Pinda ambeba Rostam Igunga

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,006
Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Igunga;
Tarehe: 21 February 2010
HabariLeo


WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amewataka wananchi wa Jimbo la Igunga mkoani Tabora kutomkataa mbunge wao Rostam Aziz wakati wa uchaguzi mkuu ujao kwa kusikia maneno yanayosemwa bungeni juu yake, badala yake wazingatie kile alichowafanyia akiwa mbunge.

Wakati Pinda anampigia debe mbunge huyo jana kwenye mkutano wa hadhara katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, baadhi ya wananchi wa jimbo hilo walimwomba Waziri Mkuu kumshinikiza mbunge wao kubaki jimboni humo, kwani amekuwa haonekani.

Wananchi hao walitoa ombi hilo ili waweze kupata fursa ya kumweleza kero zao na awaeleze yanayosemwa bungeni juu yake.

Mmoja wa wananchi aliyejitambulisha kwa jina la Moka Changalawe alimweleza Pinda kuwa kukosekana kwa mbunge jimboni kwa muda mrefu kumewafanya baadhi ya viongozi kuwanyanyasa wananchi kwa kuwabambikia kesi za uongo, zikiwemo kutishia kuua.

Hata hivyo, Pinda katika hotuba yake jana, alisema kama kuna manyanyaso na ubabe kwenye halmashauri hiyo, ni vitendo vya kuchochea rushwa na serikali imejipanga kuondoa tatizo hilo.

Hata hivyo hakujibu ombi la wananchi hao la kumwomba mbunge huyo kubaki jimboni humo. Pinda juzi mara baada ya kuwasili mjini hapa alizungumza na watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Igunga na kuwaomba kutomkataa mbunge huyo.

“Tunaelekea katika uchaguzi mkuu ujao baadaye mwaka huu. Naomba mtakapokuwa mnachagua viongozi wenu mzingatie wamewafanyia nini iwe ni katika nafasi ya udiwani au ubunge.

“Iwapo mnataka kumchagua tena Rostam zingatieni amewafanyia nini katika ubunge wake. Msisikilize kile kinachosemwa bungeni juu yake. Bunge lina mambo yake, mimi kama Waziri Mkuu nafahamu mambo ya pale bungeni,” alisema Waziri Mkuu.

Alisema iwapo wananchi wa Igunga wanaridhishwa na namna Mbunge wao anavyowatatulia matatizo yao ya kimsingi wana hiari ya kumchagua tena kuendelea kuwa Mbunge bila kusikiliza nini kinasemwa juu yake.

Ingawa Waziri Mkuu hakufafanua zaidi ni maneno gani ya bungeni ambayo yamekuwa yakisemwa juu ya mbunge huyo, Rostam ni miongoni mwa wabunge ambao wamekuwa wakihusishwa na kampuni ya Richmond iliyoingia mkataba tata na Shirika la Umeme (Tanesco).

Wakati wa kuhitimisha mjadala bungeni juu ya suala la Richmond katika mkutano wa 18 wa Bunge ulioahirishwa hivi karibuni mjini Dodoma, Spika Samuel Sitta alisema suala hilo limekwisha isipokuwa amebakiwa na kazi ya kumsihi Rostam aachane na mawazo ya kutaka liundwe jopo la majaji kuichunguza ripoti ya kamati teule iliyochunguza na kuwasilisha bungeni taarifa ya Richmond.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alionya tabia ya viongozi kujenga uhasama baina yao kwamba hatua hiyo inawafanya kutumia muda mwingi katika kugombana badala ya kuwatumikia Watanzania masikini.

Alisema serikali haitavumilia kuona viongozi wanatumia muda mwingi katika ugomvi wakati Watanzania wanakabiliwa na matatizo mbalimbali ukiwewo umasikini.

“ Kama kweli tunataka kuwahudumia wananchi masikini hawa ni lazima tuwe na ushirikiano sisi viongozi kwanza. Idadi yetu sisi Watanzania ni kama milioni 40 hivi au na zaidi kidogo. Hata hivyo asilimia 80 ni wakulima na asilimia 20 ndio sisi viongozi.

“Iwapo sisi asilimia 20 tutajali zaidi maslahi yetu na kuwasahau hawa masikini ipo siku hawa watu watatupiga marungu,” alisema Waziri Mkuu.

Alisema viongozi wa serikali wanawajibika kutumia fedha wanazozipata katika kuwasaidia masikini wanaowaongoza badala ya kujilimbikizia fedha huku wakizungukwa na watu masikini jambo ambalo ni hatari.
 
Inaelekea katumwa akaanze kazi ya kumsafisha jimboni, naona watapita wakuu wengi pale Igunga ili kumsafisha fisadi.
 
mambo ya kamati ya mzee mwinyi hayo!!!!!!!!!!!!!!

nchi ya kishikaji, hakuna utawala wa sheria............ tunarudi kulekule kwa mafisadi kuonekana mashujaa............................
 
Huyu mzee is more Idiot that I really thought!Msisikilize kile kinachosemwa bungeni juu yake. Bunge lina mambo yake, mimi kama Waziri Mkuu nafahamu mambo ya pale bungeni,” alisema Waziri Mkuu.
Kwa hiyo pale bungeni tunachezewa danadana tu!Nyambafu!
 
Huyu mzee is more Idiot that I really thought!Msisikilize kile kinachosemwa bungeni juu yake. Bunge lina mambo yake, mimi kama Waziri Mkuu nafahamu mambo ya pale bungeni," alisema Waziri Mkuu.
Kwa hiyo pale bungeni tunachezewa danadana tu!Nyambafu!

Ndiyo maana yake hiyo kwamba pale bungeni ni usanii tu. Sijui Pinda anamaanisha nini anaposema "Mimi kama WM nafahamu mambo ya pale Bungeni" Je, ni mambo gani hayo!? Watanzania wengi tungependa kuyafahamu.
 
Sunday Feb 21, 2010

02107t5hk1f.jpg


PRIME Minister Mizengo Pinda (left) gets some briefing from Igunga MP, Rostam Aziz today on the Mwamapuli pound which is used for irrigating farms in Igunga District Tabora Region, where the Premier is on official tour. (Photo by PMO)
 
'PRIME Minister Mizengo Pinda (left) gets some briefing from Igunga MP, Rostam Aziz today on the Mwamapuli pound which is used for irrigating farms in Igunga District Tabora Region, where the Premier is on official tour'. (Photo by PMO) Sasa hapa ni hatari yaani anatumia cheo cha uwaziri mkuu ambacho kinalipiwa kwa kwa kodi ya wananchi anakwenda kumpigia kampeni ya chama Mbunge,official tour kama waziri mkuu kwanini kaongelea mambo ya kumchagua mbunge?
__________________
~*~Life is Good~*~
 
Sunday Feb 21, 2010
02107t5hk1f.jpg


PRIME Minister Mizengo Pinda (left) gets some briefing from Igunga MP, Rostam Aziz today on the Mwamapuli pound which is used for irrigating farms in Igunga District Tabora Region, where the Premier is on official tour. (Photo by PMO)


Pinda dole lake alivyoliweka kikwetu ni tusi zito sana!!
 
Even if you wash with detergent and use a lot of soap, I would still see the stains from your wickedness," declares the Almighty LORD. (Jeremiah 2:22)
 
Huyu mzee is more Idiot that I really thought!Msisikilize kile kinachosemwa bungeni juu yake. Bunge lina mambo yake, mimi kama Waziri Mkuu nafahamu mambo ya pale bungeni," alisema Waziri Mkuu.
Kwa hiyo pale bungeni tunachezewa danadana tu!Nyambafu!

Bongo na communication style yetu bwana.

Hapa ilibidi Waziri Mkuu abanwe na kuulizwa ana maana gani kwa kusea "bunge lina mambo yake" ana maana bunge la Tanzania ni sehemu ya kupiga magirini na lisiaminiwe?
 
Katika hili tusimlaumu, alikwishaweka wazi tangu siku ya uteuzi wake kuwa ataendelea kuwa mwanafunzi mtiifu na mwaminifu kwa bosi wake wa zamani Lowasa. Nashangaa amekuwa anapewa sifa asizostahili mara mtoto wa mkulima, mara hajajilimbikizia mali, ...!
 
Rais ashasema kuwa huu ni 'mwaka wa SIASA',so expect the unexpected!
PM anataka kusema kuwa iwapo akatokea mbunge anakwapua mali za taifa kisha anatumia(iwe zote au sehemu yake) kwa ajili ya kutimiza ahadi zake jimboni then thats ok??Ooops,mi nilidhani alijifunza kitu pale alipowaamuru watu wajichukulie sheria mkononi juu ya wauaji wa albino kisha akabanwa na kuishia kulia?Then I was wrong kwani karudia yakufanana vilevile...
 
Kwa kweli tuna machaka ya viongozi, wanakera, wanaboa, wamekifu, wamechacha kila kona. kauli za kishenzi kama hizi za Pindo zilitolewa pia na Sumuye kule Moshi akiwataka wafanya biashara waibebe sisiemu ili biashara zao zibarikiwe na TRA. Hawa nyang'au wamebaini dhiki zetu za kutambua mambo wanafanya watakavyo. Ingekuwa pale UK au USA jioni ya leo maombi ya kumuomba ajiuzuru yangemtoa pale ofisini. MUNGU UTAIBARIKI LINI TANZANIA???????
 
Jamani tunahitaji kupambana na mapambano yaya yaanzae sasa, ufisadi utatumaliza na tuliowapa dhamana ya kutulinda wamejiengua. Mapinduzi Mapinduzi ya kifikra miongoni mwa watanzania ni muhimu. Nadhani ipo haja ya kuwaomba watanzania mwaka huu tuchague viongozi wetu kwa makini na waraka wa waislamu na wakatoriki tuzitafakari na kuzifanyia kazi kwa maslahi ya watanzania waluio wengi
 
Katika hili tusimlaumu, alikwishaweka wazi tangu siku ya uteuzi wake kuwa ataendelea kuwa mwanafunzi mtiifu na mwaminifu kwa bosi wake wa zamani Lowasa. Nashangaa amekuwa anapewa sifa asizostahili mara mtoto wa mkulima, mara hajajilimbikizia mali, ...!

Utimamu na ufikiri wa huyu ndugu PM ni wa kutia shaka kwa yote anayozungumza, nashangaa hata kuona msafara wake unasindikizwa na magari sio chini ya 20 yote hayo ya nini wewe mtoto wa mkulima? wa nii asikemee ufujaji wa matumizi mabaya? ni lazima nyuma ya pazia lake kuna uvundo wa kifisadi, mtua mweye akili zake timamu hawezi mpigia debe fisadi RA
 
Msisikilize kile kinachosemwa bungeni juu yake. Bunge lina mambo yake, mimi kama Waziri Mkuu nafahamu mambo ya pale bungeni," alisema Waziri Mkuu.

Hii ni dharau kwa bunge au nini? Inaelekea hana washauri wazuri maana mara nyingi huwa anatoa kauli tata! Au anatafuta sababu ya kutoa chozi bungeni tena?
 
Jamani haya mambo ni partisan politics sishangai au mlitaka mpasuko uendelezwe hata majimboni! Hahahah kha politics
 
Pinda ambeba Rostam Igunga
Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Igunga; Tarehe: 21st February 2010 @ 23:59
HabariLeo

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amewataka wananchi wa Jimbo la Igunga mkoani Tabora kutomkataa mbunge wao Rostam Aziz wakati wa uchaguzi mkuu ujao kwa kusikia maneno yanayosemwa bungeni juu yake, badala yake wazingatie kile alichowafanyia akiwa mbunge.

......., baadhi ya wananchi wa jimbo hilo walimwomba Waziri Mkuu kumshinikiza mbunge wao kubaki jimboni humo, kwani amekuwa haonekani.

.......Msisikilize kile kinachosemwa bungeni juu yake. Bunge lina mambo yake, mimi kama Waziri Mkuu nafahamu mambo ya pale bungeni," alisema Waziri Mkuu.


.


Inasikitisha na kuchefua sana. Hii ni uthibitisho kuwa hata Pinda hajui maana na umuhimu wa Bunge?

Kwa jinsi Igunga mjini palivyo, ukilinganisha eti utajiri wa RA....mhhhhhhhh!!!!!!
Bora awe mbunge wa Ikulu, wa kuteuliwa na jamaa yake na si mwakilishi direct wa watu.
 
Back
Top Bottom