Pinda aombe radhi Bunge

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,820
287,890
Masikini Pinda...hajui hata nini kinachoendelea ndani ya siri kali

`Pinda aombe radhi Bunge`

2008-07-02 16:57:55
Na Emmanuel Lengwa, Jijini

Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Kayanza Pinda ametakiwa kuliomba radhi Bunge la Jamhuri ya Muungano na Watanzania kwa ujumla, kutokana na kauli yake Bungeni juu ya msimamo wa Serikali kuhusu kampuni tata ya Meremeta.

Shinikizo hilo kwa Waziri Mkuu limetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa vyombo vya dola nchini tayari vimeshalichunguza suala hilo na kubaini kuwepo kwa wizi wa fedha za Watanzania, na kuwa hivi sasa vinajiandaa kuwaburuza wahusika mahakamani.

Alhamisi ya wiki iliyopita Waziri Pinda alikataa kata kulizungumzia suala hilo Bungeni, kwa madai kuwa linagusa masuala ya Usalama wa Taifa na kuwa mpaka lipate kibali cha Rais ili liweze kujadiliwa Bungeni.

Prof. Lipumba amesema leo kuwa Waziri Mkuu anapaswa kuelewa kila kinachofanywa na Serikali na kuwa alistahili kuwaeleza wabunge ukweli kuwa suala hilo linafanyiwa kazi na vyombo vya dola, hivyo analazimika kuomba radhi kutokana na makosa hayo aliyofanya .

``Waziri Mkuu anapaswa kuliomba radhi Bunge kwa kutolipatia taarifa sahihi, maana lilikuwa jambo la kuwaeleza wabunge tu kuwa suala hilo linafanyiwa kazi na vyombo vya dola, lakini hakufanya hivyo,`` akasema Prof. Lipumba.

Prof. Lipumba amedai kuwa hivi sasa inaonyesha kuwa kuna matatizo ya mawasiliano ndani ya Serikali, kiasi kwamba kila mmoja anazungumza lake na kujikuta wakitofautiana katika suala moja.

Akitoa mfano wa kujikanganya, Prof. Lipumba amesema, Waziri wa Fedha, Bw. Mstafa Mkullo hivi karibuni alilieleza Bunge kuwa fedha zilizochotwa katika akaunti ya Madeni ya Nje, EPA, sio za Serikali, lakini Waziri Mkuu akasema lazima fedha hizo zirejeshwe serikalini.

``Wamekuwa wakijikanganya katika taarifa zao wenyewe, mfano mzuri ni huo wa fedha za EPA mbapo kauli ya Waziri Mkullo ilitofautiana na ile ya Waziri Mkuu ndani ya Bunge,`` akasema Prof. Lipumba.

Wiki iliyopita wabunge walihoji uhalali wa kampuni ya Meremeta na kumtaka Waziri Mkuu atoe ufafanuzi, ambapo Mbunge wa Kigoma Kaskazini alifikia hatua ya kusema kuwa mradi huo ulikuwa ni wizi wa fedha za Watanzania.

SOURCE: Alasiri

 
Meremeta deal:pCCB investigating

-Police, national intelligence have also been on the trail

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

A FORMAL investigation into possible corruption in relation to the controversial Meremeta and TANGOLD companies has already reached an advanced stage, with local detectives having flown as far as the UK and South Africa in search of key evidence as part of the probe, it has been revealed.

According to informed sources, the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) has been officially investigating the matter for some time now, while several other government law enforcement agencies are also understood to be keeping a close eye on related developments.

Insiders also say the Meremeta/TANGOLD investigation is among five major grand corruption cases that the PCCB plans to send to court for prosecution this year, if it gets the go-ahead from higher authorities in government.

THISDAY has learnt that apart from the PCCB, the Tanzania Intelligence and Security Service (TISS) and the police's own criminal investigations department (CID) have also been trailing the dubious gold mining project involving both Meremeta and now TANGOLD.

These latest revelations cast fresh doubts on claims by Prime Minister Mizengo Pinda that the matter is a classified military secret involving ''national security''.

''If Meremeta and TANGOLD were truly classified military projects, why would the government's own corruption watchdog (PCCB) be investigating these companies?'' queried one source.

According to our findings, local detectives have so far visited the UK, South Africa and Mauritius to trace key information about the projects.

Records show that Meremeta was registered in the Isle of Man (UK) in April 1997. On the other hand, Triennex (PTY) Limited - a private company that entered into a 50-50 joint venture arrangement with the Tanzanian government to run the Meremeta project - is headquartered in South Africa.

A likely interest in the investigative visit to Mauritius is the fact that TANGOLD Limited, which took over the operations of Meremeta after it went bankrupt, was registered in that island nation as an offshore company in April 2005.

The government's law enforcement agencies are understood to have been trailing the dubious gold mining operations involving Meremeta and TANGOLD at the Buhemba mine in Mara Region since 2006.

Our informed sources say at least one top CID officer, identified as Senior Superintendent of Police (SSP) Ernest Sakawa, was making covert inquiries about the Meremeta project even before an official PCCB investigation led by a senior bureau official, Dunia Kaongo, began.

The sources say police investigators have also visited the Buhemba mine as part of their probe.

Questions about the whole affair started to emerge in 2005/06, when the Bank of Tanzania (BoT) paid a staggering $118m (approx. 150bn/-) to Nedcor Trade Services Limited of South Africa to offset a loan given to Meremeta, which had gone bankrupt.

The BoT is understood to have raised the funds to pay off the loan to Meremeta through a 155bn/- Treasury bond, raising serious audit queries in the process.

Investigations by THISDAY have also established that the BoT paid another $13.34m (approx. 17bn/-) to TANGOLD through an account at the National Bank of Commerce Limited's Corporate Branch in Dar es Salaam.

After registration in Mauritius in April 2005, the offshore TANGOLD company was in February 2006 given a certificate of compliance by the Business Registration and Licensing Authority (BRELA) to legally operate in Tanzania.

Its rather prominent shareholders included former BoT governor Daudi Ballali (now deceased); the then Minister for East African Cooperation, Andrew Chenge; the Permanent Secretary in the Ministry of Finance, Gray Mgonja; the then PS in the Ministry of Energy and Minerals, Patrick Rutabanzibwa; and the then PS in the Ministry of Livestock Development, Vincent Mrisho.

While the Ministry of Energy and Minerals has claimed that TANGOLD is 100% owned by the government, the company's articles of association has provisions that allow the listed shareholders to transfer all or part of their shares to their next of kin.

TANGOLD is also not officially listed at the Treasury Registry among companies partly or wholly-owned by the government, and has thus not been subjected to statutory auditing by the Controller and Auditor General (CAG).

When addressing the National Assembly in Dodoma last week, Premier Pinda appeared strangely evasive in his attempts to explain to curious MPs why Meremeta was a classified military operation, as he had controversially claimed.
 
Am praying for the day kiongozi yeyote yule wa serikali atakaposimama na kuomba radhi ya kweli au kusahihisha msemo wake.
 
Mi nafikiri tufike mahali viongozi wawajibike kwa kauli zao za uwongo zenye malengo ya kuficha ukweli, kuomba radhi isiwe kigezo. Mbona Zitto aliwajibishwa kwa kauli yake bungeni iweje wengine tuseme waombe radhi tu ??
 
Mi nafikiri tufike mahali viongozi wawajibike kwa kauli zao za uwongo zenye malengo ya kuficha ukweli, kuomba radhi isiwe kigezo. Mbona Zitto aliwajibishwa kwa kauli yake bungeni iweje wengine tuseme waombe radhi tu ??

CCM hawana tabia ya kuwajibisha watu, ndio maana unaona wanapondea sana kitendo cha wangwe kusimamishwa uongozi. Huyu Pinda ataendeleza madudu na kusema uongo bungeni lakini hakuna atakayemwajibisha kwa vile ccm ni chama kichafu tu na hakipendi watu kuwajibika kwa vitendo vyao
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom