Pinda asema watu wa Hali ya hewa wanachanganya

Lukwangule

Senior Member
May 25, 2009
157
2


KATIKA hali inayoonyesha kuna mushkeri wa kweli hali ay Hewa TMA, Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema Mamlaka hiyo imekuwa ikijichanganya kuhusu taarifa zake na kuleta shida kuwa kwa wananchi.

Akizungumza mjini Dodoma wakati akiwa na kikao cha kazi na wakuu wa mikoa yote nchini na makatibu tawala wa mikoa, Pinda alisema mara nyingi mamlaka hiyo imekuwa ikitoa taarifa ambazo zimekuwa tofauti na hali halisi.

Kauli ya Waziri Mkuu ilifuatia maelezo yaliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya John Mwakipesile ambaye alieleza kuwa taarifa za TMA zimekuwa zikiwachanganya wananchi ikilinganishwa na taarifa za Malawi wakati zile za wenzao wa Malawi ziko sahihi zaidi.:rolleyes:
 
Back
Top Bottom