Mpita Njia
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 6,997
- 1,163
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda leo mchana (Ijumaa, Januari 8, 2010) anatarajiwa kufanya ziara ya siku moja katika wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro kukagua athari za mafuriko na jitihada ambazo Serikali imefanya hadi sasa ili kuwasaidia waathirika wa maafa hayo.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Waziri Mkuu ambaye anatokea Mpanda alikokuwa kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka, atapokewa eneo la VETA Mikumi na viongozi wa mkoa huo na kupatiwa taarifa ya maafa ya Mkoa kabla ya kuendelea na safari ya Kilosa.
Akiwa Kilosa, Waziri Mkuu atatembelea eneo la Magomeni Kilosa na kusalimiana na wahanga na baadaye ataenda eneo la Machinjioni ambako ndiko kwenye chanzo cha tukio la mafuriko.
Pia atakwenda Njia Sita (Kasiki) kukagua uharibifu uliotokea kwenye Pump House kabla ya kwenda soko la Mbumi kuangalia maafa yaliyolikumba kwenye eneo hilo. Vilevile atakwenda maeneo ya Behewa, Kimamba na Kondoa kuwapa pole wananchi wa maeneo hayo na kukagua nyumba zilizoharibiwa na mafuriko hayo.
Wakati wa ziara hiyo, Waziri Mkuu atazuru pia kambi ya Shule ya msingi Kilosa Town na kuwapa pole wahanga walioko kwenye kambi hiyo ambako wamepatiwa hifadhi na Serikali.
Mafuriko ya Kilosa yametokana na mvua hizo zilizoanza kunyesha Desemba 24, 2009 zilizosababisha maafa ya watu kufariki, kubomolewa kwa nyumba na miundombinu kama barabara, reli na madaraja hasa katika wilaya za Kilosa na Morogoro Vijijini kwa mkoa wa Morogoro na wilaya za Kongwa, Mpwapwa na Chamwino kwa mkoa wa Dodoma.
Waziri Mkuu anatarajiwa kurejea jijini Dar es Salaam kesho (Jumamosi, Januari 9, 2010) mchana.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, JANUARI 08, 2010
===

Leo JK yupo Kilosa!
Kwa habari nilizonazo, Leo JK yupo Kilosa mkoani Morogoro kuwafariji wahanga wa mafuriko. Pinda alianza yeye anafuatia! Pia soma https://www.jamiiforums.com/threads/pinda-kukagua-mafuriko-kilosa.49292/...
www.jamiiforums.com
Serikali ya Libya yajitokeza Kusaidia Athari Za Mafuriko Kilosa kuwajengea Nyumba 200
Ndugu zanguni wana JF nilikuwa ninaperuzi kwa Michuzi nimekutana na habari hii Serikali ya Libya yajitokeza kusaidia Athari za mafiriko kilosa kuwa itawajengea nyumba 200 waathirika zenye thamani ya shilingi 1.5 bilioni. Nikajiuliza serikali hii iliyosaidiwa imegharimika kumjengea mtu mmoja...
www.jamiiforums.com
Maafa ya Mafuriko Katika Picha Na Wito Kuwachangia Wahanga
Zifuatazo ni baadhi ya Picha Za Sehemu Mbalimbali zilizokumbwa na Mafuriko, kwa hisani ya sources mbalimbali na hasa Michuzi Blog: Yeyote anayeweza kupata picha, ruksa kuzibandika. Tunaweza kuwasaidia ndugu zetu hawa kwa kutuma SMS yenye neno TPN kwenda 15522. Utakatwa TZS 250 tu za usajili...
www.jamiiforums.com