Pinda kukagua mafuriko Kilosa

Mpita Njia

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2008
Messages
7,011
Likes
35
Points
145

Mpita Njia

JF-Expert Member
Joined Mar 3, 2008
7,011 35 145


WAZIRI MKUU Mizengo Pinda leo mchana (Ijumaa, Januari 8, 2010) anatarajiwa kufanya ziara ya siku moja katika wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro kukagua athari za mafuriko na jitihada ambazo Serikali imefanya hadi sasa ili kuwasaidia waathirika wa maafa hayo.Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Waziri Mkuu ambaye anatokea Mpanda alikokuwa kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka, atapokewa eneo la VETA Mikumi na viongozi wa mkoa huo na kupatiwa taarifa ya maafa ya Mkoa kabla ya kuendelea na safari ya Kilosa.Akiwa Kilosa, Waziri Mkuu atatembelea eneo la Magomeni Kilosa na kusalimiana na wahanga na baadaye ataenda eneo la Machinjioni ambako ndiko kwenye chanzo cha tukio la mafuriko.Pia atakwenda Njia Sita (Kasiki) kukagua uharibifu uliotokea kwenye ’Pump House’ kabla ya kwenda soko la Mbumi kuangalia maafa yaliyolikumba kwenye eneo hilo. Vilevile atakwenda maeneo ya Behewa, Kimamba na Kondoa kuwapa pole wananchi wa maeneo hayo na kukagua nyumba zilizoharibiwa na mafuriko hayo.Wakati wa ziara hiyo, Waziri Mkuu atazuru pia kambi ya Shule ya msingi Kilosa Town na kuwapa pole wahanga walioko kwenye kambi hiyo ambako wamepatiwa hifadhi na Serikali.Mafuriko ya Kilosa yametokana na mvua hizo zilizoanza kunyesha Desemba 24, 2009 zilizosababisha maafa ya watu kufariki, kubomolewa kwa nyumba na miundombinu kama barabara, reli na madaraja hasa katika wilaya za Kilosa na Morogoro Vijijini kwa mkoa wa Morogoro na wilaya za Kongwa, Mpwapwa na Chamwino kwa mkoa wa Dodoma.Waziri Mkuu anatarajiwa kurejea jijini Dar es Salaam kesho (Jumamosi, Januari 9, 2010) mchana.(mwisho)

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

IJUMAA, JANUARI 08, 2010
 

Omumura

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2009
Messages
476
Likes
2
Points
35

Omumura

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2009
476 2 35
Huyu bwana amebobea kwenye masuala yote ya ukaguzi wa maafa na hasa mafuriko kama hayo ya kilosa,tutegee sikio atakalolipukanalo huko, may be anaweza sema kilosa sio nchi!!!
 

Forum statistics

Threads 1,191,220
Members 451,515
Posts 27,699,764