Pinda alifaa kuwa Waziri wa Mashambani na Si Waziri Mkuu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda alifaa kuwa Waziri wa Mashambani na Si Waziri Mkuu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by spencer, Dec 31, 2010.

 1. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2010
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  GrEatThinkers,

  Nilitegemea waziri mkuu awe ndiyo kinara wa kukomaa na mawaziri wake.

  Staili ya huruma huruma,Chozi chozi ya Mtoto wa Mkulima kinyume chake inatuCost,

  Tanzania ya leo haikustahili iwe ya kuchekeana hivyo.Ilifaa waziri Mkuu aggressive.

  Namuona anaStaki Nataka Nyiiingi, ambazo zinanipa jibu kuwa hajiamini.

  Kauli yake juu ya Mahakama ya Kadhi "Mguu nje,Mguu ndani"

  Kauli yake juu ya katiba "Nitamshauri Rais akiona inafaa...."

  Kauli yake juu ya Dowans "Ikibidi kuilipa Dowans tutailipa"

  Yeye ndiye aliyeuvunja mkataba wa Dowans, tena si muda mrefu wote tunajua.

  Alitumia vigezo gani-sasa mbona leo wanasheria hao hao kina Mzee Six anawabeza.

  Ingawa hayuko kama yule Mtalii anayetafuta riziki kwa safari,Uzalendo anao lakini hauna meno.

  Hafai kuwa waziri Mkuu wa Tanzania ya Leo. Alifaa kuwa waziri wa mashambani afundishe Power Tiller.

  :A S-coffee:Mimi yangu ni hayo:A S-coffee:
   
 2. Hmaster

  Hmaster JF-Expert Member

  #2
  Dec 31, 2010
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 347
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hata mimi kwa kweli huwa ninishangaa sana. Mara kalia bungeni, mara kakataa shangingi huku anakubali litumike na mtumishi mwingine. Mi naona kuna haja ya kubadili katiba ili tuwe na PM mwenye meno kama R. Odinga wa Kenya!
   
 3. Keynes

  Keynes JF-Expert Member

  #3
  Dec 31, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 499
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Huyu mzee ni clean lakini ananipa mashaka sana.. upole umezidi!!
  Yeye kazi yake ni kujitetea kila siku tuu kuwa yeye ni mtoto wa mkulima....Najiuliza anadhani kazi ya uwaziri mkuu ni kujitetea kua huna mali??
  Kwa kweli kwa hali ilivyo tanzania kwa sasa tunahitaji waziri mkuu ambaye ni more than mjeshi. Waziri mkuu pamoja na kumshauri rais lakini anatakiwa awe na msimamo mkali kuhusu mambo anayomshauri rais na si kuwa lege lege tu kisa rais alikupendekeza!!
  Kumbuka umependekezwa na rais lakini unatumia kodi zetu na upo kwa ajili ya kusimamia maslahi yetu
   
 4. semango

  semango JF-Expert Member

  #4
  Dec 31, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  hana u-clean wowote huyu.angekua clean angepambana na ufisadi hata kwa maneno tu.hii dowans ni ufisadi na umetendeka chini yake na yeye kabaki kuvaa gumboots tu kwenda kulima shambani kwake badala ya kupambana mpaka kieleweke kwa maslai ya nchi.me namuona mchafu tu kama wengine tena yeye ni mchafu zaidi maana anatudanganya ni mtoto wa mkulima ili tumuonee huruma.unajua jambazi sio mpaka aue mtu.hata yule anaesaidia kupanga tukio la ujambazi ni jambazi vile vile
   
 5. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #5
  Aug 18, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  GreaThinkers,
  Ushauri wangu kwa Pinda bora ajistaafishe hana kazi anayofanya.
   
 6. M

  Mjenda Chilo JF-Expert Member

  #6
  Aug 18, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 1,425
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 145
  Mambo ya kusikiliza kwenye vijiwe bora Pinda ndo hayo kateuliwa anachofanya? ila kwao naona watamkumbuka yuko busy na mkoa wa Rukwa, mara barabara, mara Agrisol nk. Mi kwangu kama akiondoka leo nitamkumbuka jinsi nilivyomuona mtu mzima anamwaga uchozi mjengoni
   
 7. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #7
  Aug 18, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Huyu jamaa ni bure kabisa hamna anachofanya tunamkumbuka sana Lowasa mzee wa ekshen!!
   
 8. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #8
  Feb 6, 2012
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lini Pinda ataachwa kudhalilishwa?

  Josephat Isango


  NAOMBA niwakumbushe Watanzania wenzangu maneno yaliyomo katika Azimio la Arusha, naamini maneno haya bado yana maana kubwa sana katika kumkomboa mwananchi.

  “Tumeonewa kiasi cha kutosha, tumenyonywa kiasi cha kutosha na tumepuuzwa kiasi cha kutosha, unyonge wetu ndio uliotufanya tuonewe, tunyonywe na kupuuzwa. Sasa tunataka mapinduzi; mapinduzi ya kuondoa unyonge, ili tusionewe tena, tusinyonywe tena.”
  Mimi naongeza maneno tusidharauliwe tena kama Pinda anavyodharauliwa na Rais Jakaya Kikwete.

  Leo ningependa kuangalia kauli za kukinzana, kudharauliana na kusutana zilizotolewa na viongozi wakuu wa Bunge na serikali ambapo kwa nyakati tofauti kila mmoja kasema lake.
  Spika wa Bunge, Anne Makinda aliuambia umma kuwa posho ya wabunge imepanda kutoka sh 70,000 hadi sh 200,000 ambazo atazipata iwapo atakuwa amehudhuria kikao cha siku husika (asubuhi na jioni).
  Kwa mujibu wa kiongozi huyo nyongeza hiyo ilipata baraka za Rais Jakaya Kikwete lakini cha ajabu Ikulu imepinga jambo hilo kwa madai kuwa rais hajamwaga wino kuliruhusu.
  Mimi kifalsafa sitaki tujiulize sana kuhusu wanaopata na wanaokosa. Je, uhalali wa kupandisha posho kutoka sh 70,000 hadi sh 200,000 ulitoka wapi? Kwanini haukufuata utaratibu unaotakiwa?
  Hivi sasa kila mbunge atakuwa akilipwa sh 80,000 kama posho ya kujikimu (per diem) anapokuwa nje ya jimbo lake, posho ya vikao (sitting allowance) sh 200,000 na mafuta ya gari sh 50,000 kila siku. Kwa siku mbunge atajikusanyia sh 330,000.
  Fedha hizi ni nyingi na waliozipandisha hawakuangalia maslahi ya wananchi walio wengi, walitawaliwa na ubinafsi pamoja na ulevi wa madaraka.
  Ikumbukwe kuwa kimsingi kwa mujibu wa masharti ya kazi za Bunge, anayepandisha posho za wabunge ni rais. Wala si spika, naibu spika au Katibu wa Bunge. Katika muktadha huu aliyezipandisha ni Rais Kikwete, kwanini tunamkwepa?
  Yeye ndiye aliyepaswa kutumia busara si wabunge. Aliyetakiwa kuzungumza ni kwanini posho zimepanda kutoka sh 70,000 hadi 200,000 ni Ikulu, wala si sika na ktibu wake. Viongozi wa Bnge wametwikwa mzigo usiowahusu.
  Spika na katibu wa Bunge wametuelekeza kusiko na sisi tumekubali kuwafuata bila kufikiria, tunaelekeza hasira zetu katika eneo lisilohusika.

  Wananchi walipaswa kukasirishwa na uamuzi wa rais wa kupandisha posho za wabunge kinyemela, maana ndiye anayeruhusu kupanda. Ikulu ilipaswa kulisemea hili maana ndiyo msemaji halali wa jambo hili.
  Ofisi ya Bunge ilizungumzia hili ili kumuondoa rais dhidi ya hasira za wananchi, kwa bahati mbaya mpango wao huo haujaweza kufanikiwa kwa kiwango kinachotakiwa ndiyo maana baadhi yetu tunaendelea kusisitiza kuwa aliyeruhusu nyongeza hizo ni rais.
  Ni kweli posho zilipanda kama alivyosema Spika wa Bunge. Zilipanda vipi ameeleza Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuwa aliyetoa Baraka ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kumbukeni kuwa waziri mkuu ni mteule wa rais, anayesema yale aliyotumwa na rais.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ndiye aliyesema kuwa nyongeza hiyo haikwepeki, nani anaweza kuhadaiwa kuwa waziri mkuu hamjui Rais Kikwete? Ikulu inataka kumfanya Pinda aonekane hamjui ‘bosi’ wake ambaye ndiye aliyelipendekeza jina lake baada ya Lowassa kujiuzulu mwaka 2008,.
  Ina maana Pinda anaweza kukosea kutaja jina la Kikwete katika suala la posho? Katika mazingira ya sasa kuna kila sababu kwa kiongozi mkuu wa nchi kuwa muungwana na kuomba radhi kwa kumdhalilisha Makinda, Pinda na wengineo waliokwazwa na msimamo huo.
  Kuna mambo mengi rais alituahidi lakini mpaka sasa hayajatekelezwa, aliwaambia wanafunzi wa vyuo vikuu kuwa hakuna atakayefukuzwa chuo kwa kukosa ada, wakatimuliwa na skari kwa marungu, mpaka sasa migomo inazuka kila kukicha.
  Aliwaahidi Waislamu atawapatia Mahakama ya Kadhi lakini mwisho wa siku kila mmoja anajua kilichotokea, serikali iliwaahidi askari kuwapandishia posho mpaka sasa imekuwa ni ndoto ya kusadikika na anayeulizwa huishia lokapu.
  Kwenye sakata la uchotaji wa mamilioni ya fedha katika Wizara ya Nishati na Madini, waziri mkuu alidhalilishwa sana. Pinda angekuwa kiongozi makini nina uhakika mpaka sasa asingeendelea na cheo hicho.
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, aliyetuhumiwa kuchangisha fedha kutoka katika idara mbalimbali zilizo chini ya wizara hiyo Julai 21, mwaka jana, Ikulu ilitangaza hatua ya kumpa likizo ya malipo katibu huyo ili kupisha uchunguzi ambao Kikwete alikuwa ameagiza ufanyike kufuatia tuhuma zilizokuwa zimeelekezwa dhidi yake.
  Katika kikao cha 18 Julai 2011, baadhi ya wabunge wakati wa mjadala kuhusu makadirio na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka 2011/12 walidai katibu mkuu huyo aliandika barua akitaka idara zilizo chini ya wizara hiyo kuchangia sh milioni 50 kila moja.
  Katika mjadala huo, wabunge walihoji uhalali wa wizara kuomba michango ya fedha kutoka kwenye taasisi zilizoko chini ya usimamizi wake ili kusaidia kupitisha kwa urahisi bajeti ya wizara hiyo.

  Waziri Mkuu, Mizengo Peter Pinda alikasirishwa sana na hatua hiyo ya Jairo akasema angekuwa na mamlaka angemfukuza kazi katibu huyo. Kwa maana nyingine Pinda alikiri kuwa Jairo anastahili adhabu.
  Wakati kashfa hiyo inaibuliwa bungeni Rais Kikwete alikuwa njiani akielekea Afrika Kusini. Siwezi kusadiki kuwa Pinda hakuwa na salio la kutosha katika simu yake ambalo lingemfanya ashindwe kumweleza vema rais sakata la Jairo. Pia sitaki kuamini kuwa Pinda hajui utaratibu unaotumika katika kupitisha bajeti.
  Pinda alijua sana ndiyo maana alisikitishwa na kitendo cha Jairo kuchangisha fedha. Hivyo ninaamini kuwa Pinda alitoa maelezo ya kutosha na rais akajiridhisha ndipo akatoa hukumu hiyo – likizo ya malipo.
  Katikati ya shauku kuu ya wananchi kutaka kujua mwisho wa sakata hilo aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo akasikika akisema ukaguzi maalumu haukuthibitisha kuwapo usahihi wa tuhuma zilizotolewa dhidi ya Jairo. Akaamua Jairo arejee kazini Agosti 24, 2011.
  Siku moja baada ya shangwe za mapokezi wizarani Ikulu iliyoamuru arudi kazini ndiyo ikaamuru arudi likizo baada ya moto kulipuka bungeni.
  Luhanjo na Pinda si wote walikuwa wanasubiri kauli ya rais? Ilikuwaje rais alimweka kando Pinda halafu akamtaka Luhanjo amrudishe Jairo? Ilikuwaje alimgeukia Pinda na kuamuru Jairo aendelee ili waziri huyo mkuu asifikie uamuzi mgumu?
  Utendaji kazi huu ni hatari ndiyo maana nasema kuwa uamuzi wa kwanza ulikuwa wa rais, wa pili, wa tatu na wa nne ulikuwa wa rais. Ilikuwaje akawa na maamuzi tofauti bila kuwa na muunganiko? Inatia shaka. Kikwete umemdhalilisha Pinda Kiasi cha kutosha, lakini pia ni dharau kwa Watanzania. Kikwete katika hili unatuchefua Watanzania.
  Na Sasa suala la Posho umeendelea kumfanya waziri mkuu kama mdoli. Hivi ni kweli Pinda alimsingizia Rais Kikwete kuwa alimpa jadala la nyongeza za posho za wabunge ili alifanyie uamuzi? Kama alimsingizia mbona hajachukuliwa hatua yoyote?
  Je, alilazimishwa? Pinda anawezaje kufanya kitu ambacho hujamtuma? Katika kikao hicho Dodoma baada ya taarifa ya waziri mkuu kuwa umebariki posho baadhi ya wabunge wanadaiwa kuwashambulia Zitto, Mbunge wa Bumbuli (CCM), Januari Makamba na Mbunge wa Nzega (CCM), Dk. Khamis Kigwangwalah kwamba wamekuwa mstari wa mbele kupinga posho hizo hadharani.
  Spika wa Bunge, Anne Makinda, aliungana na Pinda kuthibitisha kwamba Rais Kikwete ameidhinisha posho hizo mpya, pia aliwashambulia wabunge wanaozipinga akisema kwamba wanatafuta umaarufu wa kisiasa.
  Sasa Kikwete, kama Pinda na Makinda wamekusingizia mbona huwachukulii hatua? Au ndio utawala wa ‘uswahiba’ wa kusameheana kama ulivyosamehe wezi wa EPA?

  Rais Kikwete ukimya wako na matamshi tata yamesababisha fujo hadi bungeni, wabunge wanajengeana chuki kwa sababu ya kukosekana kwa msimamo wako. Wabunge wanadharauliana kwa sababu ya msimamo wako usiotabirika. Wabunge wanakashifiana eti wanaopinga posho wanatafuta umaarufu wa kisiasa kwa sababu ya misimamo yako ya kisirisiri. Kwanini?
  Kutokuwa na uamuzi unaoeleweka umesababisha Pinda kutoheshimika sasa nchini, ndiyo maana Pinda aliamuru sukari iuzwe sh 1700, watu wakauza sh 2,300 hadi sh 2,500, Pinda aliamuru madaktari warejee kazini la sivyo watakuwa wamejifukuzisha kazi, mpaka leo hii wataalamu hao wamegoma na hakuna kilichotendeka.
  Rais Kikwete unaaswa kufanya tafakuri kuwa unatuachia funzo gani sisi vijana, si jambo jema kwa kiongozi kutokuwa na msimamo unaoeleweka katika masuala ya msingi kwa taifa.
  Ni lazima kila jambo liwe zito au jepsi libebwe na kiongozi mkuu wa nchi, visitafutwe visingizio kama tunavyovisikia hivi sasa, huku ni kuwachanganya Watanzania wasijue la kufanya.
  Kuna mambo mengi ambayo uamuzi wa rais unapaswa kuwa hapana au ndiyo, kuwa moto ama baridi. Lakini rais wetu amekuwa akitoa majibu mengi sana kwa suala moja. Inafikia Watanzania wanashindwa kuelewa washike lipi na waache lipi.
  Sikubaliani na hoja eti wakati fulani Rais Kikwete huwa anatutania Watanzania. Isitoshe kama kweli huwa anatania, basi anakosea kwasababu utani wake umekuwa ukisababisha madhara makubwa kwa wananchi ambao kila kukicha maisha yanazidi kuwa magumu.
  Sitaki kuamini kuwa Mizengo Pinda si rafiki wa karibu wa Rais Kikwete. Sitaki na sipendi kuamini kuwa Mizengo Pinda huwa anapungukiwa salio katika simu wakati wa kuongea na rais, hivyo huchukua maelezo nusu au mengine hutunga mwenyewe.
  Sitaki kuamini kuwa Mizengo Pinda hatekelezi yale anayotumwa na rais. Na kama hatekelezi basi hafai na kama hafai kwanini Kikwete anamwacha pale? Ninaamini kabisa Mizengo anamjua Kikwete, anatekeleza yale anayoambiwa.
  Binafsi naamini kuwa upinganaji wa kauli ni ujasiri wa Rais Kikwete kupenda kumdhalilisha Pinda ambaye ndiye kiongozi mkuu wa shughuli za serikali pale bungeni ambapo sasa mambo si shwari tena.
  Tumefika pabaya nchi yetu inaendeshwa vibaya, lakini hata tunaposema Rais Kikwete na watendaji wake wanatuona ni wapinzani, tusiomtakia mema. Nchi hii ni yetu sote tunachokisema kina lenga kutukwamua kutoka hapa tulipo.
   
 9. Mbimbinho

  Mbimbinho JF-Expert Member

  #9
  Feb 6, 2012
  Joined: Aug 1, 2009
  Messages: 6,027
  Likes Received: 2,867
  Trophy Points: 280
  Ni siku yeye mwenyewe atakapoacha kujidhalilisha mwenyewe. Waziri mkuu gani laini kama utumbo? ndo maana kila anachotamka mkulu wake anampa nakoz.
   
 10. BINARY NO

  BINARY NO JF-Expert Member

  #10
  Feb 6, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,778
  Likes Received: 588
  Trophy Points: 280
  Akijiheshimu ata heshimika........akicha kujilizaliza ovyoovyo hatalizwa ovyoovyo
   
 11. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #11
  Feb 6, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Kikwete hamthamini Pinda na ndio maana anamdhalilisha!! Pinda angekuwa mtu mwenye msimamo angekwisha jiuzuru wakati wa sakata la Jairo!! Huyu mkweree ataendelea kumshushua mpaka hapo atakapopata akili.
   
 12. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #12
  Feb 6, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Nadhani mnamsingizi kikwete, Pinda ni dhalili tu, mwakumbuka amri yake kuwataka waganga wa jadi kuondoa mabango ya matangazo yao ya biashara, nani alitii, inawezekana kwenye mgomo wa madaktari yule prof. kutoka tanga alimhakikishia kuwatibu kwa ufanisi wagonjwa wote pale muhimbili, ameaibika, amedhalilika ile mbaya!!!!!!!
   
 13. BONGE BONGE

  BONGE BONGE JF-Expert Member

  #13
  Feb 6, 2012
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 3,398
  Likes Received: 1,523
  Trophy Points: 280
  ..........du, hili ndilo jibu sahihi, ni kama kumjua mbwa jina, wala hakupi shida......teh teh teh
   
 14. spencer

  spencer JF-Expert Member

  #14
  Feb 7, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 2,792
  Likes Received: 1,337
  Trophy Points: 280
  Ameropka vibaya kwa madaktari.
  Sasa uongozi mzima kuisoma namba.
  Nchi nzima kugoma
   
 15. F

  FUSO JF-Expert Member

  #15
  Feb 7, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,860
  Likes Received: 2,338
  Trophy Points: 280
  amechelewa alitakiwa aachie ngazi ile issue ya kina jairo; yes kwa sasa anaonekana ni kiongozi dhaifu kuliko wote waliokwisha pita kwenye post hiyo.
   
 16. F

  FUSO JF-Expert Member

  #16
  Feb 7, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,860
  Likes Received: 2,338
  Trophy Points: 280
   
 17. p

  papito Member

  #17
  Feb 7, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Angekuwa mkuu wa idara ya MAADHIMISHO

  Ni :hurt: mwanzo mwisho!!
   
 18. King2

  King2 JF-Expert Member

  #18
  Feb 7, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 1,289
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa, na Jk alitakiwa kuwa mkuu wa shule na si mkuu wa nchi.
   
 19. Higash

  Higash JF-Expert Member

  #19
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  ni waziri mkuu dhaifu, asiye na msimamo huyu kweli anafaa kuwa kiongoz wa mashamba kule mbarali.
   
 20. AK-47

  AK-47 JF-Expert Member

  #20
  Feb 7, 2012
  Joined: Nov 12, 2009
  Messages: 1,381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  PM wetu angefaa sana kuwa muhudumu wa mortuary ili alie vizuri hadi atosheke.
   
Loading...