Pinda aonja utamu wa mgawo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda aonja utamu wa mgawo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Injinia, Mar 19, 2010.

 1. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nimesoma hii habari huku nikitabasamu:
  1. Mkutano umefanyika Hoteli ya Whitesands kwa sababu gani? Hakuna ukumbi wa mikutano kwenye ofisi ya Waziri Mkuu?
  2. Mkutano unazungumzia kilimo kwanza wakati hata huo umeme wa kusukuma usindikaji na uhifadhi wa mazao ya kilimo ndio huu!!


  Gazeti la Mwananchi
  Sadick Mtulya
  WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda jana alionja makali ya mgao wa umeme na kulazimika kukaa gizani baada ya umeme kukatika katika mkutano wa kujadili mpango wa Kilimo Kwanza na wadau mbalimbali wakiwemo wasomi na Mabalozi.

  Adha hiyo ilimkumba Pinda jijini Dar es Salaam majira ya saa 4:00 asubuhi mara baada ya kumaliza kutoa taarifa ya mapendekezo ya serikali kwa watafiti kuhusu namna ya kuendeleza mpango huo wa kuboresha uzalishaji katika sekta ya kilimo.

  Pamoja na mkutano huo kufanyika asubuhi, nuru ilipotea kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Whitesands baada ya umeme kukatika na hivyo kubakia mwanga hafifu kutoka nje uliolazimisha baadhi ya maofisa kukimbilia madirishani kufungua mapazia kuruhusu mwanga zaidi, huku joto likichukua nafasi.  Katika mkutano huo umeme ulikatika mara mbili na kwa nyakati tofauti. Ulianza kukatika saa 4:36 asubuhi na hivyo jenereta kuwashwa, lakini ilipofika saa 5: 18 umeme ulikatika tena baada ya jenereta hilo kuzimika kabla ya kuwashwa tena saa 5: 24 asubuhi.


  Hata hivyo kutokana na umuhimu wa mkutano huo, Pinda alilazimika kukaa na kusikiliza, risala iliyosomwa na Profesa Hans Binswanger kutoka Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Tshwane, Pretoria nchini Afrika Kusini kwa takribani dakika 30.
  Hata hivyo, haikuweza kubainika sababu ya jenereta hilo kuzimika na hadi majira ya saa 8:00 mchana umeme wa Tanesco ulikuwa bado haujarudi kwenye ukumbi huo.  Naye balozi wa Uholanzi nchini, Dk Ad Koekkoek alisema mpango huo utafanikiwa endapo serikali itatenga bajeti kubwa ya fedha, kutunga sera pamoja na kutoa elimu ya kutosha kwa wakulima.
   
 2. W

  Wakwetu Senior Member

  #2
  Mar 19, 2010
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 157
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  aibu hiyo kwa taifa
   
 3. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #3
  Mar 20, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Jamani injinia mkutano ule haukuwa wa ofisi ya Waziri Mkuu na ndio maana haukufanyika ofisini kwake. Ile ilikuwa ni 15th Repoa Annual Workshop amabpo mwaka huu iliongozwa na theme 'Kilimo Kwanza' na kwa kuwa Waziri Mkuu ndiye 'Champion' wa Kilimo kwanza alialikwa kama mgeni rasmi atakayeifungua Workshop hiyo.
   
Loading...