Pinda arushiwa kombora la Zimbabwe

Kubwajinga

JF-Expert Member
Jan 23, 2008
2,194
296
Kama ilivyosemwa kuwa 'Nyani haoni ..............'


Pinda arushiwa kombora la Zimbabwe

2008-07-03 19:13:27
Na Waandishi Wetu, Jijini


Waziri Mkuu Bwana Mizengo Pinda leo amejikuta akirushiwa kombora la Zimbabwe wakati anajibu maswali ya papo kwa papo ya wabunge.

Kiongozi upinzani Bungeni, Mheshimiwa Hamad Rashid ndiye aliyerusha kombora hilo akitaka Serikali kueleza kwanini Mwenyekiti wa Umoja wa Nchi za Afrika (AU), Rais Jakaya Kikwete asiishauri serikali ya Zimbabwe kupiga kura za maoni juu ya tatizo lake la kisiasa kama ilivyokuwa kwa suala la Zanzibar.

Hivi karibuni CCM iliamua kuwa suala la kuundwa kwa Serikali ya mseto ya Visiwani Zanzibar lirudishwe kwa wananchi ambapo watapiga kura na kuamua.

Akijibu swali hilo Bungeni , Mheshimiwa Pinda amesema hayo ni maamuzi ya Ssrikali ya Zimbabwe yenyewe na si Tanzania.

Akasema maamuzi ya kulirudisha suala hilo kwa wananchi yanatokana na mazingira yaliyopo visiwani humo na si kama ilivyo kwa Zimbabwe na hivyo suala la Zimbabwe ni lao.

Jana AU waliazimia kuundwa kwa serikali ya mseto nchini Zimbambwe ambapo nafasi ya uraisi itashikwa na Rais Robert Mugabe na nafasi ya Uwaziri Mkuu, kwenda kwa Morgan Tsvangirai.

Kadhalika Waziri Mkuu amezungumzia suala la mipango miji nchini ambapo amesema kero kubwa inatokana na kutokuwa na wahandisi wenye uwezo na wakweli katika kusimamia kazi.

``Tuna tatizo la usimamizi wa majengo ni uwezo wa wahandisi vinginevyo yanaweza kutokea kama yaliyotokea hivi karibuni,`` akasema Waziri Mkuu.
Swali jingine lilitoka kwa mbunge Chwaka (CCM), Mheshimiwa Yahaya Kassim Issa aliyetaka kujua kwanini Ijumaa ya tarehe 27 ofisi ya Waziri Mkuu ilieleza kuwa Zanzibar si nchi wakati ina katiba yake, wimbo wake , bendera yake, muhimili na mamlaka kamili.

``Katiba ya nchi inaeleza kuwa Tanzania Bara na Visiwani ni nchi moja, yenye Serikali moja ya muungano,`` akasema na kufafanua kuwa zipo serikali mbili ya Muungano na ile ya Visiwani ambapo mambo mbalimbali yamekuwa yakiamuliwa kufuatana na katiba.

Akasema mpaka hapo katiba itakapobadilishwa ndipo mambo mengine yanaweza kufuata.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom