni vitu anavyoviabudu, hajali watu wengine kwa vile tu yeye ana pesa na mdaraka. Yeye kwake mungu si muhimu.

NAFIKIRI UMEELEWA, NA NDIYO MAANA VIONGOZI WETU HAWAJALI KUIBIA TAIFA HILI KWA KUSAINI MIKATABA ISIYO NA TIJA, WAPO TAYARI KUNUFAIKA NA UMASKINI WA WETU KWA KUOMBA MISAADA UGAIBUNI LAKINI IKIJA HAIENDI KWA WALENGWA, WAKO TAYARI WAKATIBIWE INDIA BAADALA YA KUWASOMESHA WATAALAMU WA HAPA ILI WOTE TUTIBIWE HAPA.

SWALA LA WALIMU WA SERIKALI HAWANA FAIDA KWANI WAO HUSOMESHA SHULE BINAFSI. HIVYO WALIMU WAFUNDISHE AU WASIFUNDISHE HAYAWAHUSU KAMA SWALA LA MGOMO LISIVYO WAHUSU.
 
Wana jamii,

Jana Mh Pinda alipokuwa anajibu hoja ya Mh Mlata alianza kwa kusema kuwa "Mimi sio mcha Mungu, isipokuwa ni muumini wa kawaida tu". Hivi kauli kama hii ina maana gani?

Amesema ukweli wake. Vinginevyo wangemtarajia aanze kunukuu mistari kwenye kitabu kitakatifu.
 
Wana jamii,

Jana Mh Pinda alipokuwa anajibu hoja ya Mh Mlata alianza kwa kusema kuwa "Mimi sio mcha Mungu, isipokuwa ni muumini wa kawaida tu". Hivi kauli kama hii ina maana gani?

Usemi wa "na liwe liwalo" ni tosha kuonyesha kuwa mtoa usemi huo amempa Muumba kisogo!
 
zamani mkononi alikuwa anavaa pete ya ndoa tu..lakini siku hizi kuna mapete mawili hivi huwa anavaa makuuubwaa..halafu lipo lipete limoja hivi huwa lina kama alama ya nyota na yenye rangi ya blue..basi akiwa anaongea na mtu/watu huwa analionyesha kuelekea kwa watu huku akilizungusha zungusha kwa kutumia dole gumba....
 
Mzee Muongo sana huyu, tena ni mnafiki na mzandiki, nani amemuambia kuna daraja wa waumini wa kawaida? yeye akiri kwamba ni MUOVU na ni mtu wa shirki.hapo roho ya uzinzi ndio imemsukuma kusema hivyo

Kuna kamsemo kanasema "USIHUKUMU KABLA HUJAHUKUMIWA" utakuwa umekasahau au?
 
Kuna kamsemo kanasema "USIHUKUMU KABLA HUJAHUKUMIWA" utakuwa umekasahau au?

Kako wapi? Hapo kalipo, panaauthority gani ya kuninyanganya uhuru wangu wa kufikiri na kuamua/kuhukumu, wapi?
 
Anazidi kujichanganya huyu dhaifu part 2.

Hawezi kusema ni mcha mungu maana alicho kifanya akisema ni mcha mungu mdomo unaweza kwenda upande.
 
Back
Top Bottom