Pinda Asisitiza: "Zanzibar si nchi"

Asha Abdala

JF-Expert Member
Mar 21, 2007
1,130
44
Arejea katiba ya Muungano wa Tanzania kuhusu muundo wa Taifa. Arejea pia ufinyu wa Katiba ya Zanzibar katika kipengele cha katiba ya Zanzibar kinachotaja nchi. Aeleza wapi kwenye tatizo panapostahili kurekebishwa katika katiba zote mbili

Asha
 
Arejea katiba ya Muungano wa Tanzania kuhusu muundo wa Taifa. Arejea pia ufinyu wa Katiba ya Zanzibar katika kipengele cha katiba ya Zanzibar kinachotaja nchi. Aeleza wapi kwenye tatizo panapostahili kurekebishwa katika katiba zote mbili

Asha

akiwa wapi na lini?

Mama
 
The beginning of the end of Muungano.

Hata viongozi wenyewe hawaelewani.
 
Ibara ya kwanza
Tanzania ni nchi moja na ni Jamhuri ya Muungano.

Ibara ya pili
1) Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania Bara na eneo lote la Tanzania Zanzibar, na ni pamoja na sehemu yake ya bahari ambayo Tanzania
inapakana nayo.

(2) Kwa ajili ya utekelezaji bora wa shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano au Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Rais aweza kuigawa Jamhuri ya Muungano katika
mikoa, wilaya na maeneo mengineyo, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge:Isipokuwa kwamba Rais atashauriana kwanza na Raiswa Zanzibar kabla ya kuigawa Tanzania Zanzibar katika Mikoa, Wilaya au maeneo mengineyo.Tangazo la nchi yenye Mfumo wa vyama vingi
Sheria ya 1992


Ibara ya 4
(1) Shughuli zote za Mamlaka ya Nchi katika Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na kudhibitiwa na vyombo viwili vyenye mamlaka ya utendaji, vyombo viwili vyenye mamlakaya kutekeleza utoaji haki, na pia vyombo viwili vyenyemamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji washughuli za umma.
(2) Vyombo vyenye mamlaka ya utendaji vitakuwa ni Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, vyombo vyenye mamlaka ya kutekeleza utoaji haki vitakuwa ni Idara ya Mahakama ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano na Idara ya Mahakama ya Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, na vyombo vyenye mamlaka ya kutunga sheria na kusimamia utekelezaji wa shughuli za umma vitakuwa ni Bunge na Baraza la Wawakilishi.



 
Kuna kazi kubwa hapa kwani wazenji wamekuja juu sana juu ya ukweli huu ,wao wakisema kuwa wamedhalilishwa .........

Huenda kesho likatolewa kauli bungeni kwani linaonekana kuwagawa wabunge wa zenji na wa huku bara ..........

Vikao vingi sana vimefanyika leo, na mada ilikuwa ni juu ya hilo jambo.....
 
Maneno hayo ameyasema leo bungeni alipokuwa akijibu swali la papo kwa papo lililoulizwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohammed, katika Mkutano wa 12 wa Bunge unaoendelea dodoma.


Akijibu swali hilo Mhe. Pinda alisema hajateleza kama ilivyoelezwa na Pandu na kusema kuwa kauli yake kwamba Zanzibar si nchi, bali ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inatokana na Ibara ya 1 Kifungu cha (1) na (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Pinda alisema Kifungu cha (1) cha Ibara hiyo, kinaeleza bayana kuwaTanzania ni nchi moja na pia ni Jamhuri ya Muungano. Alisema Kifungu cha (2) kinafafanua kwamba eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni Tanzania Bara na Zanzibar, ambayo eneo lake lote linajumuisha visiwa vya Unguja na Pemba.
 
Akiwa Dodoma leo.

Nae Profesa Issa Shivji aweka bayana kuwa Zanzibar sio nchi, ila ni taifa!

Lakini asema katiba ya Zanzibar ina mapungufu kwa kusema Zanzibar ni nchi.

Asha

Leta habari kamili basiiiii,
 
Nadhani umefika wakati suala hili inabidi litafutiwe ufumbuzi wa kudumu. Ingawa wazanzibari hawataki kusema wazi, lakini wanaonekana hawafurahii aina ya muungano ambao unawaondolea 'nchi' yao. Hili halikuwa lengo la kuunganisha Tanganyika na Zanzibar. Lengo lilikuwa ni kuanza na serikali mbili, kwa lengo la kuelekea kwenye serikali moja, lakini hawa jamaa wanaonekana badala ya kueleklea kwenye serikali moja, wanataka kurudi kwenye nchi mbili. Kwa hali hii, hakuna cha muunganio wala nini, tunadanganyana tu
 
Wahafidhina hawawezi kushindana na wa CCM Tanganyika ,kiboko ya tatizo hili ni hujibiwa na CUF tu na hapo CCM bara huwa kama wametiwa maji baridi na kuwekwa ndani ya Gunia ,maana CUF ndio kiboko ya CCM mafisadi na wahafidhina wao.
Nyie subirini tu mwenye ndevu apate jukwaa muone atakavyorusha mate atawachanganya wote Pinda na Pandu.Na mambo kukaa sawa.Ila kwa kutegemea Wahafidhina wa ASP na Mafisadi wa CCM msitegemee ukweli mwisho mmoja wao akiona anakaribia kushindwa atadai arudishiwe Chama Chake.
CCM imeshapoteza dira na sasa wanakamata kila wanapoona patawasaidia ,halafu huyu Sitta fisadi mkubwa ,hivi haoni kama kutayarisha kikao chengine ili kujadili mambo ya kamati ya EPA iptl sijui ,ni kuhujumu fedha ya walala hoi ,maana hata wabunge walisikika wakishangalia baada ya kusikia kuijadili ripoti kutapangwa wakati wake maalum ,mimi sikuona kuwa furaha walioonyesha wabunge ni umuhimu wa kupata nafasi nyeti kuijadili ripoti bali ni kushangilia posho tu ,kwani hakuna kilichojadiliwa na kuonekana kumeleta faida ,kila unapotazama utaona mawaziri kibao wizara zao zimevuruga na kupanga bajeti mbovu na matumizi ya fedha ambayo hayajulikani zimetumika vipi maana hakuna kilichofanywa hata kimoja,tunasikia wizara imetengewa trilioni kadhaa,chukulia mwaka uliopita sasa kama feza hiyo ilitengwa kwa ajili ya barabara au hospitali au shule ,kwa kweli barabara zilizotengewa fedha hazikuonekana kujengwa zikamaliza ,fedha iliyotengwa siku zile imekwenda wapi ?
Wabunge mnashangilia posho tu msituzingue ,hamna kimoja mnachokijadili kikapatiwa uamuzi zaidi ya fisadi kujiuzulu.
Mbona hapo Bungeni hatujawasikia kusema na kupinga bajeti mpaka muhakikishiwe kuwa mafisadi wamepandishwa kizimbani ,tutaamini vipi kama mnaenda kuijadili ripoti wakati mliowajadili mwanzo wanapeta na feza yetu mitaani ??
 
Nakwambia ya Zenji we acha tu. Bila ya serikali tatu nakwambia wataendelea kushikana makoti wao wenyewe.
Tulishasema dawa ya muungano wetu ulio dhaifu ni serikali tatu. Yaani Tanganyika, Zanzibar na ile ya Muungano. Sasa wao chama cha mafisadi kikajua wameshikwa pabaya na ujanja ujnja wao umefika mwishoni wakaipinga hoja hii ya mh yule jaji Kisanga. Na hasa huyu fisadi namba moja WBM. Sasa wanageukana wao kwa wao. Hakuna anayejua what is what and which is which!
Endeleeni toaneni macho. Maana ndani ya chama chenu hakuna domo krasia. Mnapendaga kulalamikia pembeni maana ukilalamikia katika chama wewe huna mshikamano wa chama na hufai. Kuleni matunda ya ufisadi wenu hadi katika chama chenu.
Endeleaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Nilisema toka mwanzo ni matumizi mabaya ya neno NCHI na TAIFA ktk lugha yetu ya Kiswahili. Sasa ikiwa hata KATIBA imetumia neno NCHI pale TAIFA ilipotakiwa huwezi kumlaumu Pinda hata kidogo kwa sababu kama kiongozi anaendeshwa na KATIBA ya nchi (taifa) inavyosema..Akiwa Bungeni hazungumzi kutoka kichwani mwake!
 
Nadhani umefika wakati suala hili inabidi litafutiwe ufumbuzi wa kudumu. Ingawa wazanzibari hawataki kusema wazi, lakini wanaonekana hawafurahii aina ya muungano ambao unawaondolea 'nchi' yao. Hili halikuwa lengo la kuunganisha Tanganyika na Zanzibar. Lengo lilikuwa ni kuanza na serikali mbili, kwa lengo la kuelekea kwenye serikali moja, lakini hawa jamaa wanaonekana badala ya kueleklea kwenye serikali moja, wanataka kurudi kwenye nchi mbili. Kwa hali hii, hakuna cha muunganio wala nini, tunadanganyana tu

Sasa naelewa ndiyo maana Mwalimu Myerere alikuwa mkali mlivyokuwa mnaanza kuuzungumzia Muungano kwa tafsiri zenu potofu. Kumbe alikuwa anakueleweni kweli kweli. Nakushangaeni Watanzania wa hivi sasa na tafsiri zenu hizi za kisomi. Mnaotaka moja na manotaka tatu. Muelewe huo wenu sio Muunagnao wa 1964 kama ulivyoelezwa na waasisi. Mheshimiwa Pinda yuko katika mstari na anavyoeleza ni sahihi. Nafikiri wabunge na Wawakilishi washughulikie mengine ya maana na kuacha hilo la Tafsiri. Kama uelewa wao ni mdogo basi warudie kudurusu Katiba na maandiko na kauli za baba wa Taifa.
 
Back
Top Bottom