Pinda amsifu Sitta

Josh Michael

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,523
77
na Mwandishi Wetu, Urambo



WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amemmwagia sifa kemkem Spika wa Bunge, Samuel Sitta akisema amejenga Bunge lenye sifa na umakini.
Pinda ambaye majuzi alimmwagia sifa Mbunge wa Igunga, Rostam Azziz (CCM) akiwataka wananchi wake wampime kwa kazi yake ni si kwa maneno ya bungeni, alisema Sitta amekuwa anaongoza Bunge kwa nia nzuri, na kwamba wanaolalamikia kazi yake ni wapotoshaji.
Alikuwa akihutubia wananchi katika Uwanja wa Jamhuri mjini hapa juzi, akasema Sitta ambaye ni Mbunge wa Urambo, amelifanya Bunge lisifiwe hata nje ya nchi.
Katika kusisitiza hili, Pinda alisema: “Hata watu wa nje wanalisifu Bunge letu…wanasema naam, hili ndilo Bunge…Bunge likicharuka kuhusu ufisadi wanasema hata si bure, nani asiyejua ufisadi? Ufisadi si rushwa? Bunge linachofanya ni watu wawe waadilifu.”
Aliwataka Watanzania waungane katika vita dhidi ya rushwa, kwani imesemwa tangu zamani kwamba rushwa ni adui wa haki.
Kwa takribani miaka miwili, Sitta amekuwa na uhusiano mbaya na baadhi ya vigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wengi wakiwa wabunge wenzake, kuhusu anavyoliendesha Bunge.
Miongoni mwa walioathirika kwa “kazi nzuri ya Sitta” ni Rostam ambaye pamoja na rafiki yake Edward Lowassa (Monduli – CCM) walihusishwa kinamna na kashfa ya Richmond, ambayo ilisababisha Lowassa kujiuzulu wadhifa wake wa Waziri Mkuu.
Kutokana na msimamo wa Sitta na athari za Kamati ya Mwakyembe, CCM iligawanyika makundi mawili, moja upande wa Sitta jingine likiwa upande wa Lowassa na Rostam.
Uhasama wa makundi hayo uliongezeka na kujikita katika vikao vingine vikuu vya maamuzi vya CCM, kiasi kwamba mwaka jana, wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) walimbana Sitta katika moja ya vikao vyao, wakapendekeza avuliwe uanachama na afukuzwe ubunge, kwa maelezo kuwa anatumia vibaya nafasi yake kwa kuiaibisha CCM.
Sitta aliponea chupuchupu baada ya Rais Jakaya Kikwete kuunda Kamati ya Mwinyi, ambayo kwa muda sasa imekuwa ikihaha kuwapatanisha mahasimu hao; na sasa imefanikiwa kupunguza uhasama wa wazi miongoni mwao.
Katika kikao cha 18 cha Bunge kilichomalizika siku chache zilizopita, Sitta aliwashangaza wananchi alipofunga mjadala wa Richmond, huku akitarajiwa atumie fursa hiyo kuibana serikali itekeleze maagizo 23 ya Bunge kuhusu watu waliojihusisha na kashfa hiyo.
Sitta pamoja na wabunge waliokuwa wamejipambanua kuwa ni wapiganaji vita dhidi ya ufisadi wamelazimika kunywea, licha ya kutambua kuwa maazimio muhimu yaliyomtaka Rais Kikwete kuwajibisha waliokumbwa na kashfa hiyo hayakutekelezwa.
Katika kikao cha NEC kilichoisha hivi karibuni, Sitta aligoma kusuluhishwa na Lowassa na kundi lake, akidai kwamba hana ugomvi binafsi, bali anapambana na ufisadi. Kamati ya Mwinyi imeongezewa muda ili iwapatanishe mahasimu hao.
Mara baada ya kikao cha NEC, Pinda alianza ziara ya wiki sita mkoani Tabora; na alipofika Igunga, alitoa kauli ya kumtetea na kumsafisha Rostam kwa kauli ambayo baadhi ya wachambuzi walidai inalidhalilisha Bunge, kwani ilionekana kana kwamba “maneno ya bungeni” si maneno ya maana kwa wananchi kuyatumia kumpima mbunge wao. Aliwataka wananchi wa Igunga wampime Rostam kwa kazi zake jimboni, si kwa “maneno ya bungeni;” Bunge lile lile linaloongozwa na Sitta. Jana Waziri Mkuu alitembelea Wilaya ya Sikonge. Ziara yake mkoani Tabora inatarajiwa kuhitimishwa leo.
 
Yote hiyo ni kusafisha na kufunika na kutibu majeraha kabla ya kwenda kwenye uchaguzi mkuu miezi ijayo, Si alianza Igunga na sasa yupo huko Tabora na pia utakuta wiki ijayo anakwenda Kyela na tena sehemu nyingine kupima joto linakwenda vipi. Sasa hapa Wananchi ndio wanajibu kwa kujua mtu gani safi na nani mchafu na sio siasa za ajabu ajabu kama hivi sasa hivi Tanzania
 
Akasema
“Iwapo mnataka kumchagua tena Rostam zingatieni amewafanyia nini katika ubunge wake. Msisikilize kile kinachosemwa bungeni juu yake. Bunge lina mambo yake, mimi kama Waziri Mkuu nafahamu mambo ya pale bungeni,” alisema Waziri Mkuu.


Leo anasema
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amemmwagia sifa kemkem Spika wa Bunge, Samuel Sitta akisema amejenga Bunge lenye sifa na umakini.
Pinda ambaye majuzi alimmwagia sifa Mbunge wa Igunga, Rostam Azziz (CCM) akiwataka wananchi wake wampime kwa kazi yake ni si kwa maneno ya bungeni, alisema Sitta amekuwa anaongoza Bunge kwa nia nzuri, na kwamba wanaolalamikia kazi yake ni wapotoshaji.
.
thats how politics is...don't waste your time to crake kichwa kuhusu siasa..!!
 
Akasema


Leo anasema

thats how politics is...don't waste your time to crake kichwa kuhusu siasa..!!
Ni kweli kabisa ila politics si mbaya ila players walioko kwenye mchezo huo ndio wanafanya hivyo, Ukisema siasa una maana hata kujitawala na kupanda jinsi gani ya kufuata utaratibu tu wa kuishi
 
PM huyu anafilisika kisiasa mapema kuliko hata nilivyowahi kufikiria, sifahamu ana matatizo gani kichwani kwako. Kwa mwendo huu anajimaliza mwenyewe.
 
Pinda uwaziri mkuu umeshamshinda.

Cheo chake naona ni cha kusifu wana CCM tu hata kama hawastahili sifa zozote. Juzi tu katoka kumsifu Papa fisadi Rostam Aziz, sasa naona itakuwa ni zamu ya kusifiwa Lowassa.
 
Kwa Tanzania na watanzania POLITICS maana yake ni SI-HASA (not real). Mtoto wa mkulima yuko sahihi na asisulubiwe kwa hilo labda lingine
 
Kuwa mwanasiasa bwana ni kazi kubwa. Maana kuna siku unaimba hata chorus ambazo hutaki hata kuzisikia. Ingelikuwa kanisani ungelitoka nje kimya kimya, ila kwenye siasa lazima ukae frontline na kuimba.
 
pinda anasifia kila mtu - bado aende kwa chenge na richmond majimboni kwao akawamwage misifa.
 
Back
Top Bottom