Pinda awasha mwenge MBEYA

kanganyoro

Senior Member
Jun 22, 2011
127
33
Wadau, nipo kwenye uwanja wa sokoine katika uzinduzi wa mwenge, 95% ni wanafunzi, watu wazima inaelekea wamesusa!
 
kuwa hapo ni ujinga,kuwasindikaza wana ccm ambao wakitoka hapo wanasaini kodi zetu,we unabaki na njaa
 
hiyo ndo mbeya bana!kama kuna mabadiliko yatakayotokea nchi hii,basi yataanzia Mbeya kama siyo Arusha
 
Kuna jamaa aliingia na bendera ya cdm polisi wamemnyang'anya. Nadhani wakazi wa mbeya wanaishi na ccm kimwili rohoni cdm
 
Mwenge tayari umeshawashwa, ila watu hawana hamasa kabisa, ni wanafunzi tu wasioelewa ndiyo wanashangilia.
 
Sugu hayupo, hata kama angekuwepo asingetambulishwa, waliotambulishwa ni viongozi wa ccm. Inatia huruma sana.
 
kwani wanafunzi siyo watu? Kama wewe hukwenda ni uwamuzi wako..cdm wanajipya gan4
 
Siyo siri napata kichefuchefu nikiskia watu wanapoteza muda kwenye sherehe za kuwasha mwenge. Halafu ninaanza kutapika na kuharisha nikisikia kuna watu wanashiriki mbio za mwenge.
 
katika vitu vinavyokera kutoka serikali ya CCM ni huu upuuzi wa Mwenge. Hivi hawajufunzi hawa watawala feki. Nataka kutapika kila nikifikiria hii serikali jinsi ya kuiondoa hapa TZ
 
Faida ya huo mwenge ni nini?

Ni hasara kwa nchi maana pesa nyingi sana inatumika bila tija yoyote.
Upande mwingine, kama wewe ndio kiongozi wa mbio za mwenye kitaifa, utapata ulaji (allowance) nyingi sana.
Na baada ya mbio hizo kumalizika, hutakosa ka-cheo fulani kama U-DC, n.k.
 
Ni hasara kwa nchi maana pesa nyingi sana inatumika bila tija yoyote.
Upande mwingine, kama wewe ndio kiongozi wa mbio za mwenye kitaifa, utapata ulaji (allowance) nyingi sana.
Na baada ya mbio hizo kumalizika, hutakosa ka-cheo fulani kama U-DC, n.k.

hahhaaa namkumbuka Jordan Rugimbana, na kipindi hicho nillikua Songea alikua kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa eti sasa hivi ni mkuu wa wilaya ya Kinondoni!
 

Kwani faida ya mwenge ni nini kwa dunia ya leo?
kumulika majambazi
kumulika wala rushwa
kumulika wazembe na wasiowajibika
kuchochea ngono zembe na isiyo zembe pale unapolala
...mwisho ni uchafuzi wa mazingira maana una moshi unaosababisha pollution.

Sasa huyo Sugu sijui hapendi kuwa sehemu ya haya!.

 


MUHESHIMIWA WAZIRI MKUU AKISALIMIANA NA MMOJA WA WATAKAO KIMBIZA MWENGE MUDA MFUPI KABLA YA KUWASHA MWENGE HUO

MUHESHIMIWA WAZIRI MKUU AKIWASHA MWENGE WA UHURU MUDA HUU

ENEO AMBAPO MWENGE WA UHURU UTAWASHIWA

BABY TOT WAKITUMBUIZA MUDA MCHACHE ULIOPITA

UMATI WA WATU WALIOFIKA KATIKA SHEREHE ZA KUWASHA MWENGE

HAWA NDIO MAKAMANDA WATAKAO FANYA KAZI YA KUZUNGUSHA MWENGE WA UHURU







WAZIRI MKUU MH.MIZENGO PINDA AKIWA ANAHUTUBIA MUDA HUU

WATU WAMEJAA KUNGOJA TUKIO LA KUWASHA MWENGE MUDA HUU




VIJANA WAKIWA WAMEKAA KUMSIKILIZA WAZIRI MKUU





MHESHIMIWA WAZIRI MKUU AKIWA ANAINGIA UWANJA WA SOKOINE MUDA HUU

GARI LA WAZIRI MKUU LIKIWA LIMEWASILI ENEO LA TUKIO

CHIPUKIZI WAKIENDELEA NA MAONESHO WAKATI WAZIRI MKUU ANAINGIA MUDA HUU

WAZIRI MKUU MH.PINDA AKIWA ANASHUKA KATIKA GARI LAKE NA KULAKIWA NA VIONGOZI MBALI MBALI

MUHESHIMIWA WAZIRI PINDA AKIWA ANAVISHWA SKAFU MUDA MCHACHE BAADA YA KUWASILI UWANJA WA SOKOINE

WIMBO WA TAIFA UKIWA UNAPIGWA MUDA MFUPI ULIO PITA








SOSI; Mbeya yetu!!
 
Duh, mkuu unasema Umati wa watu, wakati hapo naona wanafunzi kibao tena watoto wa shule za msingi na maaskari magereza na makda wa CCM tu.. huu mwenge hauna tija tena kwa dunia ya sasa.. zaidi ya watu kujipatia pesa na maposho yasiyo na ulazima
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom