Pinda amweka kiti moto Mwema sakata la Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda amweka kiti moto Mwema sakata la Arusha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 11, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ameingilia kati vurugu zilizotokea Arusha kutokana na mvutano wa kisiasa baina ya CCM na Chadema kuhusu suala la Meya wa Jiji la Arusha akitaka kuwapo suluhisho la kudumu baina ya pande mbili hizo.

  Taarifa za ndani ya kikao alichokiitisha Waziri Mkuu Pinda zilizolifikia Mwananchi jana zilieleza kuwa alikutana na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwamo Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema ambaye analaumiwa na jamii kwa kuwa moja ya chanzo cha vurugu hizo na Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha ofisini kwake kuanzia saa saba mchana hadi saa kumi na moja jioni.

  "Waziri Mkuu amekutana na viongozi hao, lakini kikubwa alichokuwa akitaka ni kukutana na Chadema na akataka kujifahamu katika sakata hilo nini ushiriki wa polisi katika mauaji ya raia na hasa kutokana na tuhuma mbalimbali zinazoelekezwa kwao ambapo watu watatu waliokuwamo katika maandamano hayo walipigwa risasi za moto na jeshi hilo," kilisema chanzo hicho cha habari kutoka ndani ya kikao hicho.

  Viongozi hao walimpa taarifa Waziri Mkuu Pinda ya jinsi tukio zima la Arusha lilivyotokea wakibainisha baadhi ya mambo ambayo yalijitokeza katika sakata hilo zima.

  Januari 5, mwaka huu, Jeshi la Polisi liliwaua watu watatu kwa kuwapiga risasi na kuwajeruhi wengine zaidi ya 20 katika harakati za kudhibiti maandamano ya amani yaliyofanywa na wafuasi wa Chadema mkoani humo kupinga utaratibu uliotumika kupata meya wa jiji hilo.


  Chanzo cha habari cha Mwananchi kilieleza kuwa katika suala hilo, Waziri Mkuu alisema kuwa aliamua kuchukua hatua hiyo ili kuweza kupata suluhisho la kudumu katika sakata hilo ambalo lilmesababisha ukosefu wa amani ndani ya jiji hilo na athari zake kuenea maeneo mbalimbali nchini.

  Katika kukabiliana na tatizo hilo, chanzo hicho cha habari kililieleza Mwananchi kwamba Waziri Mkuu alitoa kauli kuwa atakutana na Chadema na kuzungumza nao ingawa hakueleza ni lini atafanya hivyo kwa lengo la kumaliza mgogoro huo wa kisiasa ambao unazidi kuchukua sura mpya kila siku.

  "Unajua suala hili lilionyesha kumkera Waziri Mkuu na akatoa mfano wa suluhisho linaloweza kuchukuliwa kuwa ni mfano wa ilivyotokea katika manispaa ya Kigoma katika uongozi uliopita ambapo CCM waliongoza kipindi cha miaka miwili na nusu ya mwanzo na hatimaye miaka miwili na nusu ya mwisho kikaongoza Chadema,"kilieleza chanzo hicho.

  Ilielezwa pia kwamba lengo la kikao hicho cha Waziri Mkuu Pinda ni kuondoa utata uliopo sasa kwenye sakata zima la umeya wa Arusha na kurejesha hali ya kisiasa katika hali ya kawaida.

  Waziri Mkuu anachukua hatua hiyo wakati tayari kukiwa kumeshaibuka sintofahamu baada ya maaskofu wa makanisa ya Kikristo mkoani Arusha, kutoa tamko la pamoja la kutomtambua Meya wa Jiji la Arusha aliyeteuliwa na CCM, Gaudence Lyimo, Januari 7 mwaka huu.

  Serikali kupitia kwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha alishatoa tamko kwamba vurugu zilizotokea Arusha ni tatizo la kisiasa ambalo pia litapaswa kushughulikiwa kisiasa.

  Lakini, Chama Cha Mapinduzi(CCM) mkoa wa Arusha, kikawataka maaskofu mkoani Arusha kuvua majoho na kutangaza kuingia katika siasa, badala ya kuingilia mambo ya siasa yasiyowahusu ya Meya wa Jiji la Arusha.

  Wakati katibu huyo wa mkoa wa CCM akieleza hayo, Katibu Mkuu wa chama hicho, Yusuf Makamba alienda mbali zaidi na kuwataka maaskofu hao waende mahakamani au wawashauri Chadema kufanya hivyo kwa lengo la kupinga matokeo ya umeya.

  Makamba alisisitiza kuwa msimamo wa CCM ni kwamba chama hicho ndicho kilichoshinda katika uchaguzi huo wa umeya Arusha.

  Tofauti na Makamba na Chatanda, juzi Waziri Mkuu wa zamani, John Malecela, akakemea vikali akisema kuwa CCM imewakosea adabu maaskofu hivyo inapaswa kukutana nao na kuwaomba radhi.

  Akizungumza na Mwananchi, Malecela alisema kitendo cha kuwashambulia maaskofu hao kilichofanywa na CCM mkoani Arusha ikiwa ni pamoja na kuwataka wavue majoho na kuingia kwenye siasa, ni utovu wa nidhamu. Malecela alitaka juhudi za haraka kumaliza mzozo huo zifanyike.

  Mbali na Malecele, mwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa CCM, Peter Kisumo juzi hiyo hiyo alivitaka vyama vya Chadema na CCM kuacha kiburi na kukaa meza moja kutafuta muafaka wa mgogoro wa kisiasa jijini Arusha.

  “Arusha ni tukio moja baya sana na ni baya kwa maana kwamba mimi kama raia wa Tanzania ninashituka kuona tunashindwa kitu tunachokiita political management (utawala wa siasa) na hili ni jambo baya sana,”alisema Kisumo.

  Wakati huo huo, Rais Jakaya Kikwete amesema kwamba amesononeshwa na tukio la vurugu zilizotokea Aruisha wiki iliyotokea na kusababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi zaidi ya 20.

  Rais Kikwete alisema atahakikisha hatua zinachukuliwa ili kujenga mazingira ambayo hayataruhusu tukio jingine kama hilo kutokea tena siku zijazo.

  Azimio hilo la Kikwete lilielezwa jana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mpainduzi (CCM), Pius Msekwa katika mahojiano na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kupitia kituo chake cha televisheni cha TBC1.

  “Mheshimiwa Rais Kikwete amesononeshwa sana na kile kilichotokea katika Manispaa ya Arusha,” alisema Msekwa akinukuu kauli ya Rais Kikwete kuhusiana na tukio hilo lililotokana na maandamano ya Chadema kutawazwa umeya wa Jiji hilo, Gaudence Lyimo wa CCM.

  Kwa sababu hiyo, Msekwa alisema wameamua kikao cha Kamati Kuu ya CCM kukutana haraka iwezekanavyo ili kujadili suala hilo na kuliwekea msimamo utakaotoa suluhishio la kudumu.

  Msekwa alikataa kata kata kutoa maoni yake kuhusiana na tukio hilo ambalo limeonekana kulitikisa taifa na kuwafanya wanasiasa, wasomi, viongozi wa kawaida kulizungumzia kwa hisia tofauti.

  Pinda amweka kiti moto Mwema sakata la Arusha
   
 2. czar

  czar JF-Expert Member

  #2
  Jan 11, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 340
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  How?
   
 3. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #3
  Jan 11, 2011
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,970
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Inabidi serikali iache kichwa ngumu na iiachane na makamba msema ovyo
   
 4. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #4
  Jan 11, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Alichokifanya Pinda kinapaswa kiwe mfano wa kuigwa!!nampongeza kwa hilo!!
   
 5. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hakuna kiti moto hapo
  Alikuwa anampongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kuwakomesha chadema kwani anajua kwamba saidi mwema alitoa amri batili kuzuia maandamano ya chadema yaliyokuwa na "kibali' cha polisi cha kutoa ulinzi kwa waandamanaji na badala yake akakubali kuburuzwa na wanaccm kusababisha machafuko na mauaji kwa raia wasiokuwa na hatia.
  Waziri mkuu huyo huyo ndiye alikuwa kimya muda wote serikali yake ikikiuka taratibu na kanuni za uchaguzi wa meya wa arusha pamoja na maeneo mengine mengi, sasa leo amepata wapi uchungu na huruma kwa wananchi hadi amuweke kiti moto said mwema?
  Chanzo cha purukushani zote hizi ni yeye mizengo pinda wala katika hili hana namna ya kukwepa kuwajibika.
   
 6. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #6
  Jan 11, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  It is amazingly!!I am puzzled,your question is too vague!can you please crarify what specific issue do you want to know on this thread!!
   
 7. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #7
  Jan 11, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  msukule pinda leo kaongea!
   
 8. Keynes

  Keynes JF-Expert Member

  #8
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 499
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Mi pinda nshapoteza imani kwake siku nyingi so hata nikiona anaongea kitu mi wala sitilii maanani tena.
  He acting like toothless dog!!
   
 9. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #9
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,523
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Pinda ajue kwamba hakuna demokrasia ya mezani . Uchaguzi ulio huru na wa haki ndio kilio cha wananchi wa Arusha. Huyo mama anayeleta vurugu Arusha Chitanda arudishwe kwao Tanga. Hizi mbinu za Ccm ni chafu hazifai kwa nyakati hizi za watu walioamka ,wanaojua haki zao , walioichoka ccm na waliotayari kufa kwa ajili ya nchi yao.
   
 10. m

  matambo JF-Expert Member

  #10
  Jan 11, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 728
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  pinda hana lolote huyu, ni mnafiki sana tu,
   
 11. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #11
  Jan 11, 2011
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mhhhhh TUKUTUKU wampongeza Pinda kwa lipi alilolifanya??? Kuongea na IGP na Shamsi Vuai Nahodha???. Sidhani kama anastahili kupongezwa!!. Akiwa kama Waziri Mkuu, Chaguzi zote za Mameya zinazoendelea ziko chini ya Ofisi yake, lakini hujasikia akitoa angalizo au ufafanuzi wowote pale panapotokea utata au vurugu.Anzia Mwanza, Kigoma, Njoo Arusha, nenda Hai kote huko kumekuwa na vurugu lakini mhh yuko kimyaaaaaaaaa!!!
   
 12. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #12
  Jan 11, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hakuna kiti moto wala nini, alikuwa wapi tangu malalamiko yaanze kutolewa kuwa kuna hujuma ktk uchaguzi wa meya arusha?hana lolote huyo mi huwa namwita mzee wa mchakato,maana yeye kila kitu tupo kwenye mchakato
   
 13. Jeremiah

  Jeremiah JF-Expert Member

  #13
  Jan 11, 2011
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 642
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Maskini mtoto wa mkulima hata meno ya kushughulika na chochote
   
 14. babayah67

  babayah67 JF-Expert Member

  #14
  Jan 11, 2011
  Joined: Mar 28, 2008
  Messages: 493
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mhh Nahisi kama kichwa cha habari hii hakiendani hasa na yaliyomo ndani ya habari yenyewe maana sijaona sehemu yoyote ambapo Pinda Alimweka kiti moto Mwema, zaidi ya kuwa alimwita ofisini kutaka tu kujua hali ya usalama ikoje mjini arusha na sehemu zote zenye wabunge wengi wa CDM
   
 15. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #15
  Jan 11, 2011
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,236
  Likes Received: 928
  Trophy Points: 280
  He need to do more,tumechoka na kauli za Pinda we need actions
   
 16. K

  Kishalu JF-Expert Member

  #16
  Jan 11, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 850
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  Tukiangalia kwa undani kuhusu hali halisi ya Arusha lazima tuanze na Pinda kwa sababu ipo ndani ya kazi yake na tangia chaguzi zianze kufanyika na kutokea machafuko kila penye upinzani kama Mwanza hai,kigoma na kwingine hatujamzikia kwa maana hiyo yeye ndiye anapanga hizo njama ili ccm washinde kiujanja,pili mauaji yametokea tangia 5/01/2011 leo ni siku ya 5 ndiyo anaongea na IGM na waziri wa mambo ya ndani na kuongea nao hatujui alikuwa anawapongeza kwa kazi ya kusambaratisha maandamano ya chadema au mikakati ya kukaa mezani kwa uzuhilisho, sasa hapa lipi la kumpongeza PM Pinda
  MM naungani na mjumbe aliyesema kuwa ni mzee wa mchakato na anatakiwa awajibishwe kwa kusababisha maisha ya watu kupotea
   
 17. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #17
  Jan 11, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  ndo amejua leo kwamba polisi waliua wananchi arusha?
   
 18. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #18
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Angalau wapo wenye akili CCM, nilidhani vichwa vyote ni type ya makamba, tambwe na yule katibu wao wa arusha. Kumbe!
   
 19. Mabel

  Mabel JF-Expert Member

  #19
  Jan 11, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,018
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Pinda ni SHOCK ABSOBER ya Serikali ya JK
   
 20. M

  Mkare JF-Expert Member

  #20
  Jan 11, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hana lolote... Ndo anakurupuka leo!
   
Loading...