Pinda Jiuzulu kazi imekushinda!

Wacha1

JF-Expert Member
Dec 21, 2009
16,682
8,233
Pinda Jiuzulu kazi imekushinda

pm1w.jpg

Pinda said:
“Iwapo mnataka kumchagua tena Rostam zingatieni amewafanyia nini katika ubunge wake. Msisikilize kile kinachosemwa bungeni juu yake. Bunge lina mambo yake, mimi kama Waziri Mkuu nafahamu mambo ya pale bungeni,” alisema Waziri Mkuu.

Huwezi kuwa waziri mkuu wakati huo huo unalidharau Bunge. Waziri mkuu Pinda ni wakati wako sasa wa kujiuzulu kwa kauli yako uliyoitoa na kulidhalilisha bunge. Kama huwezi kujiuzulu ni wajibu wa rais kukuwajibisha na kama JK hawezi kuchukua uamuzi huo ni jukumu la bunge kumpiga marufuku kuhudhuria vikao vya Bunge hadi atakapoomba msamaha kama sheria inaruhusu kuzingatia kanuni za Bunge.

23641905.jpg

Alipoapishwa hapo juu aliapa kuilinda katiba na sio marafiki na Mafisadi papa.

Je ni huyu Pinda ambaye tunamlipa bonge la fweza ambaye anakuja kulikashifu Bunge la Jamhuri?
 
miye nilishakata tamaa naye; madaraka ni kitu kibaya sana hasa yakiwa mikononi mwa watu kama yeye..
 
Mwacheni ndugu yetu angalau na sisi wakulima tumepata mtu anayefanana japo kidogo na sisi.

Hivi nyie mlitegemea Pinda alete mabadiliko gani? Mungepitia utendaji wake kwanza kule serikali za mitaa kabla ya kumfikiria kwamba angeweza kufanya makubwa.
 
waacheni vipofu wasaidiane kuvushana darajani, kamwe mchawi na mfuga majini hawezi ishi na mtu wa maombi,
maana si rahisi msemelezi kukaa na mtu mwizi
 
Uchambuzi wako ni mzuri sana, Pinda amelidharau Bunge. Wasiwasi wangu akiambiwa ajiuzuru atakimbilia kulia ili aonewa huruma.
 
Kinachoniuma sana kwenye ziara anatumia cheo cha uwaziri mkuu kupigia kampeni za kichama nikimaanisha hapo zinatumika pesa za walipa kodi kumpigia kampeni fisadi la chama. Je kwa nini asingemtuma kiongozi wa kichama kwenda kumpigia kampeni fisadi?

Katibu wa Bunge alisema Mawaziri wanalipwa na Serikali na hizo pesa ni za walalahoi.

Nashindwa kuelewa Mh. Waziri mkuu alikuwa anamaanisha nini.
 
Uchambuzi wako ni mzuri sana, Pinda kalidharau bunge. Wasiwasi wangu akiambiwa jiuzuru atakimbilia kulia ili aonewa huruma. RA bwana anajua kushika watu. Hata Mtikila na ujanja wake aliingia mtegoni. Sasa Pinda kisha nunuliwa rasmi na Fisadi kama muungwana alivyokamatwa vilivyo.
 
Yaelekea wote wamefirisika tu, hayo si maneno ya kusemwa na Waziri Mkuu (Kiongozi wa shughuli za "siri-kali" bungeni). Hatuna wa kutuokoa, kila mtu atajiokoa mwenyewe.
 
"Iwapo mnataka kumchagua tena Rostam zingatieni amewafanyia nini katika ubunge wake. Msisikilize kile kinachosemwa bungeni juu yake. Bunge lina mambo yake, mimi kama Waziri Mkuu nafahamu mambo ya pale bungeni," alisema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu aliendelea kusema .......nafahamu mambo ya pale bungeni ni ya UZUSHI na UMBEA wala msiwe mnayasikiliza sana......kaazi kweli kweli
 
Huyu mzee siyo fisadi isipokuwa anafikiria watu wote wako innocent kama yeye, hawezi ku-grasp kwamba sasa anatumika...yaani akili yake ni nzito kama kondoo inachukua muda mrefu sana kuelewa kinachoendelea...

Pinda dunia uwanja wa fujo bado uko usingizini unasafisha wasiosafishika
 
Tuliambiwa na JK na Pinda mwenyewe kwenye mikutano ya Bunge kuwa mswaada kuhusu kutengansha siasa na biashara upo njiani;na walituambia utapelekwa bungeni kwenye kikao kijacho cha Bunge ambapo wafanyabishara HAWATARUHUSIWA KUGOMBEA nafasi za kisiasa za kuchaguliwa!

Sasa kama Rostam Azizi anajulikana kuwa ni mfanyabiashara mkubwa,iweje PM Pinda audharua waraka aliotueleza wenyewe watz?Ndiyo kusema ule mswaada wa kukataza wafanyabishara kugombea hauletwi tena Bungeni kupitishwa na hatimaye Rais autie saini kuwa sheria?

Mwenye dondoo kuhusu mswaada huu please atueleze!
 
Tumaini, nakubaliana na wewe, ndiyo maana hatuhitaji wenye ubongo mzito kama wa kondoo kutuongoza katika dunia ambayo mambo yanakwenda mchaka mchaka.
 
Kwakweli nasikitishwa sana na viongozi wetu, kauli ya pinda ina maana kubwa zaidi ukiitafsiri kwa nadharia ya bunge kama wawakilishi wa wananchi; kwa maana hiyo pinda kasema wananchi wanawazulia majungu mafisadi! Maana bunge ni sauti ya wananchi wa tanzania!
 
Ni Kama kuotesha Mnazi halafu utegemee kuchuma embe kila mwisho wa mwaka, mlitegemea makuu kwa PINDA? swali dogo tu, pinda anawajibika kwa nani? ukipata jibu utajua kwa nini analialia Bungeni
 
Tuliambiwa na JK na Pinda mwenyewe kwenye mikutano ya Bunge kuwa mswaada kuhusu kutengansha siasa na biashara upo njiani;na walituambia utapelekwa bungeni kwenye kikao kijacho cha Bunge ambapo wafanyabishara HAWATARUHUSIWA KUGOMBEA nafasi za kisiasa za kuchaguliwa!

Sasa kama Rostam Azizi anajulikana kuwa ni mfanyabiashara mkubwa,iweje PM Pinda audharua waraka aliotueleza wenyewe watz?Ndiyo kusema ule mswaada wa kukataza wafanyabishara kugombea hauletwi tena Bungeni kupitishwa na hatimaye Rais autie saini kuwa sheria?

Mwenye dondoo kuhusu mswaada huu please atueleze!

Suala hapa si wasigombee bali watakapoamua kuwawakilisha wananchi basi waweke biashara zao pembeni kwa muda wote watakaokuwa wanawawakilishi wanancvhi bungeni ama kwenye councils.
 
Msiwe na akili za mbogo nyie.. Inamaana wananchi wa Igunga huyu sio waziri mkuu wao..? DO you really think that Rostam needs Pinda kwenda jimboni kwake ili ashinde?lol Ameapa kutumikia Jamhuri yote including Igunga so STFU!
 
Suala sio kushinda, ila ni kusafishwa. Kwamba kule Bungeni ni majungu tuu na umbea juu ya Rostam, according to Pinda.
 
miye nilishakata tamaa naye; madaraka ni kitu kibaya sana hasa yakiwa mikononi mwa watu kama yeye..
kukataa tamaa juu yake mwanakijijii ulikosea kwani ulikuwa unamlinganisha labda na wenzake na kupata matumaini ya muonekanoo wakee...
 
“Iwapo mnataka kumchagua tena Rostam zingatieni amewafanyia nini katika ubunge wake. Msisikilize kile kinachosemwa bungeni juu yake. Bunge lina mambo yake, mimi kama Waziri Mkuu nafahamu mambo ya pale bungeni,” alisema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu aliendelea kusema .......nafahamu mambo ya pale bungeni ni ya UZUSHI na UMBEA wala msiwe mnayasikiliza sana......kaazi kweli kweli

Hivi mwana wa mkulima Kayanza Pinda, zile fokafoka zote za akina Kilango kwa Bungeni kutachimbika ni porojo, uzushi na umbea! Sasa milioni 46 kama kinua mgongo ni kwa ajili ya kuongea mambo ya umbea na uzushi. Kama hivyo ndivyo basi nyote ni mafisadi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom