Pinda hastahili kuwa PM, si mbunge wa kuchaguliwa

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
302
51​
.-(1) Kutakuwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano atakayeteuliwa na Rais kwa kufuata masharti ya ibara hii na ambaye kabla ya kushika madaraka yake ataapa mbele ya Rais kwa kiapo kinachohusika na kiti cha Waziri Mkuu kitakachowekwa na Bunge.
(2) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile ndani ya siku kumi na nne, baada ya kushika madaraka yake, Rais atamteua Mbunge wa kuchaguliwa kutoka katika Jimbo la Uchaguzi anayetokana na chama cha siasa chenye Wabunge wengi zaidi Bungeni au kama hakuna chama cha siasa chenye Wabunge wengi zaidi, anayeelekea kuungwa mkono na Wabunge walio wengi kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, naye hatashika madaraka hayo mpaka kwanza uteuzi wake uwe umethibitishwa na Bunge kwa azimio litakaloungwa mkono na kura za Wabunge

walio wengi.
 
afadhali...
Manake bunge lile la ndio mzee alimwaga chozi na makamasi.

Je hili la kamanda Tundu Lissu?
 
Duuh aisee hii issue ni very technical kwa kweli. Hebu tuone huyo mwanasheria mkuu atamshauri vipi JK hii issue....!
 
Kwa mujibu wa katiba yetu kuna Ubunge wa aina tatu tu:
1)Ubunge wa kuchaguliwa
2)Ubunge wa kuteuliwa
3)Ubunge wa Mwanasheria Mkuu.

Utaona Pinda ni mbunge wa kuchaguliwa.
 
mkuu kwani jimboni kwake pinda hawajapiga kura za ubunge sio?
Ni mmoja kati ya wabunge waliopita bila kupingwa hakuna uchaguzi wa ubunge uliofanyika jimboni kwake nafikiri hata karatasi za kura hazikuwepo, it means no single vote was casted i.e ZERO votes, huyu kweli ataitwa mbunge wa kuchaguliwa akiulizwa amechaguliwa kwa kura ngapi atasemaje.
 
Pinda anarudi kwenye nafasi yake ya uwaziri mkuu kwa sababu atakuwa tishio kwa mtu ambaye JK atataka amrithi na kama atambadilisha atampa atakaye kuwa mrithi wake.
 
Kwa mujibu wa katiba yetu kuna Ubunge wa aina tatu tu:
1)Ubunge wa kuchaguliwa
2)Ubunge wa kuteuliwa
3)Ubunge wa Mwanasheria Mkuu.
Utaona Pinda ni mbunge wa kuchaguliwa.
Kwa kura ngapi? labda awe kwenye kundi la wabunge wa viti maalum (wanawake).
 
haya tutaona lkn hawa jamaa hii katiba huwa wanaiunga wenyewe lkn hawaifuati............znz walisea mpiga kura lazima awe ameishi kwenye eneo kwa muda wa miaka 5 ndio atakuwa na uhalali wa kufanya hivyo lkn shein kura pia kapiga da lkn ndio rais wao................hi tz imekwisha usanii mtupu.
 
Ni mmoja kati ya wabunge waliopita bila kupingwa hakuna uchaguzi wa ubunge uliofanyika jimboni kwake nafikiri hata karatasi za kura hazikuwepo, it means no single vote was casted i.e ZERO votes, huyu kweli ataitwa mbunge wa kuchaguliwa akiulizwa amechaguliwa kwa kura ngapi atasemaje.

kama ni hivyo anakosa uhalali wa kuchaguliwa ila waitafsiri kw maana nyengine hiyo katiba yao feki................maana hii mijamaa haichelewi kuja na kiwahili chao cha uzushi.kama kura haijapigwa that means hakuna uchaguzi na ikiwa hakuna uchaguzi that means jamaa hajachaguliwa sio.
 
haya tutaona lkn hawa jamaa hii katiba huwa wanaiunga wenyewe lkn hawaifuati............znz walisea mpiga kura lazima awe ameishi kwenye eneo kwa muda wa miaka 5 ndio atakuwa na uhalali wa kufanya hivyo lkn shein kura pia kapiga da lkn ndio rais wao................hi tz imekwisha usanii mtupu.
Unasema hawaifuati katiba lakini ujatuonyesha ni wapi wamevunja katiba!
 
Ni wapi kwenye katiba inasema mbunge wa kuchaguliwa lazima apigiwe kura jimboni kwake.
Hivi sentensi hii ina maana gani:

'Rais atamteua Mbunge wa kuchaguliwa kutoka katika Jimbo la Uchaguzi'
 
Ni mmoja kati ya wabunge waliopita bila kupingwa hakuna uchaguzi wa ubunge uliofanyika jimboni kwake nafikiri hata karatasi za kura hazikuwepo, it means no single vote was casted i.e ZERO votes, huyu kweli ataitwa mbunge wa kuchaguliwa akiulizwa amechaguliwa kwa kura ngapi atasemaje.

Luteni ina maana pinda kapata 100 % ya wapiga kura wa jimboni kwake. Kama hakujitokeza mtu wa kupambana naye sasa yeye afanye nini?
 
Salim aliteuliwa kuwa mbunge na Nyerere kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu hakuwa mbunge wa kuchaguliwa.
 
ni ile aliyoisaini jk ya sheria ya uchaguzi waliifuata mkuu kwani ile wakati wa uchaguzi na waliisaini wenyewe?
Ninaongelea katika context ya ulichoandika hapa chini.
haya tutaona lkn hawa jamaa hii katiba huwa wanaiunga wenyewe lkn hawaifuati............znz walisea mpiga kura lazima awe ameishi kwenye eneo kwa muda wa miaka 5 ndio atakuwa na uhalali wa kufanya hivyo lkn shein kura pia kapiga da lkn ndio rais wao................hi tz imekwisha usanii mtupu.
 
Hapo ccm lazima wakwambie Pinda kapita bila kupingwa kwa sababu hata hao wapinzani wamemchagua
 
Back
Top Bottom