Pinda azuia kufanyika kwa chaguzi za serikali za mitaa

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,796
12,239
Kwa mujibu wa kiongozi wa upinzani rasmi bungeni Mhe. Mbowe ni kwamba Pinda amezuia kufanyika kwa chaguzi za serikali za mitaa nchini hadi hapo CCM itakapomaliza chaguzi zake ndani ya chama! Mbowe amesema huku ni kubaka demokrasia na kuzorotesha maendeleo nchini. Tayari mkoa wa mara umesimamisha chaguzi zote mkoani huko!

Aidha Mbowe amesema Pinda amesimamisha chaguzi kwa woga wa CCM kupoteza nafasi nyingi za uongozi wa serikali za mitaa kwa vyama makini vya upinzani! Mbowe alikuwa anachangia hotuba ya bajeti ya Pinda.

Tafakari!

Source: live broadicasting TBC yesterday (5.00 - 7.40pm)
 
mzee anayeendeshwa na chama na siyo busara anabaka democrasia waziwazi...hawa wanatakiwa kupumzika...lakini kwa sababu hawajui la kufanya wanang'ang'ana tu kwenye siasa mpaka wanaanza kusemwa vibaya sasa shauri yake...afuate mwenendo wa Dr. Chrisant maji ya Tanga Mzee Ngakaya
 
mzee anayeendeshwa na chama na siyo busara anabaka democrasia waziwazi...hawa wanatakiwa kupumzika...lakini kwa sababu hawajui la kufanya wanang'ang'ana tu kwenye siasa mpaka wanaanza kusemwa vibaya sasa shauri yake...afuate mwenendo wa Dr. Chrisant maji ya Tanga Mzee Ngakaya
CCM imeshikwa pabaya!
 
Mr Mbowe, Waache wamalize hizo chaguzi zao wakae mkao wa kujiamini then waje wakutane na watanzania waone game ilivyo upande usio wao. Wataondoka kuanzia huko mitaani hadi Magogoni, here we are time will tell.
 
Huu ni upumbavu, udhaifu, upuuzi na ujinga wa CCM! Hawa watu wanatakiwa wapimwe akili chama kikongwe mpaka wanachama wake na viongozi akili zao zimechakaa na zimekuwa kongwe pia, Magamba mnachekesha!
 
HAKIKA HAYA NI MAGAMBA KWELIKWELI! yaani yanadhani bado yapo kwenye mfumo wa chama kimoja!
 
Huwezi kuzuia risasi kwa kukinga na mkono, wala huwezi zuia mvua ya mawe kwa jani bichi la mgomba, twende kazi
 
Pinda anaogopa Kipigo cha mwizi dalili sio nzuri
Misenyi- Chadema wamechukua
Chato=Chadema wamechukua
Geita- Chadema wamechukua
Sengerema-Chadema wamechukua
Kisarawe-Chadema wamechukua
Shinyanga-Chadema wamechukua
Mbeya vijijini-Chadema wamechukua huko kote ni ngazi ya vijiji na mitaa ,huko ndiko siku zote walikuwa wanajidai nak sasa wananchi wamekataa katakata kuibeba CCM kwa nini asiogope,lakini mdharau mwimba mwisho mguu huota tende
 
Duh kweli ngumi zimezidi!
Sura yote ni manundu tu!
Hata ingekuwa mimi ningekimbia
kabisa ulingoni!
 
Back
Top Bottom