Elections 2010 Pinda amweka kiti moto Mwema sakata la Arusha

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,172
Pinda amweka kiti moto Mwema sakata la Arusha
Monday, 10 January 2011 21:39

Mwandishi Wetu
pinda1.jpg
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ameingilia kati vurugu zilizotokea Arusha kutokana na mvutano wa kisiasa baina ya CCM na Chadema kuhusu suala la Meya wa Jiji la Arusha akitaka kuwapo suluhisho la kudumu baina ya pande mbili hizo.

Taarifa za ndani ya kikao alichokiitisha Waziri Mkuu Pinda zilizolifikia Mwananchi jana zilieleza kuwa alikutana na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwamo Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema ambaye analaumiwa na jamii kwa kuwa moja ya chanzo cha vurugu hizo na Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha ofisini kwake kuanzia saa saba mchana hadi saa kumi na moja jioni.

"Waziri Mkuu amekutana na viongozi hao, lakini kikubwa alichokuwa akitaka ni kukutana na Chadema na akataka kujifahamu katika sakata hilo nini ushiriki wa polisi katika mauaji ya raia na hasa kutokana na tuhuma mbalimbali zinazoelekezwa kwao ambapo watu watatu waliokuwamo katika maandamano hayo walipigwa risasi za moto na jeshi hilo," kilisema chanzo hicho cha habari kutoka ndani ya kikao hicho.

Viongozi hao walimpa taarifa Waziri Mkuu Pinda ya jinsi tukio zima la Arusha lilivyotokea wakibainisha baadhi ya mambo ambayo yalijitokeza katika sakata hilo zima.

Januari 5, mwaka huu, Jeshi la Polisi liliwaua watu watatu kwa kuwapiga risasi na kuwajeruhi wengine zaidi ya 20 katika harakati za kudhibiti maandamano ya amani yaliyofanywa na wafuasi wa Chadema mkoani humo kupinga utaratibu uliotumika kupata meya wa jiji hilo.

Chanzo cha habari cha Mwananchi kilieleza kuwa katika suala hilo, Waziri Mkuu alisema kuwa aliamua kuchukua hatua hiyo ili kuweza kupata suluhisho la kudumu katika sakata hilo ambalo lilmesababisha ukosefu wa amani ndani ya jiji hilo na athari zake kuenea maeneo mbalimbali nchini.

Katika kukabiliana na tatizo hilo, chanzo hicho cha habari kililieleza Mwananchi kwamba Waziri Mkuu alitoa kauli kuwa atakutana na Chadema na kuzungumza nao ingawa hakueleza ni lini atafanya hivyo kwa lengo la kumaliza mgogoro huo wa kisiasa ambao unazidi kuchukua sura mpya kila siku.

"Unajua suala hili lilionyesha kumkera Waziri Mkuu na akatoa mfano wa suluhisho linaloweza kuchukuliwa kuwa ni mfano wa ilivyotokea katika manispaa ya Kigoma katika uongozi uliopita ambapo CCM waliongoza kipindi cha miaka miwili na nusu ya mwanzo na hatimaye miaka miwili na nusu ya mwisho kikaongoza Chadema,"kilieleza chanzo hicho.

Ilielezwa pia kwamba lengo la kikao hicho cha Waziri Mkuu Pinda ni kuondoa utata uliopo sasa kwenye sakata zima la umeya wa Arusha na kurejesha hali ya kisiasa katika hali ya kawaida.

Waziri Mkuu anachukua hatua hiyo wakati tayari kukiwa kumeshaibuka sintofahamu baada ya maaskofu wa makanisa ya Kikristo mkoani Arusha, kutoa tamko la pamoja la kutomtambua Meya wa Jiji la Arusha aliyeteuliwa na CCM, Gaudence Lyimo, Januari 7 mwaka huu.

Serikali kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha alishatoa tamko kwamba vurugu zilizotokea Arusha ni tatizo la kisiasa ambalo pia litapaswa kushughulikiwa kisiasa.

Lakini, Chama Cha Mapinduzi(CCM) mkoa wa Arusha, kikawataka maaskofu mkoani Arusha kuvua majoho na kutangaza kuingia katika siasa, badala ya kuingilia mambo ya siasa yasiyowahusu ya Meya wa Jiji la Arusha.

Wakati katibu huyo wa mkoa wa CCM akieleza hayo, Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuf Makamba alienda mbali zaidi na kuwataka maaskofu hao waende mahakamani au wawashauri Chadema kufanya hivyo kwa lengo la kupinga matokeo ya umeya.

Makamba alisisitiza kuwa msimamo wa CCM ni kwamba chama hicho ndicho kilichoshinda katika uchaguzi huo wa umeya Arusha.

Tofauti na Makamba na Chatanda, juzi Waziri Mkuu wa zamani, John Malecela, akakemea vikali akisema kuwa CCM imewakosea adabu maaskofu hivyo inapaswa kukutana nao na kuwaomba radhi.

Akizungumza na Mwananchi, Malecela alisema kitendo cha kuwashambulia maaskofu hao kilichofanywa na CCM mkoani Arusha ikiwa ni pamoja na kuwataka wavue majoho na kuingia kwenye siasa, ni utovu wa nidhamu. Malecela alitaka juhudi za haraka kumaliza mzozo huo zifanyike.

Mbali na Malecele, mwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa CCM, Peter Kisumo juzi hiyo hiyo alivitaka vyama vya Chadema na CCM kuacha kiburi na kukaa meza moja kutafuta muafaka wa mgogoro wa kisiasa jijini Arusha.

“Arusha ni tukio moja baya sana na ni baya kwa maana kwamba mimi kama raia wa Tanzania ninashituka kuona tunashindwa kitu tunachokiita political management (utawala wa siasa) na hili ni jambo baya sana,”alisema Kisumo.

Wakati huo huo, Rais Jakaya Kikwete amesema kwamba amesononeshwa na tukio la vurugu zilizotokea Aruisha wiki iliyotokea na kusababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi zaidi ya 20.

Rais Kikwete alisema atahakikisha hatua zinachukuliwa ili kujenga mazingira ambayo hayataruhusu tukio jingine kama hilo kutokea tena siku zijazo.

Azimio hilo la Kikwete lilielezwa jana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mpainduzi (CCM), Pius Msekwa katika mahojiano na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kupitia kituo chake cha televisheni cha TBC1.

“Mheshimiwa Rais Kikwete amesononeshwa sana na kile kilichotokea katika Manispaa ya Arusha,” alisema Msekwa akinukuu kauli ya Rais Kikwete kuhusiana na tukio hilo lililotokana na maandamano ya Chadema kutawazwa umeya wa Jiji hilo, Gaudence Lyimo wa CCM.

Kwa sababu hiyo, Msekwa alisema wameamua kikao cha Kamati Kuu ya CCM kukutana haraka iwezekanavyo ili kujadili suala hilo na kuliwekea msimamo utakaotoa suluhishio la kudumu.

Msekwa alikataa kata kata kutoa maoni yake kuhusiana na tukio hilo ambalo limeonekana kulitikisa taifa na kuwafanya wanasiasa, wasomi, viongozi wa kawaida kulizungumzia kwa hisia tofauti.
 
Tunachotaka kuona ni watu wanawajibika na kuachia ngazi siyo blaa...........blaaa....
 
[CCM CCM OOOOH CHAMA CHA CHA MAPINDUZI,,CCM NUMBER ONEEEEE

Msekwa alikataa kata kata kutoa maoni yake kuhusiana na tukio hilo ambalo limeonekana kulitikisa taifa na kuwafanya wanasiasa, wasomi, viongozi wa kawaida kulizungumzia kwa hisia tofauti.[/QUOTE]
 
Nothing is new here! Huyu mshikaji ni hodari wa kupiga dana dana! Kumbukeni alivyofanya kwenye maazimio ya bunge kuhusu richmond! Kinyaa!
Anyone who doesn't take truth seriously in small matters cannot be trusted in large ones either.
 
Alikuwa wapi wakati Mary Chitanda anahudhuria mkutano wa madiwani Arusha na hatimaye kuwa chanzo cha vurugu hizo? Watu wakifa ndiyo anaanza kuchangamka. Pinda anaonekana anapwaya hata kama akijifanya yupo makini.

Alienda kuomba msamaha kule Sumbawanga kwa niaba ya serikali wakati anaowaombea msamaha walikuwa hawana mpango wowote wa kufanya hivyo baada ya kukashifu imani ya Kikatoliki. Alikuwa wapi kuwashauri kuomba msamaha kabla.

Alitupiga dana dana kwenye suala la utekelezaji wa maazimio ya bunge kuhusu Richmod. Katika suala la kesi ya Dowans anatuambia kuwa Tanzania inajali utawala wa sheria hivyo Dowans watalipwa. Akiulizwa Dowans ni ya kina nani hajui kujibu.
 
binafsi mi huwa namuona huyu jamaa pinda ni muoga wa kuchukua hatua hinyo chochote anachosema huwa sikiamini
 
Mkuu huyu ni mtaalamu wa kuwacheza watanzia. Anajua ni lugha ipi mnataka kuisikia na anawapa mistari yake. Kuna hoja na maswali mbalimbali yanayohusu mustakabali wa taifa ambayo anaizima wa maneno matupu. Ukianzania na ile ya matumizi mabaya ya kodi zetu (hususani ile ya magari ya kifahari, akadai ya kuwa ameyapiga stop, kesho na kesho kutwa na yamejaa mtaani ilihali na yeye pia analo la Series 200 la kwake), mambo ya Richmond/Dowans, mauaji ya walemavu wa ngozi (machozi ya uongo bungeni) n.k

Mtoto wa mkulima kweli kweli huyu
 
huyu mzee ni mnafiki tu,hana lolote kashaambukizwa maneno mei na Mkwere,kwani tangia aanze kuongea utekelezaji wa mambo hamna,sasa haya mambo yalipofikia bora atulie tu muda ndio utakaowaumbua na si kinginecho.
Pinda aache unafiki,sound zake tumezichoka,
 
Ukweli hakuna cha maana wanachotaka kukifanya zaidi ya kuwadanganya watanzania kuwa wanachukua hatua. We angalia maamuzi walioyatoa jana hiyo wanayoiita kamati ya CCM.
 
Nothing is new here! Huyu mshikaji ni hodari wa kupiga dana dana! Kumbukeni alivyofanya kwenye maazimio ya bunge kuhusu richmond! Kinyaa!
Anyone who doesn't take truth seriously in small matters cannot be trusted in large ones either.

I totally agree with you. KWa sasa Mh Pinda si mtu wa kuwa na imani naye sana, yeye alitakiwa kutoa leadership kwenye issue hii nzima. He is the head of government operations kwa hiyo anajua au alitakiwa ajue kinachoendelea Arusha, bila hata ya kukutana na wanachadema or wanaccm. NI kama anaingiza tu jina lake kwenye issue ili ionekane serikali iko serious, lakini nothing will happen
 
Msitegemee kitu kutoka kwa PINDa, huyu mzee ni mwoga hujaona. Tangu aingie magogoni ni maamuzi gani ya kuwajibisha watendaji we serikali walioboronga!! nani kesha mpa hata warning letter
 
Hapo umenena kweli mkuu smz. Upande mwingine ukiangalia speech yake ya jana kwenye semina ya wabunge wa sisiem sehemu ya kusema mengi inatakiwa kuwa kwenye kamati ya wabunge wa sisiem labda huko ndiko huwa anawakaripia watu wake maana kwa mujibu wake issue ikifika bungeni wote wawe kitu kimoja ... , ni argument etc .
 
Pamoja na kuwa Mzee Mizengo ni mwendeshaji mkuu wa serikali, tusisahau kuwa ni mtu wa CCM, na utaratibu tuliojiwekea Watanzania ni kuwa jukumu la mwanzo la mwanachama wa chama chochote ni kulinda maslahi ya chama chake. Mizengo hawezi kuimba nyimbo tafauti na wenzake, vyenginevyo atakuwa msaliti wa chama chake. Hapa hapaangaliwi maslahi ya Taifa bali ya chama. Kwa hiyo Watanzania wenzangu, tusitegemee makubwa kutoka kwa "mtoto wa mkulima"; sisi tulie tu. Kama tuna ubavu tuiondoshe CCM madarakani, "by hook or crook".
 
Jukumu la kwanza la mtanzania ni kulinda maslahi ya Taifa, jukumu la pili ni kulinda maslahi ya chama na jukumu la tatu ni kuangalia maslahi yake binafsi. So Kama uko CCM, CHADEMA, CUF, au DP, ni lazima kwanza Tanzania iwe mbele ya chama na wewe binafsi.

Hili ni moja ya mambo tunayotakiwa kuyaweka kwenye katiba na kila anayechukua nafasi ya uongozi ni lazima aape kuwa atafanya hivyo. Na akienda kinyume basi kuwa na msingi wa kumchukulia hatua.

Kwenye issue ya DOwans unaona wazi kabisa kuwa Rostam na wenzake wameweka maslahi binfasi mbele na wanaliangamza taifa, CC imeweka maslahi ya Chama mbele kuliko maslahi ya taifa.

It is very ridiculous kusema kuwa eti kwa kiwa ICC imeamua basi ni lazima tutekeleze, that is crazy, hatukujiunga na ICC ili kuifanya i-facilitate wizi wa fedha za umma, tunaweza kujitoa ICC na tusituekeleze maamuzi yao. We are a republic we should behave like one, not like a banana repulic.

Issue hii hakuna haja ya kujiuliza mara mbili wala mara tatu, pure and simple ni wizi tu wa fedha za umma, unatakiwa kuzuiwa. Hata kama itakuwa kwa kujitoa ICC au kuunda Tume nyingine kama ya Mwakyembe.
 
Tatizo letu la kwanza ni ubovu wa katiba tuliyonayo kama ulivyosema, lakini halitaishia kwa kuandika mpya tu bali kuwa makini katika ufuataji na utekelezaji wake: kuilinda. Hawa jamaa huwa wanaapa (samahani kwa hili neno - mpaka na mamazao), lakini kumbe ni viapo vya uongo, baadaye wanatafuna na kufanya uzembe na mali ya umma, na hakuna hatua wanayochukuliwa.:disapointed:
 
Back
Top Bottom