Pinda apindishwa kuongea na wananchi wa Nyamongo wanaoishi karibu na mgodi

Mosachaoghoko

Senior Member
Apr 19, 2011
137
10
wana jf leo ilikuwa ni ziara ya kiongozi wa shughuli za serikali bungeni na PM wa JMT kufanya ziara kule mgodini north mara nyamongo lakini hakutaka hata kuuliza kuwa mbona haoni mgodi ambao unazungukwa nA WANANCHI ni baada ya kupelekwa kwingine na viongozi wakiongozwa na mkuu wa malaya dc na hii ni baada ya jhana majira ya saa 17;00 barrick kufanya mauaji ya mwanafunzi wa sekondari aliyekuwa akitokea kwenye sherehe ya mahafali yake kumaliza f4 hivyo kugongwa na dumper truck la mgodi na kuuawa hapohapo eneo la boom gate kama linayojulikana na kufanya idadi ya watu waliouawa katika eneo hilo la boom gate kuwa isiyo pungua wananchi watano lakini hakuna hatua zozote zinazochukuliwa na mgodi,serikali kuu na serikali za mitaa
 
Tumekupata baba. Bora tu hawakumpeleka maana ngeishia kwenda kulia na hakuna ambacho angeweza kufanya. Old teethless dog...
 
Hivi Nyamongo ni Tanzania hii au sehemu ya Kenya ? Mbona matukio mengi lakini hakuna hatua zozote ? Pinda kweli anaweza kusema kadanganywa ? Siamini maneno haya maana ana akili na macho kwa nini asiulize ?Hao waliokuwa kwenye mkutano mbona hawakusema lolote kwamba hapo si mahala husika?
 
kuna watu wamenunua hii nchi si bure, hata watanzania wenzetu hawayaoni haya kina pinda, Jk, na wabunge wengine vilaza wa ccm, aaaha tunakoelekea siko....!
 
Hv tokea tupate uhuru hadi siku ya kiama inawezeka kuja kutokea kupata Waziri mkuu wa ajabu kama Pinda kweli?
 
Hivi Nyamongo ni Tanzania hii au sehemu ya Kenya ? Mbona matukio mengi lakini hakuna hatua zozote ? Pinda kweli anaweza kusema kadanganywa ? Siamini maneno haya maana ana akili na macho kwa nini asiulize ?Hao waliokuwa kwenye mkutano mbona hawakusema lolote kwamba hapo si mahala husika?

Kama kweli Pinda hakuona umuhimu wa kuongea na wananchi wanaoishi kuzunguka mgodi wa nyamongo basi atakuwa amejishushia sana heshima na hadhi yake.

Na hii ni kuthibitisha kwa mara nyingine tena kwamba viongozi wa nchi hii wote wako mifukoni mwa wafanyabiashara.

Pinda anagfahamu unyama unaotendwa na wawekezaji wa barrick north mara, yeye kutotaka kuongea na wananchi wa nyamongo amenisikitisha sana na amezidi kuwakatisha tamaa wananchi.
 
Back
Top Bottom