Pinda apingwa kuhusu Mkapa

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
5,565
836
Sunday, 28 June 2009 10:32
*Wataka afikishwe mbele ya sheria
*Mwingine awashukia wanaomtetea
*Aambiwa alikiuka sheria ya maadili

Na Reuben Kagaruki

SIKU moja baada ya Serikali kumsafisha Rais Mstaafu Mzee Benjamin Mkapa, kutokana na tuhuma za ufisadi ambazo zinaelekezwa kwake, Katibu Mkuu wa Chadema Dkt. Wilbroad Slaa, amesema kamwe hawatanyamaza kimya kwa kuwa rais huyo mstaafu hayupo juu ya sheria.

"Sheria inafanyakazi kama msumeno, haina ubaguzi ukiona tunaanza kuwa na sheria za aina hiyo ujue nchi inaenda pabaya,"alisema Dkt. Slaa.

Dkt. Slaa ambaye pia ni Mbunge wa Karatu kwa tiketi ya CHADEMA alitoa kauli hiyo alipozungumza na gazeti hili jana akiwa mjini Bukoba kwa njia ya simu. Alisema hata wabunge wanaopiga kelele kumtetea Mzee Mkapa nao wanastahili kuchunguzwa.

"Mimi nawaheshimu sana viongozi wetu na ninamheshimu Waziri Mkuu Pinda (Mizengo) ni mwanasheria anajua kuwa hata mtu akipitiwa sheria inakata kama msumeno...hauwezi kumuacha aliyetenda kosa kwa sababu ya kupitiwa," alisema.

Alisisitiza kuwa kama ni hivyo basi magereza yote yafunguliwe ili watu wote wawe huru. Dkt. Slaa alisema hadi leo Mzee Mkapa hajawahi kujitokeza hadharani na kujibu tuhuma zinazoelekezwa kwake ili asamehewe.

Dkt. Slaa alisema inashangaza kuona watu wanajitokeza kwa ajili ya kumsafisha wakati wakijua kuwa taratibu za tenda zilikosewa. Kuhusu mgodi wa Kiwira kushindwa kuwalipa wafanyakazi wake mishahara kwa miezi 10, alisema Serikali ilipaswa kuusadia kama ambavyo imekuwa ikifanya kwa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) Alisisitiza kuwa wataendelea kupiga kelele.

Kwa upande wake Mwanasheria wa CHADEMA, Bw. Tindu Lisu, alisema "Jaribio la Pinda ni kutaka kubadilisha ufisadi kwa lengo la kumtetea," alisema na kuongeza; "Kama mzee Mkapa sio fisadi kwa nini wanataka kumnyang'anya mgodi wa Kiwira?" Alisema Mzee Mkapa akiwa Rais alivunja sheria ya maadili ya viongozi wa umma kwa kujimilikisha mgodi huo wakati akijua fika kuwa kufanya hivyo ni makosa.

"Serikali inajua kuwa alivunja kiapo chake ndiyo maana inataka kurejesha mgodi huo mikononi mwake," alisema na kusisitiza kuwa Waziri Pinda alitakiwa kuwaeleza wananchi ni kwa mazingira gani Mzee Mkapa alijimilikisha mgodi huo. Alisema fisadi anaweza akawa mtu anayetumia madaraka aliyopewa na umma kujimilikisha mali, hivyo sio lazima awe tajiri.

Juzi Waziri Pinda alimtetea mzee Mkapa akisema ni mwadilifu, mcha Mungu na mtu anayependa Kanisa. "Hadi leo Mzee Mkapa anapendwa na kutambulika kimataifa kama kiongozi mwadilifu," alisema Bw. Pinda na kuongeza; "Kama kweli ni fisadi, basi tuoneshwe ufisadi wake kauwekeza wapi."

Kauli ya Waziri Pinda inalenga kujibu madai ambayo yamekuwa yakitolewa na wanasiasa dhidi ya Mzee Mkapa, ambapo anadaiwa kujimilikisha mgodi wa makaa ya mawe wa Kiwira.

Wanasiasa hao wanadai kuwa kila kukicha mgodi huo umekuwa ukimwingizia mamilioni ya fedha. Madai mengine ni kuwa Mzee Mkapa alifanyabiashara akiwa Ikulu.
Source: Pinda apingwa kuhusu Mkapa
 
Pinda apingwa kuhusu Mkapa

*Wataka afikishwe mbele ya sheria
*Mwingine awashukia wanaomtetea
*Aambiwa alikiuka sheria ya maadili

Na Reuben Kagaruki
Majira
Jumapili, 28 Juni 2009

Pinda amepindisha hata ile kasi yake alioanza nayo...sasa amekuwa wakili wa mafisadi...kweli madaraka matamu anasahau kabisa kuwa yeye anawajibika kwa walala hoi sio mafisadi...jama amebadilika kabisa..ameshakuwa pure pilitik ...............hamna kitu hata uadilifu wake utakuwa na mashaka soon maana nae ataona mm yaani nami nitoke hapa sina kitu....atakwiba soon mtaona nyie tulieni tu.
 
Kasi gani alianza nayo ? Toka lini amewajibika kwa Walala hoi ? Uadilifu wake huo unauongelea ni upi na toka lini ? Sifa pekee aliyokuwa nayo wakati wa kuteuliwa ni kuwa hakuwa na kashfa iliyojulikana. Viongozi wengi wa kisiasa huteuliwa kwa njia hii - uchafu wao kutojulikana. Utakuwaje serikalini miaka nenda rudi ukose sifa hata moja ya mema uliyotendea jamii - yaani upo upo tu. Mtu kama Tindu Lissu akiteuliwa hivi leo kuwa AG wa Tz kwa mfano, sidhani itakuwa shida kutaja rekodi yake katika kusimamia utawala wa sheria. Lakini kuna watu wanateuliwa halafu wanaanza kutafutiwa visifa vya kufikirika ama kubuni - ndivyo alivyopatikana Waziri Mkuu wetu, [FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]Rt. Hon. Mizengo Kayanza Peter Pinda.

[/FONT]
 
Pinda naye ni product ya ufisadi tu!!! Hana jipya hata kidogo!!!

Tiba
 
Back
Top Bottom