Pinda: Mawaziri kutangaza upendeleo wa ki-itikadi ni 'unfortunate'!

kibunda

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
403
52
Nimeona na kusikia kwenye taarifa ya itv waziri mkuu akisema mawaziri wanaotangaza kupeleka maendeleo kwa upendeleo wa ki-itikadi za kisiasa ni unfortunate. Alikuwa akijibu swali la mbowe kwenye maswali ya papo kwa papo.

My take, swali hilo hakutegemea. Ndiyo maana amelijibu bila kujiandaa. Ameshindwa kupiga siasa ndiyo maana amekiri kiaina kuwa serikali ilikosea. Lakini, kwa kweli walikuwa wanajua wanachokifanya. Hatujawahisikia serikali ikikanusha kauli hizo.

Aidha, kwa nini watanzania wasihoji kauli za ccm kujinadi kuwa ndiyo yenye serikali. Hivi hawajui kuwa serikali ni ya wananchi? Siku moja ukweli utajulikana tu. Leo pinda ametupeleka hatua moja mbele.
 
Daaa nlitamani hili swali liulizwe ili kuskia tamko la serikali so now iko poa ku clear hali ya hewa........big up Mbowe!!!!
 
Nimeona na kusikia kwenye taarifa ya itv waziri mkuu akisema mawaziri wanaotangaza kupeleka maendeleo kwa upendeleo wa ki-itikadi za kisiasa ni unfortunate. Alikuwa akijibu swali la mbowe kwenye maswali ya papo kwa papo.

My take, swali hilo hakutegemea. Ndiyo maana amelijibu bila kujiandaa. Ameshindwa kupiga siasa ndiyo maana amekiri kiaina kuwa serikali ilikosea. Lakini, kwa kweli walikuwa wanajua wanachokifanya. Hatujawahisikia serikali ikikanusha kauli hizo.

Aidha, kwa nini watanzania wasihoji kauli za ccm kujinadi kuwa ndiyo yenye serikali. Hivi hawajui kuwa serikali ni ya wananchi? Siku moja ukweli utajulikana tu. Leo pinda ametupeleka hatua moja mbele.
Siamini kauli yake, si mnakumbuka ahadi ya Magufuli Igunga? Eti akichaguliwa mgombea wa CCM basi atajenga daraja. Kama angechaguliwa mgombea wa CDM inamaana daraja lingejengwa?
 
Kama PM alitakiwa kuwa straight na kusema kama kuna mtu kasema hivyo ni KOSA na mimi kama Waziri Mkuu NAKEMEA kauli hizo. Serikali inatoa fedha za maendeleo kwa kufuata miongozo ya nchi na maamuzi yenu Wabunge katika bajeti.

Huwezi kusema ni unfortunate bila kutoa mwongozo. Afterall, kauli za namna hiyo huwa zina backfire katika chaguzi zote maana Wananchi wanakuwa na huruma na upande wa pili ambao unataka kuwaonyesha kuwa wao hawana access na keki ya Taifa!!
 
Hii ni hoja nzito sana nakumbuka hivi karibuni huko Arumeru mashariki waziri Nagu aliuambia umati wa kampeni za ccm iwapo Sioyi atachaguliwa basi ule mradi wa Economic Preferrential Zone (EPZ) utawahishwa ili wanaarumeru hasa vijana wapate ajira, na iwapo angechaguliwa Nassari basi angecheleweshachelewesha mradi huo. Sasa ngoja tusubiri. Wajuwe serikali ya ccm inatumia kodi zetu sote bila kujali itikadi za vyama. Ni vizuri ccm wakaelewa hivyo na kwamba kura walipigiwa na wananchi wa itikadi zote hadi wakawa chama tawala.
 
Ni kweli. Pm amelijibu simple lakini lina maana kubwa sana.
Alitakiwa kupitia majibu yake Bungeni kukemea vikali na kupiga marufuku kauli za kibaguzi kama hizo kutolewa na viongozi wa serikali. Kama kawaida yake ameshindwa kuonyesha uongozi kwa kujibu kinafiki ili hasiwahudhi wana magamba wenzake!
 
Pinda ni waziri mkuu dhaifu sana kwa wakati huu. Nilitarajia angetamka bila kuuma maneno kuwa mawaziri wake walifanya makosa na akatoa onyo kali kwani vitendo na kauli zao ni kinyume cha katiba na sheria za nchi.

Hata hivyo lazima tukumbuke kuwa serikali ya ccm inatawala kwa hila na hila zao zinaelekea mwisho. Kuna umuhimu kwa wanahabari na asasai za kiraia kuendelea kutoa elimu juu ya sheria na taratibu za uendeshaji wa nchi ili Watz wasiendelee kudanganywa na wenye uchu wa madaraka kama ccm.
 
Kwa hili, serikali inatia aibu. Hatuwezi kuwa na Serikali inayotangaza ubaguzi wa wazi kabisa. Nimepata taarifa hata kule UDOM wanachuo ambao ni CDM wanaitwa kila majina mabaya, tena na viongozi wa chuo. Imefikia wanaambiwa Alshabab, ama Bokoharam! Dhambi hii inaweza watafuna hata CCM watakapo kuwa wapinzani. Najua wao watapiga kelele sana.
 
Kama PM alitakiwa kuwa straight na kusema kama kuna mtu kasema hivyo ni KOSA na mimi kama Waziri Mkuu NAKEMEA kauli hizo. Serikali inatoa fedha za maendeleo kwa kufuata miongozo ya nchi na maamuzi yenu Wabunge katika bajeti.

Huwezi kusema ni unfortunate bila kutoa mwongozo. Afterall, kauli za namna hiyo huwa zina backfire katika chaguzi zote maana Wananchi wanakuwa na huruma na upande wa pili ambao unataka kuwaonyesha kuwa wao hawana access na keki ya Taifa!!

jamani huyu mizengo msameheni bure tu mkiendelea kumuuliza sana atamwaga chozi sasa hivi.
 
Swali zito akatoa majibu mepesi sana!
Alafu mwanzo alikuwa kama anapinga kuwa hakuna kitu kama icho mbowe alipompa mifano naona akaona haya na kuanza kujikanyaga!
Tatizo wabunge wa CCM wanakosaga cha kuongea so wakiishiwa chochote kitakchomjia kichwani twende kazi
 
Tangu tupate uhuru, tokea Jk Nyerere first prime minister, mpaka yeye Pinda, hakuna waziri wa ajabu kama Pinda. Ana mapungufu ya kiutendaji hata kuyaorodhesha yanatia kichefukichefu.
 
Tangu tupate uhuru, tokea Jk Nyerere first prime minister, mpaka yeye Pinda, hakuna waziri wa ajabu kama Pinda. Ana mapungufu ya kiutendaji hata kuyaorodhesha yanatia kichefukichefu.

Ndio maana watu hwamchukulii serious, kila siku anapindisha maneno, hata jambo alilowahi kulifanya hata tukamkumbuka (legacy), tungekuwa na PM madhubuti hakuna ambaye angekuwa anamkumbuka Lowassa, au Sokoine, nchi inakosa kabisa viongozi ina watu waliojaza nafasi za uongozi.
 
Ujumbe umefika kwa mawaziri wote na pia kwa wabunge wanaojikomba!
 
Bonyeza hapa Down:

Mbowe awalipua mawaziri bungeni

My Take: Binafsi sijaridhika na majibu ya PM Pinda;

Ingelikuwa kauli hizi za Ubaguzi zinatolewa na Vyama Pinzani basi wangelifunguliwa kesi za kupinga matokeo.

PM - Pinda huoni aibu kutoa majbu hayo, kama hujajiandaa kwa nini usimuombe Spika ili uyajibu siku nyingine!!!!!!!

MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
wewe ndio mara kwanza kusikia majibu ya PIMBI @PINDA hapo mbona kajitahidi kujibu
 
Swali la Kamanda Mbowe halikutendewa haki kabisa na Prime Minister..kwa kweli sikumbuki ni lini nimepata kuridhishwa na PM Pinda...
Kwake yeye ,maswali magumu hayana nafasi katika ubongo wake na ndio maana majibu yake yanaishia kutuacha wazi baadhi yetu.
Kama yeye,tena akiwa msaidizi mojawapo wa RAIS na kiongozi wa shughuli za serikali bungeni hatoi majibu ya kina na yenye kujitosheleza, Naibu waziri gani afanye hivyo?Hali itakuwaje huko katika halmashauri na serikali za Mitaa ambazo kwa mujibu wa utaratibu wao,zipo chini yake?
Kanuni za bunge zinasemaje kuhusu watu watoao majibu ya reja reja ya aina hii?
 
Back
Top Bottom