Pinda angalia serikali inavyopaswa kuwabana mawaziri kuhusu magari!!

Ubumuntu

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
14,314
10,775
http://www.dft.gov.uk/gcda/cars/default.php


"Ministers are permitted to use an official car for official business and for home to office journeys within a reasonable distance of London on the understanding that they would normally be carrying classified papers on which they would be working. Where practicable, Ministers are encouraged to use public transport."


Sasa ndugu Pinda, nini kinakufanya hushindwe kuwaagiza mawaziri wako wazingatie haya??
Hivi mkienda kuzurura Ulaya uwa hata mjifunzi wenzenu wanavyofanya??
Kama waziri toka nchi ambayo inakupa msaada anashauriwa kupanda usafiri wa umma au atumie gari za serikali kwa kuzikodisha, kwanini waziri toka kwa nchi unayosema masikini hasifanye hivyo???
Ndugu Pinda, hivi wewe ni waziri mkuu au waziri mkuu kivuli???
 
Je Tanzania mna miundombinu mizuri na mabasi mazuri ya kuweza kuwachukua hawa waheshimiwa.

Msije mkamuiga tembo kunya xxxxxx mkapasuka msamba.
 
Hivi ndivyo vitu ambavyo viongozi wetu kwa pepo la ubinafsi hawawezi kuvufanya.....very striking na vinavyoeleweka maana hapa kwetu hutofautishi gari binafsi na la ofisi, zaidi ni zile namba tu za ST
 
Je Tanzania mna miundombinu mizuri na mabasi mazuri ya kuweza kuwachukua hawa waheshimiwa.

Msije mkamuiga tembo kunya xxxxxx mkapasuka msamba.

Kaka swali zuri sana ila hebu nikuulize ka swali ka nyongeza na kakizushi ka swali lako...Hivi kama wasipopata ile suluba ambayo mimi na wewe tunaipata kwenye hizi public transport (kama upo Tanzania na unatumia japo nahisi hupo Tz kwa maneno hayo ya kwenye red) je watajua umuhimu wa kuzitumia?.......

Unajua ndio maana tunapopiga kelele za kero za usafiri hawatuelewi kwa kuwa wao trafiki wanasimamisha njia zote wapite wao, nyambafu zao...hadi wakina NAPE wa CCM eti nao wanasafishiwa njia na trafiki!! Upuuzi mkubwa kabisa huu
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Je Tanzania mna miundombinu mizuri na mabasi mazuri ya kuweza kuwachukua hawa waheshimiwa.

Msije mkamuiga tembo kunya xxxxxx mkapasuka msamba.

Waheshiomiwa ni kina nani?
kwani kabla yapo walikuwa wanaitwaje?
hawajawahi kupanda hizo public transport au?
kama wapo kikazi basi watapewa usafiri ila kama wapo na mishemishe zao basi wajitegemee!
 
Je Tanzania mna miundombinu mizuri na mabasi mazuri ya kuweza kuwachukua hawa waheshimiwa.

Msije mkamuiga tembo kunya xxxxxx mkapasuka msamba.

Mkuu heshima kwako!

Hao unaowaita waheshimiwa hawajui adha ya matatizo ya usafiri wa umma ndio maana linapokuja suala la kuboresha miundombinu ya usafiri wa umma, wanaleta usanii na longolongo!!
Hawapati hata adha ya bei kubwa ya petroli; hawapati adha ya kubanana kwenye daladala ziendazo Mbagala, Tegeta, Kimara n.k. Hawapati adha ya kufa au kujeruwiwa na ajali katika mabasi yaendayo mikoani!!

Hao unaowaita waheshimiwa wanashindwa nini kupanda basi kwenda Dodoma, bungeni?? Pengine wangekua wanapanda wangepata uchungu wa kutafuta suluhisho la kudumu dhidi ya ajali hizo.

Mkuu, haya mambo yanawezekana sana, ila hakuna political will kwasababu wanasiasa wetu hawajui adha ya usafiri wa umma!
 
tena wapande daladala lililojaa kukiwa na foleni kuubwa awe amesimama
daladala lenyewe liwe kipanya tena kile kifupii kinachobidi kuinamana ndo itakuwa vizuri zaidi
loool wangejua tunapata shida kiasi gani huku uswazi
 
hawa jamaa ni kitu huwezi hamini lakini hawatumii muda kufikiri juu ya umma wanaouongoza na suala linalohusu dignity ya binadamu (kwa Tanzania) hawajui kuwa ndiyo wamelibeba. Haiwezi kuwa kitu kizuri kujua mambo haya miaka 30 ijayo!
Mtoto wa mkulima hana habari.
 
Je Tanzania mna miundombinu mizuri na mabasi mazuri ya kuweza kuwachukua hawa waheshimiwa.

Msije mkamuiga tembo kunya xxxxxx mkapasuka msamba.

Hivi ukiwa mheshimiwa unakuwa binadamu kuliko wengine eeh?
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom