Pinda ametuomba tuchangie tena mradi wa mabasi ya wanafunzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda ametuomba tuchangie tena mradi wa mabasi ya wanafunzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Jun 8, 2010.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Uzinduzi wa mabasi hayo umefanywa jana Dar es Salaam na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete kwa Shirika la Usafiri la Dar es Salaam (Uda) kuhadharishwa mradi usifie mikononi mwake.

  Waziri Mkuu alitangaza kwamba Serikali iko tayari kuwaondolea ushuru watu binafsi, kampuni na mashirika watakaoguswa na kununua mabasi kwa ajili ya mradi huo uliokabidhiwa Uda kwa mkataba na utaratibu maalumu wa uendeshaji.

  “Hatutakubali kuona mradi uliozinduliwa leo ukifa au ukapotea kimaajabu tu,” alisema Pinda.

  Serikali yetu ni ya ajabu kweli, bila aibu inawaomba wananchi wachangie tena??, mbona hatujaambiwa yale mabasi karibu 20 tuliyochangia na kuwapa UVCCM yaliko, halafu anajua UDA ni shirika linalochungulia kaburi kama siyo kufa still anakabidhi mradi mkubwa kama huo, he must be joking.

  Natabiri mradi huu tayari umeshakufa kabla ya kuanza, stay tuned.
   
 2. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  100%,.....No comments![​IMG]
   
 3. J

  JO KIBAHA Member

  #3
  Jun 9, 2010
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu
  Tunashukuru kwa hilo!`ila cha kushangaza na kusikitisha juu ya mradi huu jamani tusiibuke tu na "kuiga Mambo" CRDB na wizara zote husika zikumbuke kuwa Chama cha madereva na makonda cha DCA Dar Mlandizi kilisha kaa nao vikao na badala yake kuishia kuwapiga chenga na kumbe nia ilikuwa ni kuiba MAWAZO yao na kuyaweka katika miradi yao, hii ina maanisha kuwa ipo siku kama Waziri Mkuu wetu alivyosema inawezekana kabisa wala Mradi huu usifike popote na UTAKUFA TU! kwa vile haukubuniwa kimakini na wahusika au watu wenye kuona mbali ni watu wachache wameulukia na kuuweka katika shirika la UDA ambalo kwa historia yake ni MFU! itakuwa aibu na fedheha kubwa sana kwa jambo hili kujitokeza, hapa la msingi ni kuwa VIONGOZI mliopewa mamlaka haya muwe wabunifu ninyi wenyewe si kwa kuiga yaliyotayarishwa na wengine kama hawa wa CHAMA CHA MADEREVA NA MAKONDA WA DAR MLANDIZI, hamjawatendea haki hata kidogo, wizara husika na hao wa CRDB kwa vile tayari waliisha fika hapo ofisini penu kuomba mikopo ya mabasi hayo bila mafaniko cha ajabu leo tumeona ati CRDB wametoa mabasi bure tena kwa shirika ambalo ki historia lina utata hapo sijui tutegemee nini! hawa DCA tayari waliisha tangaza nia yao katika vyombo mbalimbali ili waungane na wadau na hamna hata mmoja aliyejitokeza achilia mbali wizara husika leo hii tumeona nini kimefanyika. Lejea mahojiano yao na kipindi cha JAMBO TBC 1 na Radio Uhuru cha lisaa zima na Kagaliuki jamani tunakwenda wapi? Na leo naona CRDB hao hao wanaomba waungwe mkono na nani sasa si waendelee tu kivyao na wadau wengine watengeneze mtandao mwingine ili kuwe basin a USHINDANI tuone itakuwaje. Vinginevyo Mradi huu upo tu HEWANI.
  Hamna neno tutaona ni nguvu ya soda na ya kuiga iga tu! ilibidi CRDB baada ya kupata WAZO la hawa watu wangelikaa nao na uona nini cha kuboresha siyo kukurupuka na kumwita kiongozi wa nchi kwa kushirikiana na wenye mamlaka kuu kufungua mradi huu! basi ni vema waendelee nao wenyewe si kuwaomba na wengine waingie hapo! sana sana kutakuwa na ubadilifu mkubwa wa pesa na uendeshaji kwa ujumla. ni picha kamili imejionyesha.


  Na hawa watu wa Chama cha madereva na makonda wamepeleka na WAZO LA MABASI MAREFU kwa ajili ya CITY BUSSES na wizara ya miundombinu SASA tutasikia tena UDA wanaleta hayo magari, jamani hivi sisi hadi tusikie furani kasema na anataka kufanya hili basi tufuatilie sisi SI WABUNIFU AIBU

  Poleni viongozi wetu!
   
 4. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #4
  Jun 9, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye bold...........muondoeni Lukuvi Dar kwanza....yeye ndio aliua yale ya wakati ule......hii ni kusaka kura za Dar au?
   
Loading...