Pinda hongera,lakini... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda hongera,lakini...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Netanyahu, Feb 19, 2009.

 1. Netanyahu

  Netanyahu Senior Member

  #1
  Feb 19, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mizengo Pinda katika ziara yake mkoani Moshi alisema kuwa atajitahidi kukipa kipaumbele cha kwanza kilimo cha kisasa katika uongozi wake.

  Serikali ya makaburu ya Afrika ya kusini ilikuwa ikiitwa serikali ya wachache sababu ni serikali ambayo ilikuwa ikisimamia maslahi na maisha bora ya watu wachache yaani makaburu tu.Tanzania nayo kwa sasa imekuwa ni serikali ya watu wachache.Nasema hivyo kwa sababu asilimia 80 ya watanzania wanaishi vijijini na asilimia 20 wanaishi mijini,lakini inapokuja kwenye maslahi ya kijamii asilimia 20 ndio wanaopewa kipau mbele kwa barabara nzuri,hospitali nzuri,shule nzuri zilizosheheni walimu wengi,zenye madawati mazuri n.k na kero za watu wa mijini hupata majibu haraka haraka tofauti na wale wa vijijini.Hivyo serikali ya Tanzania ni ya wachache kama ilivyokuwa ya makaburu sababu sehemu kubwa ya Raslimali zake ikiwemo hata bajeti ya serikali hulenga zaidi maisha bora zaidi kwa wakazi wa mijini karibu katika kila eneo la huduma za jamii ikiacha ile asilimia 80 nje.

  Nyerere enzi zake ukikaribia uchaguzi alikuwa akisambaza vijana wake kila kona ya nchi mjini na vijijini kuwauliza kwa siri wanamuonaje ili ajue kama utawala wake ni wa walio wengi au ni wa walio wachache? Swali hili aliwahi kuuliza miaka ya mwanzo ya utawala wake na akajibiwa kuwa utawala wake ni wa walio wachache wa mijini.Ndipo akaamua kutaifisha mashule na kutoa elimu bure kuanzia shule za msingi hadi chuo kikuu ili watoto wa vijijini waliokuwa wengi kuliko wa mijini nao wapate upenyo wa kunyanyuka sawa na wale wa mijini ambao walikuwa na uwezo wa kujilipia enzi zile elimu inalipiwa.

  Sasa hivi serikali sijui kama inajiuliza swali hilo la kuwa ni yenyewe ni serikali ya walio wengi au wachache na kama viongozi nao je wanajiuliza kama wapo pale kwa maslahi ya walio wengi au wachache?

  Niliwahi kwenda mtaa wa kongo safari moja kwenye tafiti zangu binafsi za kukuza uelewa wangu wa binafsi wa mambo mbalimbali ya maeneo yanayonizunguka nikawahoji machinga kwa nini machinga wamefurika Dar es salaam na kuondoka kwao Mtwara.Mmoja akanijibu kuwa kilichowaleta mjini ni kuwa wao wamefuata jasho la wazazi wao.Wakaniambia kuwa walichogundua ni kuwa pesa nyingi za kigeni zilikuwa zinapatikana kutokana na wakulima kupitia mazao wanayolima kama vile korosho,chai,kahawa,pamba n.k lakini baada ya mapato hayo kupatikana yamekuwa yakitumiwa kujenga vitu vizuri kama hospitali,shule,barabara nzuri,n.k mijini. Kwa hiyo wao kama watoto wa wakulima wameona bora waende mijini kufaidi na wao jasho la wazazi wao.

  Ni miaka mingi imepita nilikuwa sijaenda Tanzania.Niliporudi nikaona nirudi tena Mtaa wa Congo niwasalimie machinga.Nilipofika nikakuta hawapo mtaa ule nikauliza mtu mmoja mwenye duka rafiki zangu wa miaka ile machinga wako wapi nikaambiwa halmashauri ya jiji iliamua kuwatoa kwa kuwajengea jengo lingine zuri sana la maghorofa linaloitwa MACHINGA COMPLEX .Nikagundua kuwa kumbe Machinga walikimbia Mtwara kuja mjini kufuata rushwa.si unaona sasa wamehongwa rushwa ya Machinga Complex katikati ya jiji?.

  Nikajua kumbe ndio maana machinga wengi wasomi waliozaliwa vijijini walikimbia vijijini kwenda mijini kuingia katika katika,siasa,ubunge,mahakama,ajira ya umma n.k kumbe wamefuata rushwa za kuwawezesha kuwa na machinga complex ili wakae watulie nao wale jasho la wazazi wao waache longo longo wabaki wakiongelea mambo ya mjini na ya kumpongeza mheshimiwa Meya wa jiji na mkuu wa Mkoa Abbasi Kandoro na serikali waaache kuongelea matatizo ya Mtwara na mikoa kama hiyo na vijiji vya Tanzania.After all pilipili iko shamba inawawashia nini wakati tayari wana Machinga Complex zao mijini,magari ya kifahari,n.k.

  Nikajiuliza ni lini serikali itakuwa serikali ya watu wengi na itajenga Machinga Complex Mtwara vijijini na vijiji vingine Tanzania kwa wakulima wa korosho,chai,kahawa,mahindi,mpunga n.k ili na wao wawe na majengo mazuri ya ku-kuprocess,kuhifadhi na kuuzia korosho zao yanayokidhi viwango vya kimataifa? Au hizo Machinga Complex nazo ni kwa wakazi wa mijini tu(Wale asilimia 20).Au Complex vijijini hazitakiwi nini? Au serikali ya wachache haipendi hayo?


  Anyway labda kwa kuwa Pinda kasema atakipa kipaumbele kilimo nafikiri labda serikali sasa imezinduka na inaamua kuwa serikali ya walio wengi pia (ile asilimia 80 ya wakazi wa vijini) badala ya kuwa ya wachache (wale asilimia 20 wakazi wa mijini).

  Tusubiri.Tunaposubiri wacha angalau tu nimpe pongezi Mheshimiwa Pinda japo kwa huko kutamka .

  Mwenye macho haambiwi tazama.Macho yetu yanasubiri kitakachofuata baada ya hizo kauli. Tunampa pongezi kwa kauli LAKINI tunasubiri utekelezaji.Lakini kama serikali itaendelea kuwa ya wachache (asilimia 20) iko siku walio wengi (asilimia 80) wataamua kuitimua madarakani serikali ya wachache kama makaburu walivyotimuliwa kwa kuwa walikuwa hawawakilishi maslahi ya walio wengi bali wachache.
   
Loading...