Pinda apatwa hofu takwimu za SENSA;Huenda MIPANGO ya Serikali ikafeli kwa kuwa sio sahihi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda apatwa hofu takwimu za SENSA;Huenda MIPANGO ya Serikali ikafeli kwa kuwa sio sahihi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 16, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]

  na Sitta Tumma, Kwimba


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]SIKU chache baada ya kwisha kwa sensa ya watu na makazi, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ametilia shaka takwimu zilizopatikana na kusema huenda mipango ya serikali ikafeli kwa kukosekana kwa takwimu sahihi za idadi ya Watanzania.


  Amesema serikali inategemea sana kupata takwimu sahihi za wananchi wake kwa ajili ya maendeleo, lakini sensa ya mwaka huu inatia shaka kubwa.


  Pinda alitoa kauli hiyo juzi alipokuwa akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mpira wa Ngudu mjini hapa.

  Ingawa alilizungumzia kwa kifupi suala hilo, alitolea mfano kwa kusema kuwa usambazwaji mzuri wa huduma ya maji wilayani Kwimba, utategemea na takwimu sahihi za sensa kwa wananchi.


  “Ili serikali itekeleze vema mikakati yake ya kimaendeleo, lazima takwimu sahihi za sensa ziwepo. Hofu yangu ni pale takwimu hizi zisipokuwa nzuri, maana yake serikali itakuwa na mtihani mgumu kupeleka kwa haraka maendeleo kwa wananchi,” alisema.


  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alisema inamkasirisha sana kusikia albino ameuawa ama amejeruhiwa kwa imani za kishirikina na aliagiza vyombo vyote vya ulinzi mkoani hapa kuhakikisha vinawakamata na kuwafikisha kwenye vyombo vya dola watuhumiwa wote wa mauaji hayo.


  Kuhusu kero ya maji, alitoa muda wa miezi mitatu kuanzia sasa kwa uongozi wa Wilaya ya Kwimba na mkoa wa Mwanza kwa ujumla kuondoa adha hizo haraka iwezekanavyo, vinginevyo atamwajibisha Mkurugenzi Mtendaji na Mkuu wa wilaya hiyo, Seleman Mzee.


  “Tatizo la uhaba wa maji hapa Kwimbva litatuliwe kabla ya mwisho wa mwaka huu. Kama itashindikana Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya tutashikana mashati,” alisema Pinda.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Who is to blame? SIO WAISLAMU ni Serikali ya CCM kutoondoa Dosari za SENSA kwa Wananchi ambao ni WAISLAMU

  CCM na Serikali yake VIONGOZI walilala... kutegemea VITISHO na last min fight will help them... POOR CCM
   
 3. MPIGA ZEZE

  MPIGA ZEZE JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2012
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 515
  Trophy Points: 280
  Kwani hata takwimu zilipokuwa sahihi, mfano za sensa ya 2002 na kabla ya hapo, mbona hatukuona mipango ya serikali ikibadilika? Tuangalie vitu kuntu: mfano idadi ya mashangingi ya seikali iliongezeka pengine mara thenashara lakini idadi ya wototo wa shule za msingi waliokalia sakafu (tena za udongo) na kulundikana kama magunia ya maharage katika vyumba vya madarasa iliongezeka mara mia. Siamini kama takwimu za sensa zinatumika kupanga maendeleo. Sensa ya watu na makaazi nchini Bongoland ni political slogan nyingine ya kuwakumbusha wananchi kuwa kuna dola (kama inavyoambatishwa na visheria visivyo na miguu wala kichwa, vitisho, na hata mauaji yanayofanywa na vyombo hivyo hivyo vya dola). Niliwaunga mkono Waislamu kuigomea na ninaendelea kuwaunga mkono. NI USANII!!!!
   
 4. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2012
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Si afadhali mtishe halafu zoezi lifaulu, sasa wao wametisha watu na zoezi la sensa limedoda!!! katika wadhaifu ndani ya awamu ya nne, huyu anamfuata JK!!! Hana amri, hana mamlaka, ameshajiamulia kulialia tu!!

  pheeew!!!
   
 5. Thanda

  Thanda JF-Expert Member

  #5
  Sep 16, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,915
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kati ya mwaka ambao zoezi la sensa limekwama ni mwaka huu...hata tuishio nje ya mipaka ya Jamhuri yetu, na bado tuna uraia wa nchi moja (TZA) tumetoswa na hatukuhesabiwa, tuliambiwa balozi alikuwa "busy" kumbana akasema wengi wetu majina yetu hayapo huenda tulizamia, tulipombana zaid akasema hakuwa na staff wa kutosha ambao walipaswa kufika kwenye makazi yetu kwani wengine tumeshazaliana, kumbana zaidi akasema waliozaliwa huku hawapaswi kuwa raia halali wa TZ labda wakaombe uraia wakiwa wakubwa na kufika TZ, kumbana tena akaingia mitini eti ana safari ya ghafla, anauguliwa na mke wake ( Stupid response, nani wa kudanganywa hivi?)...Ubalozi utakutambuaje halafu ghafla uambiwe hauko registered? ati ulizamia?...Naombeni personal mobile contact ya Membe, Ben Kamillius. Nitam-skype na kumrusha humu JF...Niko serious wadau!!
   
 6. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Watavuna walichopanda...
   
 7. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #7
  Sep 16, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,747
  Likes Received: 12,841
  Trophy Points: 280
  Hofu yanini si walisema sensa imefanikiwa kwa kiasi kikubwa?
   
 8. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #8
  Sep 16, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,078
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Wamepanda nini!?
   
 9. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #9
  Sep 16, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Hawa jamaa ni kuwafungulia mashtaka haraka sana; ya uhujumu uchumi, ubadhirifu wa mali ya umma na uzembe.

  Kama Waziri Mkuu Pinda alivyonukuliwa hapo:-

  1) Kwa vile kulikuwa na kila dalili za serikali kutokuwa na mahusiano mazuri ya kijamii na wananchi kwa nini waliendelea na "zoezi la sensa"?

  2) Maandalizi ya zoezi lenyewe yalijaa kasoro kubwa kubwa za kimsingi. Mfano watekelezeji wakuu yaani walimu, viongozi wa mitaa nk walikuwa na misuguano na serikali juu ya posho/malipo. Kwa upande wa walimu ndio kwanza mgomo wao usiokuwa na kikomo ulikomeshwa kwa nguvu na zuio la mahakama.

  3) Kwa sababu kama alivyokiri (pengine kwa unafiki) kuwa sensa ni muhimu kwa takwimu za kimaendelo za nchi yoyote ni kwa nini serikali hii imeliharibu zoezi hili na kupelekea ukosefu wa takwamu sahihi?

  4) Ni nani atakayelipa hasara ya zoezi hilo lililoshindwa? (Naomba ifahamike hapa kuwa pamoja na juhudi binafsi za kuwasiliana na mjumbe wa mtaa ninakoishi bado sikuhesabiwa!)

  Mwisho, hapo kwenye nyekundu, TAKWIMU NZURI ni zipi? Je ni za kupika? Alidhani hii ni Tume ya Uchaguzi au alimaanisha nini hapo?
   
 10. Kankwale

  Kankwale Senior Member

  #10
  Sep 16, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 128
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hofu ya nini ikiwa matatizo mengi yalielezwa kabla ya zoezi kuanza lakini wanayaita changamoto kila kukicha.
   
 11. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #11
  Sep 16, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  CCM na serikali wana kpaji cha KUUDHI na KUKASIRISHA mno. Kila walifanyalo au walisemalo kama sio karaha basi utaishia kukasirishwa kwa namna moja au nyingine.

  Hii incompetency na unaccountability wanayoonesha haipaswi kusubiri hadi 2015.
   
 12. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #12
  Sep 16, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,818
  Likes Received: 83,217
  Trophy Points: 280
  Usanii mtupu!!!! Kwani takwimu za miaka ya nyuma ambazo zilikuwa sahihi walifanya mipango ipi ya Serikali ambayo iliboresha maisha ya Watanzania kwa namna moja au nyingine!? Wasisingizie ukosefu wa takwimu sahihi kama ndio kikwazo cha kushindwa kupanga mipango ya kimaendeleo.

  Watu wengi tuliandika hapa kuhusu matatizo mbali mbali katika maandalizi ya sensa ile na kushauri labda isogezwe mbele ili kushughulikia mapungufu mbali mbali ikiwemo kuhakikisha Watanzania wote wanashiriki bila kukosa lakini hii Serikali SIKIVU ikatia pamba masikioni sasa imekula kwao.

  Sasa wimbo maarufu kwa miaka ijayo utakuwa, "Tunashindwa kupanga mikakati ya kimaendeleo kwa sababu takwimu za sensa tulizonazo si sahihi."

  Wanaostahili kulaumiwa kwa hili si wengine bali ni DHAIFU na Pinda.
   
 13. Mkali Tozz

  Mkali Tozz JF-Expert Member

  #13
  Sep 16, 2012
  Joined: Aug 9, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  DUH! Serikali ya CCM imeshapata KISINGIZIO cha kutuyeyusha.Ili watufisadi zaidi.
   
 14. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #14
  Sep 16, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  huyu mzee ni mzigo sana kwa taifa hili..
   
 15. hekimatele

  hekimatele JF-Expert Member

  #15
  Sep 16, 2012
  Joined: May 31, 2011
  Messages: 9,489
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Hawa jamaa ni kweli hawakujipanga. Imewachukua miaka 10 kujiandaa na sensa na ghafla wanatuambia wana wasiwasi na takwimu. no wonder hata wananchi wenyewe washakua na wasiwasi na serikali kitambo sana. Its just a matter of time watanzania waamue upya.
  Mda wote huu walikua wanafanya nini mpaka leo waje kusema wana wasiwasi na takwimu za sensa?
   
 16. Nyikanavome

  Nyikanavome JF-Expert Member

  #16
  Sep 16, 2012
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Sio wasiwasi tu, hapo ametumia lugha ya kiutu uzima tu; matokeo ya sensa ya mwaka huu hayatakuwa sahihi. Mimi najua watu kibao ambao hawajahesabiwa hapa mtaani kwetu. Makarani walipoonekana siku ya kwanza hawakurudi tena mpaka kile kiini macho cha kuongeza muda bila kuwaongezea hela watendaji kilipotokea.
   
 17. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #17
  Sep 16, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,782
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  jamaa mchovu kabisa,kabakia kuratibu mauaji ya wananchi wasiokua na hatia.
   
 18. Bavaria

  Bavaria JF-Expert Member

  #18
  Sep 16, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 44,105
  Likes Received: 11,254
  Trophy Points: 280
  kila ki2 kinafanywa kisiasa.
   
 19. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #19
  Sep 16, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Masikini Pinda, je alijisikiaje Mwandishi Daud Mwangosi alipolipuliwa na polisi? Alikasirika, alisikitika au vipi?
   
Loading...