Pinda hastahili kuwa PM, si mbunge wa kuchaguliwa

Salim aliteuliwa kuwa mbunge na Nyerere kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu hakuwa mbunge wa kuchaguliwa.

Mbona hiyo ilikuwa zamani sana. Uko nyuma sana mkuu. Katiba inasema "....Rais atamteua Mbunge wa kuchaguliwa kutoka katika Jimbo la Uchaguzi anayetokana na chama cha siasa chenye Wabunge wengi zaidi Bungeni..." Sasa wakati wa Nyerere kulikuwa na vyama vingapi vya siasa?
 
Kwa mujibu wa katiba yetu kuna Ubunge wa aina tatu tu:
1)Ubunge wa kuchaguliwa
2)Ubunge wa kuteuliwa
3)Ubunge wa Mwanasheria Mkuu.
Utaona Pinda ni mbunge wa kuchaguliwa.

Mkuu unaweza ukawa right, kama ni mbunge wa kuchaguliwa, alichaguliwa lini na akina nani? Katika uchaguzi uliopita kuna mtanzania yoyote alipyepiga kura ya kumchagua au kutomchagua Pinda kama Mbunge? Lakini kwa upande mwingine, kwa nini ateuliwe kura waziri kwa simply because vyama vya upinzani havikuweka mgombea huko jimboni kwake?

Issue imekaa kiaina, lakini objectively, sioni kwa nini ahukumiwe kwa sababu ya weakness ya upinzani kutoweka mgombea ubunge. Na hata kama wangeweka still angeshinda anyway.
 
Katika Tanzania hii Rais hawezi kumteua waziri mkuu mtu aliyemzidi kwa akili na utendaji (competence).

Hana cha kupoteza tena - he has nothing to lose anymore - na hata makamu wake anayevaa miwani 'tinted' ni profesa wa nyuklia(uranium?)!
 
Mkuu unaweza ukawa right, kama ni mbunge wa kuchaguliwa, alichaguliwa lini na akina nani? Katika uchaguzi uliopita kuna mtanzania yoyote alipyepiga kura ya kumchagua au kutomchagua Pinda kama Mbunge? Lakini kwa upande mwingine, kwa nini ateuliwe kura waziri kwa simply because vyama vya upinzani havikuweka mgombea huko jimboni kwake?

Issue imekaa kiaina, lakini objectively, sioni kwa nini ahukumiwe kwa sababu ya weakness ya upinzani kutoweka mgombea ubunge. Na hata kama wangeweka still angeshinda anyway.

Mkuu una-point kisasi. Lakini inaonekana kama Kayanza Pinda ni mbunge anayewakilisha jimbo. Sijui katiba yetu inamuweka wapi mbunge aliyepita bila kupingwa na kuwakilisha jimbo. Je anakuwa ni mbunge wa kuteuliwa na wananchi? au nni mbunge wa kuchaguliwa? Inawzekana kuwa katiba yetu iko bubu kwenye issue hiyo. Tusibiri kuona hali itakuwaje.
 
Pinda kachaguliwa na wananchi wao ndio maana hakuna mwananchi yeyote aliyejitokeza kumpinga. Pinda atakuwa waziri mkuu, kwamfano lowasa alipoteuliwa kuwa waziri mkuu huko jimbon kwake alipita bila kupingwa kwa term kama mbili hivi.

Ulitaka jina lake liwepo kwenye karatas ya kupigia kura?halaf anacontend na nan?kivuli! Ubadhirifu huo,acha kupinga kila ki2 kwa kujifanya unajua
 
so jimboni kwake kulifanyika uchaguzi wa raisi tu na madiwani..?
 
Mkuu una-point kisasi. Lakini inaonekana kama Kayanza Pinda ni mbunge anayewakilisha jimbo. Sijui katiba yetu inamuweka wapi mbunge aliyepita bila kupingwa na kuwakilisha jimbo. Je anakuwa ni mbunge wa kuteuliwa na wananchi? au nni mbunge wa kuchaguliwa? Inawzekana kuwa katiba yetu iko bubu kwenye issue hiyo. Tusibiri kuona hali itakuwaje.

Wakuu nafikiri nimepata jibu. Kifungu cha 44 cha Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 1985 kinadeal na unoposed candidates. Kifungu hiki kiliongezwa kwenye hii sheria mwaka 1995 nafikiri kwa ajili ya mfumo wa vyama vingi. Kifungu kinanasema na ninanukuhu: "Where only one candidate is nominated for an election in a constituency, such candidate shall be be deemed to be elected and the Commission shall by notice in the Gazette, declare him to have been elected."

http://www.tz.undp.org/ESP/docs/Legal_Documents/Tanzania_Elections_Act 1985_(dated 30 June 2005).PDF
 
Pinda, January Makamba na hao wote wanaoitwa wabunge waliopita bila kupingwa actually si wabunge.

Kwenye thread moja ya kumhusu January Makamba nilishawahi kugusia uvunjwaji wa katiba unaofanyika kwa kuwaingiza watu bungeni bila kuchaguliwa na watu au kuteuliwa kama ilivyoainishwa katika katiba. Swala zima la mgombea kupita bila kupingwa halina msingi katika katiba, na kwa kweli linavunja katiba.

Kifungu cha 66 cha katiba kinaainisha wabunge ifuatavyo

66.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengine ya ibara hii, kutakuwa na aina zifuatazo za Wabunge, yaani-

(a) Wabunge waliochaguliwa kuwakilisha majimbo ya uchaguzi;

(b) Wabunge wanawake wa idadi inayoongezeka, kuanzia asilimia ishirini ya Wabunge waliotajwa katika aya ya (a), (c ) na (d), itakayotajwa mara kwa mara na Tume ya Uchaguzi kwa taarifa iliyochapishwa katika Gazeti la Serikali baada ya kupata kibali cha Rais,watakaochaguliwa na vyama vya siasa vinavyowakilishwa Bungeni, kwa mujibu wa ibara ya 78, na kwa kuzingatia masharti ya uwiano wa uwakilishi baina ya vyama hivyo;

(c) Wabunge watano waliochaguliwa na Baraza la Wawakilishi kutoka miongoni mwa wajumbe wake;

(d) Mwanasheria Mkuu;

(e) Wabunge wasiozidi kumi walioteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa kwa mujibu wa ibara ya 67, isipokuwa sifa iliyotajwa katika ibara ya67(1)(b).
Sasa Pinda, Makamba na wengine "waliopita bila kupingwa" wana qualify katika aina gani kati ya haya?

Tumeona Nyamagana walivyotaka kumpitisha Masha bila kupingwa kwa hila, mwisho wake aliposhindwa kufanya hivyo tumejua kumbe watu hawamtaki.

Hawa watu si wabunge, basi tu Tanzania hamna strict constitutionalists.

Lakini unategemea nini wakati rais wa Tanzania kashawahi kumpa Augustine Mrema unaibu Waziri Mkuu ambao hata haukuwapo kikatiba, na hakuna mtu yeyote aliyesema neno kuhusu hilo.
 
Luteni ina maana pinda kapata 100 % ya wapiga kura wa jimboni kwake. Kama hakujitokeza mtu wa kupambana naye sasa yeye afanye nini?

Hii issue ipo technical kweli. Anachosema Luteni ni kuwa kama kachaguliwa 100% ni kwa ushahidi upi? kura za urais zimetaja hadi asilimia 0.15 alizopata Mziray, hii ina maana kujenga uhalali wa uchaguzi. Vinginevyo Jaji Makame angesema mshindi ni JK wa pili...,tatu...., lakini kisheria ilibidi aweke evidence.

Sasa Pinda akiulizwa alichaguliwa na nani na kwa kura ngapi atasemaje 100% ili hali tunajua upo uwezekano wa kura kuharibika!

La Dr Shein nalo ni technical, alipigaje kura TZ bila kupiga kura ya kumchagua rais wa Zanzibar! ili hali sheria inamtaka mtu awe na miaka 5 Zanzibar?

Wanasheria tusaidieni.
 
Wakuu nafikiri nimepata jibu. Kifungu cha 44 cha Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 1985 kinadeal na unoposed candidates. Kifungu hiki kiliongezwa kwenye hii sheria mwaka 1995 nafikiri kwa ajili ya mfumo wa vyama vingi. Kifungu kinanasema na ninanukuhu: "Where only one candidate is nominated for an election in a constituency, such candidate shall be be deemed to be elected and the Commission shall by notice in the Gazette, declare him to have been elected."

http://www.tz.undp.org/ESP/docs/Legal_Documents/Tanzania_Elections_Act 1985_(dated 30 June 2005).PDF

Hata kama sheria zinanyumbulisha katiba, kwa maana ya kwamba katiba ni sheria mama na haiwezi kuelezea kila kitu in great detail, lakini sheria zinazoelezea zaidi pale ilipoishia katiba ziwe zimejikita katika msingi wa katiba.

Huwezi kuwa na katiba inasema Tanzania ni nchi ya kiislamu na rais lazima awe Alhaji, halafu ukawa na sheria inayosema kasisi naye anaweza kuwa rais. Sheria zote zinatakiwa zi converge kwenye katiba, kwa sababu katiba ni sheria mama. Sasa katika hili unaona wazi kabisa katiba imeshaweka wigo wa jinsi gani mbunge anapatikana, kwa kupitia kifungu cha 66, halafu inakuja sheria inayotoka nje ya katiba kabisa, na ku introduce kitu ambacho hakipo kwenye katiba kabisa.

Hii sheria imevunja katiba na inatakiwa kuondolewa, hao wagombea wanaoitwa wamepita bila kupingwa wapigiwe kura za "NDIYO" au "HAPANA". Mbona enzi za chama kimoja tuliwapigia watu kura hizi, what's the big deal kufanya hivi sasa? Zaidi ya kuwapa wananchi nafasi ya kuwapigia kura wagombea, tutawapa nafasi wagombea kupigiwa kura na wananchi, kwa maana nyingine mfumo wa sasa unamnyima mgombea legitimacy fulani hivi, hata kama mgombea anakubalika kwa 99% hatuwezi kujua kwa sababu hapigiwi kura.
 
"Where only one candidate is nominated for an election in a constituency, such candidate shall be be deemed to be elected and the Commission shall by notice in the Gazette, declare him to have been elected."

Nadhani hii inahitaji kuwekwa wazi zaidi kwani kuna ujikanganya kwingi hapa. Kama thinkers tutoe tathmini objectively. Pamoja nakuwa wakati wa chama kimoja kulikuwa na mgombea 1 wa urais na kivuli bado wananchi walipiga kura. Deemed to be elected ni kasoro iliyowekwa na wadau wavivu walioruhusu provision hiyo kwenye katiba. Suppose kuna wapiga kura 20,000, mgombea kapita bila kupingwa lakini anakubalika na wapiga kura 1000 tu kati ya 20,000. Je hapa ni sawa?

There is a lacuna in the constitution amabayo imetumika vibaya mwaka huu wengine waliwashawishi wapinzani kujitoa, wengine kufanya ubabe ili wasipate wapinzani HASA MASHA tumeona ukweli wake tungedahani ndiye chaguo la wananchi kumbe sivyo.
 
Pinda, January Makamba na hao wote wanaoitwa wabunge waliopita bila kupingwa actually si wabunge.

Kwenye thread moja ya kumhusu January Makamba nilishawahi kugusia uvunjwaji wa katiba unaofanyika kwa kuwaingiza watu bungeni bila kuchaguliwa na watu au kuteuliwa kama ilivyoainishwa katika katiba. Swala zima la mgombea kupita bila kupingwa halina msingi katika katiba, na kwa kweli linavunja katiba.

Kifungu cha 66 cha katiba kinaainisha wabunge ifuatavyo

Sasa Pinda, Makamba na wengine "waliopita bila kupingwa" wana qualify katika aina gani kati ya haya?

Tumeona Nyamagana walivyotaka kumpitisha Masha bila kupingwa kwa hila, mwisho wake aliposhindwa kufanya hivyo tumejua kumbe watu hawamtaki.

Hawa watu si wabunge, basi tu Tanzania hamna strict constitutionalists.

Lakini unategemea nini wakati rais wa Tanzania kashawahi kumpa Augustine Mrema unaibu Waziri Mkuu ambao hata haukuwapo kikatiba, na hakuna mtu yeyote aliyesema neno kuhusu hilo.

Mkuu,

Kwanza kabisa inabidi tuelewe kuwa Katiba sio sheria pekee ya Tanzania. Katiba ni sheria mama lakini kuna sheria nyingine ambazo zinaimplement Katiba. Ndio maana unakuta ibara nyingi kwenye Katiba yetu zinaanza kwa kusema "Subject to other laws" au "Bila kuathiri sheria nyingine za nchi".. Hata kifungu cha Katiba ulichoquote kinasema "Bila ya kuathiri masharti mengine ya ibara hii". Kama nilivyosema hapo juu Kifungu cha 44 cha Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 1985 kinasema kuwa:

"Where only one candidate is nominated for an election in a constituency, such candidate shall be be deemed to be elected and the Commission shall by notice in the Gazette, declare him to have been elected.".

Sasa hapo sijui kama kuna tatizo. Unless tatizo liwe ni sheria yenyewe ambayo ni issue nyingine tofauti. Kwa hiyo kisheria hao akina Pinda, Makamba, nk ni wabunge wa kuchaguliwa na Pinda anaweza kuwa waziri mkuu.
 
Hii issue ipo technical kweli. Anachosema Luteni ni kuwa kama kachaguliwa 100% ni kwa ushahidi upi? kura za urais zimetaja hadi asilimia 0.15 alizopata Mziray, hii ina maana kujenga uhalali wa uchaguzi. Vinginevyo Jaji Makame angesema mshindi ni JK wa pili...,tatu...., lakini kisheria ilibidi aweke evidence.

Sasa Pinda akiulizwa alichaguliwa na nani na kwa kura ngapi atasemaje 100% ili hali tunajua upo uwezekano wa kura kuharibika!

La Dr Shein nalo ni technical, alipigaje kura TZ bila kupiga kura ya kumchagua rais wa Zanzibar! ili hali sheria inamtaka mtu awe na miaka 5 Zanzibar?

Wanasheria tusaidieni.

Kura za rais ni za rais wala si za mbunge, hakuna sehemu ya kifungu cha 66 kinachoainisha wabunge inayosema lolote kuhusu mbunge kupita bila kupingwa, wala kura za rais kutumika.

Kifungu kinataja "wabunge waliochaguliwa kuwakilisha majimbo ya uchaguzi". Pinda kachaguliwa na nani ? Pinda si mbunge na hana sifa hata za kuingia mjengoni kama muwakilishi wa wananchi, achilia mbali uwaziri mkuu.
 
Wana sheria tudadavulieni haya kwenye media live wananchi wajue, moja Dr. Shein kupiga/kutopiga kura na pili Pinda haqualify kuwa waziri mkuu. Haya ndio mapungufu yatakayo haribu mambo baadae yawekwe wazi.
 
Mkuu,

Kwanza kabisa inabidi tuelewe kuwa Katiba sio sheria pekee ya Tanzania. Katiba ni sheria mama lakini kuna sheria nyingine ambazo zinaimplement Katiba. Ndio maana unakuta ibara nyingi kwenye Katiba yetu zinaanza kwa kusema "Subject to other laws" au "Bila kuathiri sheria nyingine za nchi".. Hata kifungu cha Katiba ulichoquote kinasema "Bila ya kuathiri masharti mengine ya ibara hii". Kama nilivyosema hapo juu Kifungu cha 44 cha Sheria ya Uchaguzi ya mwaka 1985 kinasema kuwa:

"Where only one candidate is nominated for an election in a constituency, such candidate shall be be deemed to be elected and the Commission shall by notice in the Gazette, declare him to have been elected.".

Sasa hapo sijui kama kuna tatizo. Unless tatizo liwe ni sheria yenyewe ambayo ni issue nyingine tofauti. Kwa hiyo kisheria hao akina Pinda, Makamba, nk ni wabunge wa kuchaguliwa na Pinda anaweza kuwa waziri mkuu.

I anticipated this line of thought, soma nimejibu swali lako hata kabla hujaliraise katika post yangu namba 31 hapo juu.

Ukishasema katiba ni sheria mama, maana yake katiba ni sheria inayotoa muongozo kwa sheria nyingine zote.

Sheria inayotoa muongozo kwa sheria zote nyingine ikishasema mbunge ni lazima achaguliwe na watu, ateuliwe na rais au awe mbunge kutokana na nominations za baraza la wawakilishi na kinamama pamoja na viti maalum, bila kusema chochote kuhusu kupita bila kupingwa, ukija kusema habari za kupita bila kupingwa unakuwa umeongeza kitu ambacho sheria mama haikukisema.

Sheria zinatakiwa kuelezea zaidi vitu vilivyopo katika katiba, sio ku introduce vitu vipya kabisa ambavyo hata havipo wala kuwa na msingi katika katiba, ukiintroduce vitu vipya maana ya katiba ni nini sasa?

Hii sheria kama ingefanyiwa DNA test ionekane kama imezaliwa kihalali kutoka katika katiba ingefail, haijatokana na katiba na kwa kweli inavunja katiba.
 
Kura za rais ni za rais wala si za mbunge, hakuna sehemu ya kifungu cha 66 kinachoainisha wabunge inayosema lolote kuhusu mbunge kupita bila kupingwa, wala kura za rais kutumika.

Kifungu kinataja "wabunge waliochaguliwa kuwakilisha majimbo ya uchaguzi". Pinda kachaguliwa na nani ? Pinda si mbunge na hana sifa hata za kuingia mjengoni kama muwakilishi wa wananchi, achilia mbali uwaziri mkuu.

Kiranga, soma vizuri nilichosema. Nimetaja kura za urais kama mfano na wala si mwingiliano. soma tena maelezo yangu utanielewa vizuri.
 
Kwa nini unafikiri sijaelewa ulichoandika mpaka nirudie kusoma?
 
Nadhani hii inahitaji kuwekwa wazi zaidi kwani kuna ujikanganya kwingi hapa. Kama thinkers tutoe tathmini objectively. Pamoja nakuwa wakati wa chama kimoja kulikuwa na mgombea 1 wa urais na kivuli bado wananchi walipiga kura. Deemed to be elected ni kasoro iliyowekwa na wadau wavivu walioruhusu provision hiyo kwenye katiba. Suppose kuna wapiga kura 20,000, mgombea kapita bila kupingwa lakini anakubalika na wapiga kura 1000 tu kati ya 20,000. Je hapa ni sawa?

There is a lacuna in the constitution amabayo imetumika vibaya mwaka huu wengine waliwashawishi wapinzani kujitoa, wengine kufanya ubabe ili wasipate wapinzani HASA MASHA tumeona ukweli wake tungedahani ndiye chaguo la wananchi kumbe sivyo.

Mkuu,

Upo sahihi kabisa. Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi ya mwaka 1985, Pinda ni mbunge wa kuchaguliwa. Ila kama ulivyosema hii sheria ina walakini. Sio tuu issue ya kama mgombea mwenyewe anakubalika na wapiga kura wangapi bali pia hii sheria inaweza kuleta mazingira ya rushwa.

Sina maana kuwa Pinda na wenginao wamehonga ili wagombee unoposed. Lakini tumesikia tetesi kuwa baada ya kura kuhesabiwa baadhi ya wagombea walioshindwa walikuwa tayari kuwahonga walionshida ili wao watangazwe washindi.

wasiwasi kwenye uchaguzi ujao wagombea watakaona kuwa wanakaokabiliwa na upinzani mkali wataanza kuwahonga wapinzani wao wajitoe kabla ya uchaguzi kufanyika ili wao waingombee unoposed. Au wahuni wanaweza kugombea ubunge kwa nia ya kutaka kuhongwa ili wajitoe.
 
pinda ni mbunge wa kuchaguliwa anayetokana na jimbo la uchaguzi la mlele. alichaguliwa kwa kupita bila kupingwa, say alichaguliwa kwa asilimia 100
 
Back
Top Bottom