Gosbertgoodluck
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 2,856
- 401
- Thread starter
- #81
Jatropha nimekuelewa vizuri lakini kama na wewe umenielewa ugomvi wangu ni kwa waziri mkuu kutamka hivyo hadharani, haoni kwamba hata wale ambao walisitisha ujenzi maeneo husika wataendelea kwa kuwa wameruhusiwa kufanya hivyo.
Na kitu kiinge angemwita ofisini amweleze bwana hili unalofanya litatugharimu, ili wananchi tubaki tunajua kwamba kujenga kwenye hifadhi ya barabara ni kosa, lakini walojenga kwa hizo sheria za zamani wasibomolewe.
Halafu naamini Magufuli sio mbumbumbu wa sheria kiasi hiki, nadhani anafahamu anachokifanya, incidencies za makosa zipo unapotekeleza majukumu yako. Mimi nadhani Magufuli aendelee kusimamia sheria hata kama waathirika wa usimamizi wake wataendelea kumpinga akiwemo PM Pinda.
Ugomvi wangu siyo kusitisha ubomoaji bali ni nani alistahili kutoa tamko la kusitisha. Na kama ilikuwa ni lazima kwa yeye kutoa tamko, basi alipaswa kutumia lugha ya kistaarabu kulinda heshima waziri wake Pombe Magufuli. Kuna mchangiaji anasema Pinda angeweza hata kutumia maneno kama 'nitakaa niongee na waziri magufuli ili tuone namna bora ya kutekeleza zoezi hili'. Lakini tatizo la viongozi wa nchi hii kila mtu anataka ajitutumue mbele ya wananchi kwamba ana mamlaka. Kazi kwelikweli!