Pinda: Hatutakurupuka kuwakamata mafisadi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,004
Utawala wa sheria ni applicable kwa vingunge tu wanapofanya ufisadi? :confused: Mbona makapuku wanakamatwa kila kukicha na kuozea rumande?

Pinda: Hatutakurupuka kuwakamata mafisadi

na Mwandishi Wetu, Iringa
Tanzania Daima~Sauti ya watu

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, amesema serikali inawashughulikia watuhumiwa wa rushwa na wizi kwa kuzingatia sheria na taratibu na si kukurupuka tu na kuwasweka ndani kama baadhi ya watu wanavyotaka.

"Kamatakamata, funga, funga funga ni kinyume cha sheria…watuhumiwa watakaobanika ni wahalifu itabidi kwanza wafikishwe mahakamani ili wahukumiwe kwa mujibu wa sheria na si kuwahukumu kabla," alisema.

Alikuwa akizungumza katika hafla ya kumuweka wakfu Askofu Mteule, John Simalenga kuwa Askofu wa Dayosisi ya Kusini Magharibi mwa Tanganyika ya Kanisa Anglikana, mjini Njombe, mkoani Iringa, juzi.

Pinda alisema haiwezekani kuwashughulikia watuhumiwa wa rushwa na wizi kwa kuwakamatakamata na kuwasweka ndani bila ya kufuata sheria, kwa sababu Tanzania inazingatia utawala wa sheria na inasisitiza utawala bora.

Alitoa kauli hiyo baada ya Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Mhashamu Dk. Valentino Mokiwa, kusema katika sherehe hiyo kuwa serikali inaonekana kama vile haichukui hatua zinazostahili kwa watuhumiwa wa rushwa na wizi nchini.

"Serikali inashughulikia matatizo hayo kwa nguvu zake zote, lakini lazima izingatie sheria, kanuni na taratibu," alisisitiza Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu pia aliwataka viongozi wa dini waendelee kuhimiza uadilifu kwa waumini wao, ili kupunguza kasi ya kuenea kwa ukimwi na wasiilaumu serikali kwa kusisitiza kwa watu wote ngono salama.

Alisema pamoja na kuwa kiwango cha maambukizi kimeshuka kitaifa na kufikia asilimia 5.8 mwaka huu ikilinganishwa na asilimia 7 mwaka 2003/4, bado kiwango hicho si cha kujivunia.

Mkoa wa Iringa unaongoza kwa maambukizi ya ukimwi kwa kiwango cha asilimia 15.7, alisema akinukuu matokeo ya uchunguzi wa hivi karibuni nchini. Mikoa mingine yenye viwango vikubwa ni Dar es Salaam asilimia 9.3; Mbeya (9.2); Mara (7.7); Shinyanga (7.4); Pwani (6.7); Tabora (6.4) na Ruvuma (5.9).

Askofu Simalenga aliyewekwa wakfu alichaguliwa kuwa Askofu Mteule wa Dayosisi ya Kusini Magharibi Tanganyika ya Kanisa la Anglikana Juni 3, mwaka huu.

Anakuwa askofu wa saba wa dayosisi hiyo iliyoanzishwa mwaka 1952 na makao yake kuwa Njombe. Dayosisi hiyo inajumuisha wilaya za Njombe, Ludewa, Makete, Mafinga na Kilombero.
 
teh teh teh, Pinda eeh, hamtakurupuka au hamtawakata kabisa?
 
Tumeshachoshwa na porojo zako Pinda.Naona umepinda kama jina lako linavyo suggest.Huyu jamaa he is a damn loser hana jipya yaleyale ya kila siku and we all know he is a coward just like the top guy.Wanawajua na tangu wamewajua wamefanya lipi kama sio umbea tuu?Pinda concentrate on your health my dear achana na politics hazikufai.Huna agenda weye.
 
Anajenga uhalali wa na mazingira ya kuzembea.

Eti kisingizio ni "Rule of Law" mbona mnakalia ripoti na tume zinazoficha ukweli hamjawa subpoena watu kufuata "rule of law" ?

Kukurupuka bila kufuata rule of law and due process ni kubaya kama vile kusinzia bila kuheshimu these same two tenets of justice.

Just like in vehicular traffic, overspeeding as well as underspeeding can kill you.
 
Hahaaha jamani hii watendaji wakuu wa serikali hii naifananisha na joka la maonyesho(kibisa)
 
Back
Top Bottom