Pinda kakumbuka shuka asubuhi ampa rungu CAG | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda kakumbuka shuka asubuhi ampa rungu CAG

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Feedback, Jul 3, 2011.

 1. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amempa ‘rungu’, Mdhibiti na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu Hesabu za Serikali (CAG) la kuwafikisha moja kwa moja kwenye vyombo vya Dola, viongozi wa Serikali wanaoiba au kufuja fedha za umma.

  Kutokana na rungu hilo, sasa utaratibu wa awali wa CAG kusubiri kuwasilisha kwa Kamati za Bunge majina ya viongozi wa taasisi za Serikali zinazobainika kufuja au kuiba fedha za umma, ili kuwasilishwa bungeni umefutwa rasmi.

  Hii inaweza kuwa habari mbaya kwa viongozi wengi wa taasisi za umma, ambao wamekuwa wakitajwa bungeni, kwamba taasisi zao zimefanya manunuzi au kutumia fedha kinyume
  na taratibu, kwa vile kwa agizo hilo la Pinda, CAG atakuwa akiwafikisha kwenye vyombo vya Dola moja kwa moja.

  “Nachukua nafasi hii kumwagiza rasmi CAG, kwamba kwa zile taasisi ambazo atabaini kuwapo ubadhirifu wa fedha za umma, awafikishe moja kwa moja kwenye vyombo vya Dola wahusika wa ubadhirifu huo na si kusubiri kuwasilisha taarifa bungeni,” alisema Pinda.

  Katika majumuisho ya hotuba yake ya Makadirio ya Matumizi kwa mwaka huu wa fedha, bungeni juzi jioni, Pinda pia alisema Serikali haitakuwa na huruma kwa viongozi wa halmashauri ambao watabainika kufuja au kuiba fedha za umma.

  Alisema kutokana na mpango huo wa Serikali, kitengo cha ukaguzi wa ndani ambacho awali kilikuwa chini ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya, kimeondolewa katika ofisi hiyo na kuwa kitengo kinachojitegemea.

  Alisema kwa kuwa huru, kitengo hicho kitafanya ukaguzi wa matumizi ya fedha za umma zilizoelekezwa kwenye halmashauri husika bila kuwapo kwa mwingilio au ushawishi kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri na maofisa wake.

  Alisema tofauti na ilivyokuwa awali, sasa viongozi wa halmashauri watakaobainika kufuja
  fedha au kukosa maadili ya kazi, hawatahamishwa kutoka wilaya au halmashauri moja kwenda nyingine na badala yake watafukuzwa kazi na kufikishwa mahakamanimara moja.

  Aliwataka viongozi wa halmashauri na idara nyingine za Serikali kuanzia sasa kuweka
  hesabu zao sawa kila mara ili CAG anapofika akute hesabu hizo zipo tayari kwa kukaguliwa tofauti na ilivyo sasa ambapo CAG anapofika kwenye ofisi hizo ndipo viongozi wake wanaanza kuhaha kutafuta vielelezo vya hesabu za fedha.
   
 2. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Aanze na PPF, Halafu akimaliza awakague NSSF kwa kina tuwe na uhakika, halafu aende wizara ya fedha.
   
Loading...