Pinda kumlegeza Waziri Magufuli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda kumlegeza Waziri Magufuli

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by issenye, Sep 15, 2012.

 1. i

  issenye JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 1,146
  Likes Received: 989
  Trophy Points: 280
  Na George Ramadhan | 14th September 2012

  Kuna dalili kwamba Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, huenda akalegea kuwabomolea nyumba wananchi waliojenga katika maeneo ya hifadhi za barabara katika baadhi ya maeneo nchini, baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuahidi kumshawishi alegeze kamba.

  Waziri Magufuli mara kwa mara amekuwa akisisitiza kuwa watu wote waliojenga katika maeneo ya hifadhi ya barabara lazima wabomoe nyumba zao na kuondoka vinginevyo serikali itazibomoa bila kuwalipa fidia.

  Wakati Magufuli akiendelea kushikilia msimamo huo, Pinda amewaahidi wakazi wa Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza kwamba atazungumza na Waziri huyo ili asibomoe nyumba ambazo zimejengwa kwenye hifadhi ya barabara wilayani humo.

  Akiwahutubia wananchi wa wilaya hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika juzi kwenye uwanja wa Getrude Mongella mjini Nansio, Pinda alisema licha ya ukweli kwamba nyumba nyingi zimejengwa ndani ya hifadhi, lakini ameona si busara kuzibomoa kupisha upanuzi wa barabara.

  Alisema kwamba baada ya kutembelea wilaya hiyo katika ziara ya kikazi, amejionea mwenyewe jinsi barabara za mji wa Nansio zilivyo finyu kutokana na nyumba nyingi kujengwa kwenye hifadhi, hali ambayo alisema endapo Dk. Magufuli ataingia wilayani humu kutekeleza sheria ni wazi atabomoa nyumba nyingi.

  "Hakuna ubishi kwamba mnahitaji barabara nzuri, lakini suala la barabara pia lina kero zake, akija Magufuli hapa atawaambia anataka mita zake 30 kila upande wa barabara, lakini kwa jinsi nilivyoona, nyumba nyingi zitabomolewa," alisema.

  Hata hivyo, alisema kwamba kutokana na uhaba wa ardhi, ameona ni busara azungumze na Dk. Waziri Magufuli aangalie uwezekano wa kupindisha sheria ili wakazi wa Wilaya ya Ukerewe waliojenga kwenye hifadhi ya barabara wasibomolewe nyumba zao.

  "Ni kweli kwamba ipo sheria, lakini ni lazima sheria hiyo imsaidie mwananchi, kwa hiyo suala hili mniachie nitakwenda kuongea na Magufuli kusudi aangalie nini cha kufanya kunusuru nyumba zenu nzuri nzuri nilizoziona zisibomolewe," alisema Waziri Mkuu.

  Waziri Mkuu Pinda alibainisha kuwa Wilaya ya Ukerewe yenye wakazi wapatao 260,000 na eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 6,400, ni asilimia 10 pekee ndiyo nchi kavu na sehemu iliyobaki ni maji.

  Kwa kuzingatia hali hiyo, alisema haoni kwa nini wananchi wabomolewe nyumba kwa ajili ya kupanua barabara hasa ikizingatiwa kuwa wilaya hiyo ni kisiwa, hivyo hakuna mahitaji makubwa ya barabara kuu.

  Wakati huo huo, Pinda amesema Wilaya ya Ukerewe inastahili kupata meli mpya na kubwa zaidi ambayo itachukua nafasi ya meli ya muda mrefu MV Clarias na MV Butiama ambayo hivi sasa ni mbovu.

  Alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo, kujenga hoja kuishawishi serikali ili ipeleke meli hiyo mapema iwezekanavyo.

  CHANZO: NIPASHE


  Hapo kwenye nyekundu?????????
   
 2. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Magufuli akilegea tu,italeta shida hasa kwa wale ambao tayari wamevunjiwa nyumba zao!!!
  Mawazo yangu,Waziri Mkuu anawaahidi kitu ambacho kitashindwa kutekelezeka!!
   
 3. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Waziri mkuu wetu vipi mbona hatumwelewi. Amwache Magufuri afanye kazi yake kwa kufuata sheria na kanuni.Pinda aendelee kuwasafisha mafisadi kama vile Ngeleja (Mzee wa mgao feki) lakini mwisho wa siku wananchi tutaamua la kufanya.
   
 4. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,693
  Likes Received: 12,742
  Trophy Points: 280
  Ni ngumu sana
   
 5. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,524
  Likes Received: 10,441
  Trophy Points: 280
  mwacheni magufuli afanye kazi yake, pm gani unakua mwoga wa kufuata sheria.?
   
 6. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #6
  Sep 15, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Naona Pm ameacha kufikiria wajibu wake sasa anafikiria kura za 2015
   
 7. M

  Mcjoe Member

  #7
  Sep 15, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 71
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kulikuwa na ulazima gani kwa pm kulizungumzia swala ambalo utatuzi wako ni wa ofisi nyingine?
   
 8. i pad3

  i pad3 JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,520
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  serikali legevu
   
 9. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #9
  Sep 15, 2012
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Ameanza kulialia tena,ngoja uchaguzi unakuja muwajibikaji ndiye atakaye kaki.
   
 10. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #10
  Sep 15, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hii ndiyo double standard inayotuchanganya wananchi. Kwanini wengine tuvunjiwe na wengine kuwe na flexibility hiyo. Halafu kwani Mh.Pinda aliapa kwaajili ya Mh.Magufuli na kumuahidia kuwa atapindisha kusimamia sheria pale itakapobidi.
   
 11. M

  MTK JF-Expert Member

  #11
  Sep 15, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280
  Kauli ya Pinda inafanya dhana ya utawala wa sheria kuwa kichekesho japo sishangai kwani this has become "the practice rather than the exception" hapa nchini!!

  On the flip side of it, John Pombe Kali magufuli akiridhia "kupindisha sheria" itamuweka mahali pabaya sana kuendelea na kasi yake ya kutekeleza sheria ya barabaya ya mwaka 2007; wahanga waliotangulia wa sheria hiyo will go up-in arms kwa sababu sheria nzuri haitakiwi itumike kwa ubaguzi. tusubiri tuone!
   
 12. I

  Ichobela JF-Expert Member

  #12
  Sep 15, 2012
  Joined: Jan 7, 2012
  Messages: 249
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  Hapa kuna watu wa kadhia mbili tofauti. Kuna mwanasiasa na mtendaji. Magufuli ni mtendaji wakati aliekuwa mtoto wa mkulima kajiingiza kwenye siasa wkt ki ukweli haukuwa mwelekeo wake. Hapa nionavyo mm,Magufuli atakubari kupindisha sheria,na wala hataenda Ukerewe" kwa nn nasema hayo,ndugu yangu Magufuli inasemekana kuwa anampango wa kuingia magogoni,hivyo ataombwa kulinda kura za 2015. Kwa hiyo sitashangaa sheria kupindishwa!
   
 13. m

  mkupuo JF-Expert Member

  #13
  Sep 15, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180
  Kweli nimekubali kwa 100% kuwa hii serikali ni dhaifu! kwani wakati sheria hiyo inatungwa wilaya ya Ukerewe ilikuwa haijaanzishwa? je, si hawahawa magamba walioipitisha? Nimeamini tena sasa kuwa gamba limeendelea kujitanua mwilini mwa wana CCM na sasa limehamia kwenye bongo zao!
   
 14. F

  FJM JF-Expert Member

  #14
  Sep 15, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Sijui nitumie maneno gania lakini itoshe tu kusema kuwa sipendi hata chambe uongozi wa Mizengo Pinda. Hana jipya la kusaidia hii nchi zaidi ya siasa za ujima na visasi.
   
Loading...