Pinda ameshindwa kusimamia serikali kuhamia makao makuu -Dodoma

bwegebwege

JF-Expert Member
Jul 30, 2010
1,071
185
Miaka kadhaa iliyopita serikali ya CCM iliaamua kuhamishia Makao Makuu ya Serikali Kutoka DAR ES SALAAM na kuhamia DODOMA! Uamuzi huo ulifuatwa na hataua za utekelezaji, ikiwemo kujenga Ofisi za Bunge (mhimili mmoja wapo wa Serikali) na pia kuamuru baadhi ya Wizara kuhamishia shughuli zake mjini Dodoma.Kati ya ofsi nyeti zilizohamishiwa kule ni OFISI YA WAZIRI MKUU!!
PM, ambaye kwa sasa ni PINDA (sijawahi kumsikia akilizungumzia hili hata kidogo) alijengewa Nyumba ya kuishi pamoja na Ofisi. Serikali ya Awamu ya Tatu na hii ya Mh. J Kikwete ziliahidi kwamba zitahaklikisha Serikali inahamia DODOMA!!
Leo bado Waziri Mkuu yupo Oyster Bay, ofisi yake ipo pale Magogoni jirani na president! Kule Dodoma kuna Makazi na ofisi, na nina hakika kuna watendaji/watumishi wako kule na serikali inawalipa mshahara, posho, achilia mbali magari na kadhalika!! Naamini pia baadhi ya Wizara zina watendaji kule….
Swali: Kama tumeshindwa kwenda Dodoma, kuna haja gani serikali kupoteza fedha nyingi kuendesha hizi ofisi na makazi kule?? Kuna haja gani kwa PM kuwa na ofisi na makazi katika sehemu mbili tofauti wakati zaidi ya 90% ya muda wake anakuwa Dar es Salaam?? Serikali haioni kwamba mpango wa kuhamia Dodoma UMESHINDIKANA?
Siku za karibuni watu wengi wamechangia threads za ukosefu wa uwezo wa ndugu yetu PINDA. Leo nimelikumbuka hili, Nawasilisha na nitawashukuru wabunge wenye mapenzi ya kweli ya nchii hii kuishinikiza serikali kuamua kusuka ama kunyoa. KAMA TUNAKWENDA DODOMA BASI TWENDE MARA MOJA, KAMA HAIWEZEKANI BASI TUENDELEE KULA UPEPO WA PWANI DAR, LAKINI TUISELEKEZE HELA KULE DODOMA AMBAKO HATUNA MUDA NAPO, HUU NI UFUJAJI WA FEDHA ZA SERIKALI!!
 
Kaka pole sana najua unauchungu sana ila jibu ni HAIWEZEKANI serikari kuamia dom.kumbuka utawala wa mkapa uliahidi hivyo lakini wakajenga makao ya benki kuu dar,then kikwete akaja na propaganda mpaka kesho.chamsingi tujibu swali lifuatalo makao makuu ya tanzania yapo wapi?ukiuliza watu 100,kati ya hao 30 watajibu dom,30 watajibu dar then wengine 40 watajibu hawajui.nimefanya utafiti nawe jaribu,watu hawaelewi na serikali haielezi.
 
hiyo nayo ni moja ya challenge ambayo serikali inatakiwa ijiulize mara moja na kulitafutia suluhiso. Mambo hayo yanasababisha sisi wananchi kukosa imani na serikali juu ya mipango mbalimbali inayojinadi kuitekeleza.
 
Nilitegemea siku ile ya semina elekezi Kikwete angetangaza watawala wote wabaki dodoma kwani ndio makao makuu ya nchi. Tatizo viongozi wetu hawana uthubutu.maendeleo ni ndoto
 
Ameshindwa kila kitu si kuhamia dodoma tu..(mkuu hiyo ni jambo kubwa sana kwake) huyu jamaa ni "Incompetent, lazy, and harmless
 
Muache kumbebesha mzigo usiomstahili. Maamuzi ya kuhamia Dodoma yalifanywa mwaka 1972 na Nyerere alikaa miaka 13 lakini hakutekeleza mpango huu, ikaja 10 ya Mwinyi, hakuna kitu na baadae Mkapa na hata Kikwete, Pinda akiwa waziri mkuu wa pili. Hata huyo Lowassa anayesifiwa hakupata kuchukua hata hatua moja kutekeleza hilo, hata kuzungumzia hakuthubutu.

Katika kipindi hicho chote, nchi hii imeshuhudia mawaziri wakuu takribani 9 na hakuna aliyebebeshwa msalaba huu. Iweje leo Pinda asakamwe? Kujenga Chuo kikuuu kuna uhusiano gani? Si ni sawa tu na kujenga malambo ya maji kule Monduli? Pinda katika hili hana makosa, kama unamchukia mtafutie lingine.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom