Pinda alisema "WAPIGWE TU MAANA TUMECHOKA" Kwanini hajajiuzulu?? Hatujasahau

Mtanke

JF-Expert Member
Nov 19, 2011
327
500
Wakati Operesheni Kimbunga, Mikutano ya Kampeni za Kata 26, na Tokomeza zikiendelea na Wananchi kuanza kulalamika pamoja na Wanaharakati Pinda akiwa ndani ya Bunge mbele ya Wabunge wote alitoa maneno ya dharau na kutokuthamini uhai na utu wa Mtanzania na kesi iko Mahakamani.

Pinda huyu huyu alisema Liwalo na Liwe kuhusu Dr. Ulimboka na aliteswa usiku wake kiasi cha kutaka kuuawa ila Mungu akamuokoa. Nchimbi na Kova wakatuletea Joshua Mulundi Mkenya na kesi imeisha kienyeji enyeji tu.

Pinda huyu huyu wakati wa Bomu la Soweto hakuonyesha kujali zaidi ya kuendelea na kikao cha Bunge kama kawaida na mwisho wake jeshi lilikuja kuharibu mali za vijana pale arusha pamoja na kuwaweka rumande wabunge wa Upinzani.

Kwanini Pinda hajajiuzulu?? Anafikiri tumesahau?? Damu hizo zitaendelea kuililia Serikali yake na hataongoza kwa amani ang'oke na yeye asijifanye anataka huruma za Watanzania asiowajali hata kidogo. Utawala wa Damu kama lilivyosema gazeti la Mtanzania na likafungiwa
 

fikirikwanza

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
7,448
2,000
Kamuuliza rais juu ya mawaziri 4, kuhusu yeye hajauliza. JK may be smart akirudi anavunja baraza lote maana hata wale mizigo bado hawajaguswa, ardhi inaua watu Tibaijuka anasema wizara inaendeshwa kama alivyoikuta, hakuna sera wala mipango ya kusukuma kila MTz apate kiwanja/ardhi
 

Inkoskaz

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
6,364
2,000
Pinda amepinda alihitaji anyooshww kwa kuwajibishwa
Yanyotekea na kiburi cha vyombo vya usalama ni matokeo ya kauli yake kuwa MIMI NAONA WAPIGWE TU!
 

Mike Scofield

Senior Member
Dec 10, 2013
137
0
Kwa sababu hujajua tu 'calculations' za mkulu. Pinda yuko kilengeoni. Vumbi la akina Nchimbi likishatua tu, yeye atashughulikiwa kinamna. We vuta subira tu!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom