Pinda amuumbua Kikwete

ipo wapi??? hatuwezi changia kitu ambacho hakijaletwa jamvini.... kama unayo habari basi tujeze japo in brief
 
Mussa Mwangoka, Sumbawanga
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ameliangukia Kanisa Katoliki nchini, akiomba radhi kutokana kashfa zilizotolewa kwa kanisa hilo wakati wa mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Pinda aliomba radhi jana mbele ya viongoizi wa madhehebu mbalimbali ya dini kwa niaba ya Serikali na CCM, wakati ambao baadhi ya waumini wa Kanisa Katoliki katika Jimbo la Sumbawanga mkoani Rukwa wametengwa kwa tuhuma kwamba 'walilinajisi' Kanisa katika kusherehekea ushindi wa kisiasa.

Mbali na viongozi wa dini, kikao hicho kilichofanyika jana asubuhi katika Ukumbi wa Libori, pia kiliwashirikisha baadhi ya wazee maarufu wa mjini Sumbawanga.

Wengi waliotengwa na Kanisa hilo wanadaiwa kuwa wanachama wa CCM waliokuwa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi na tuhuma zinazowakabili ni kutoa kauli zilizokinzana na imani za dini zao wakati wa kampeini na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31 mwaka jana.

Katika kikao hicho, Pinda alisema Uchaguzi Mkuu uliopita hakuwa rahisi kama ilivyodhaniwa, na badala yake ulikuwa na changamoto nyingi ikiwemo tofauti za kimtizamo na kiimani hivyo yasamehewe.

"Hali hiyo siyo ilijitokeza tu Sumbawanga... najua tulimkwaza Mhashamu Baba Askofu (Damian Kyaruzi), tumekejeli imani ya dini yake, tunaomba radhi, mimi naomba radhi kwa niaba ya CCM na Serikali si hapa tu, lakini ni maeneo mengi nchini kama vile majimbo ya uchaguzi ya Hai na Same ambapo baadhi ya wagombea katika kuomba kura ya ndiyo walilazimika kutumia baadhi ya maneno yanayotumika katika injili ya mateso" alisema Waziri Mkuu Pinda.

Alisema kuwa kutokana hali hiyo iliyojitokeza chama na Serikali imepata fundisho ambapo katika chaguzi zijazo aliomba viongozi wa dini, Serikali na vyama vya siasa wakae pamoja na kuweka angalizo ili wagombea wajiepushe na kukejeli imani za dini za watu wengine na kuwasihi viongozi hao wa dini nchini nzima kuanza ukurasa mpya ambapo muda mwingi wanapaswa kuutumia kwa ajili ya kuhamasisha maendeleo.

Hayo ni maneno ya pinda na si kama KIKWETE alivyosema bungeni.Mnasemaje????
 
Inaelekea Pinda ni mmoja wa wakatoliki ambao wanahudhuria sana misa lakini hawasomi kabisa katekism.

Kanisa halitoi hukumu kwa kikundi bali kwa mtu mmojammoja. Hivyo hata toba haiombwi kwa kikundi bali kwa muhusika mwenyewe. Aliyekosa huwajibika yeye binafsi wala haombewi msamaha na mwingine.

Wakatoliki wote wanajua hili ndiyo maana hakuna anayekwenda kwenye chumba cha maungamo kutubu dhambi za mwenzake.
 
Sasa kama ameona ni kosa si ujinga kuomba msamaha.. Amefanya vyema sana kuomba msamaha.. Na wakristo wanajua vyema kuwa si vizuri kuweka vinyongo wala si vizuri kutokusamehe...
 
Na wewe ni walewale. Wale hawakumkosea Askofu au Papa. Wamemkosea Mungu kwa kumlinganisha na Kikwete kama Mungu Baba.

Kosa hili hakuna duniani mwenye mwenye mamlaka ya kulisamehe wala mwenye mamlaka ya kuomba wasamehewe.

Maana yake ni kwamba hata Papa hana mamlaka ya kuwasamehe au kuomba wasamehewe kama anavyofanya Pinda.

Kusamehewa kwao kunawezekana pale wao binafsi tena mmojammoja watakapofanya toba hadharani ikiwemo kukiri imani yaani kanuni ya imani.
 
Inaelekea Pinda ni mmoja wa wakatoliki ambao wanahudhuria sana misa lakini hawasomi kabisa katekism.

Kanisa halitoi hukumu kwa kikundi bali kwa mtu mmojammoja. Hivyo hata toba haiombwi kwa kikundi bali kwa muhusika mwenyewe. Aliyekosa huwajibika yeye binafsi wala haombewi msamaha na mwingine.

Wakatoliki wote wanajua hili ndiyo maana hakuna anayekwenda kwenye chumba cha maungamo kutubu dhambi za mwenzake.

Anajari kufanya siasa katika dini, hili swala si la kisiasa hata kidogo, ni suala la kiroho PINDA kaPINDA hapo
 
Nashindwaga kuelewa hivi CCM imewalisha nini wanachama wake?

Yaani wanachama wao mpaka wanawatunishia msuli viongozi wao wa kiroho kisa CCM!
Hilo zindiko walofanya CCM ni kiboko ya njia.
 
Alichofanya Pinda kimepinda,bado hakijanyooka! Hao waliokufuru na kujifananisha na utatu mtakatifu ndo wanapaswa kukiri makosa na kuomba msamaha hadharani. Kisha wakatubu makosa yao.
 
Back
Top Bottom