Pinda kuweka hadharani majina ya mawaziri wanaojizulu

COSTOMER

Member
Feb 24, 2012
70
9
Waziri mkuu pinda leo ifikapo majira ya saa sita za mchana anatarajia kuweka hadharani majina ya mawaziri saba walioamuliwa kujiuzulu kufuatia kashfa za ufisadi ambazo zinaelezwa ama kusababishwa na wao ama watendaji wao na wao kubeba dhamana hiyo.

mawaziri ambao wanatajwa kukumbwa na sakata hilo ni pamoja na Waziri wa Fedha, Mustapha Mkulo, Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu, Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Cyril Chami na naibu wake, Lazaro Nyalandu.

hata hivyo mpaka hapo jana usiku mwenyekiti wa POAC Zitto kabwe amefanikiwa kukusanya kura 75 tano zikiwa za wanachama wa CCM ambao ni Deo Philikunjombe wa Ludewa, Ally Keissy Mohamed wa Nkasi Kaskazini, Alphaxard Kange Lugola wa Jimbo la Bunda, Murtaza Ally Mangungu na mbunge mmoja wa Viti Maalumu kutoka Kanda ya Ziwa ambaye hakutaka atajwe kwa sasa.
 
Tupeni taarifa za uhakika jamani.hivi sasa jf inataka kubadilika kuwa kama sehemu ya kupiga umbea.tafadhali wana jf wote tulete taarifa zilizo sahihi.
 
Idadi ndogo ya wabunge wa CCM watiokubali kuweka saini zao katika kuiunga mkono hoja ya Mh. Zitto ina dhiditisha nijinsi gani CCM walivyo kuwa wanafki pindi wawapo bungeni na kujidai wanatetea maslahi ya umma! eg Mama Kilango, Makamba,Olesendeka na wengine wengi.
 
Tupeni taarifa za uhakika jamani.hivi sasa jf inataka kubadilika kuwa kama sehemu ya kupiga umbea.tafadhali wana jf wote tulete taarifa zilizo sahihi.
hiyo taarifa ni kwa mujibu wa katibu wa wabunge wa chama cha mapinduzi Jenista muagama ndugu yangu hakuna uongo hapooooo!!!! hata hivyo nikimnukuu jam]nuary makamba kupitia Power breackfast jumamosi amesema hivi" kuna maamuzi yamefanywa na atakaye tangaza maamuzi hayo ni waziri mkuu pinda leo kabla ya kikao cha saa saba kuhairishwa". tufuatilie bunge tutayaona unless jenista awe amedanganya wanahabari bungeni jana usiku kwenye oresscof. aliiyoitishwa
 
Back
Top Bottom