Pinda atoka nje ya mstari na kuvunja Katiba

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Kauli ya Pinda ni kupindisha Sheria
na Asha Bani

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimeeleza kushitushwa na kauli ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, aliyoitoa mkoani Iringa kwa kuagiza uongozi huo kuiondoa mahakamani kesi iliyofunguliwa dhidi ya Diwani wa Kata ya Itunundu, kwa madai kuwa wapinzani wataitumia kama ‘mtaji’ kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Pinda alinukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari akiagiza kufutwa kwa kesi hiyo inayomkabili diwani huyo, Philip Mkumbata (CCM), aliyefikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kuhujumu miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji katika kata yake.

Katika maagizo yake, Waziri Mkuu aliutaka uongozi huo uliomburuta diwani huyo mahakamani kusikiliza mashauri hayo nje ya mahakama na si mahakamani kama walivyofanya hapo awali.

Taarifa ya CUF imeeleza kuwa chama hicho kinatambua kuwa utawala wa sheria ni kuendesha mambo kwa kuheshimu, kulinda na kufuata katiba na sheria nyingine za nchi, hivyo wananchi pia wana haki ya kuishi kwa amani katika mazingira ambayo haki zao zinalindwa. Jukumu la serikali ni kuhakikisha kuwa haki za wananchi zinalindwa.

Inaeleza kuwa Watanzania wana-demokrasia wanatambua kuwa maagizo na matendo kama haya yapo mengi nchini na hiyo ndiyo kasoro kubwa ya serikali ya CCM na kwa kipindi chote ambacho imekuwa madarakani kutokana na kuendesha nchi kwa mabavu, vitisho na ukatili.

Chama hicho kinamtaka Waziri Mkuu kuhakikisha kuwa serikali inaongozwa na katiba na sheria katika utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku na si matamanio binafsi ya viongozi wake, kama inavyofanyika hivi sasa na kwa kipindi kirefu cha CCM kuwa madarakani.
 
Kwa chama kinachowajibika kwa wananchi kwanza wangemvua uanachama. That means hata udiwani anakuwa ameupoteza. Hatua kama hiyo itawafanya wananchi wapate imani na chama cha mapinduzi na pia kuruhusu sheria kufuata mkondo wake. Sisiemu wangechukua uamuzi huu natumai hata wangeitisha uchaguzi mwingine wangeshinda maana wananchi waangewaona kuwa hawana msalie mtume na watu wanaofuja pesa za wananchi. Kwa uamuzi wa Pinda,anazidi kuwafanya wananchi waamini kuwa CCM ni chama cha kulea na kulinda mafisadi!
 
Huyu Pinda kila siku anavuruga ,sijui hajui kama kuna sheria za nchi na hii ni shida iliyoletwa na Kikwete kuokoteza watu ,nafikiri ni kuhifadhiana hivyo wanawekana karibu karibu ,wote hawa walikuwa usalama wa Taifa hivyo mmoja tu akija kuona anapuuzwa basi mambo mengi ya umafia yatajitokeza kuna vifo vinahusishwa na serikali kama Sokoine,Kolimba ,Malima,Kaduma ,Omar Ali Juma ,yule mwanamke alievalia njuga madawa ya kulevya ,Ditopile ,hawa mashahidi wa kesi ya Zombe kama haya ni kweli serikali imehusika basi kuna siri kubwa na watunzaji lazima wawe na madaraka ndani ya serikali hii hivyo mmoja akaja akaponyoka basi kuna kazi kubwa.
 
Kuna mambo mengine yakiachwa yaendelee mahakamani yanaweza kuchelewesha maendeleo.
 
Huyu Pinda kila siku anavuruga ,sijui hajui kama kuna sheria za nchi na hii ni shida iliyoletwa na Kikwete kuokoteza watu ,nafikiri ni kuhifadhiana hivyo wanawekana karibu karibu ,wote hawa walikuwa usalama wa Taifa hivyo mmoja tu akija kuona anapuuzwa basi mambo mengi ya umafia yatajitokeza kuna vifo vinahusishwa na serikali kama Sokoine,Kolimba ,Malima,Kaduma ,Omar Ali Juma ,yule mwanamke alievalia njuga madawa ya kulevya ,Ditopile ,hawa mashahidi wa kesi ya Zombe kama haya ni kweli serikali imehusika basi kuna siri kubwa na watunzaji lazima wawe na madaraka ndani ya serikali hii hivyo mmoja akaja akaponyoka basi kuna kazi kubwa.

Mkimmaind sana siatamwaga chozi bungeni mtamsamehe tu
 
Back
Top Bottom