Pinda ali shinda bahati nasibu ya kisiasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda ali shinda bahati nasibu ya kisiasa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaFalsafa1, Jun 6, 2009.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Ukiangalia kwenye siasa kuna wale ambao wanaonekana wazi kuwa na malengo ya kuja kupata nyadhifa fulani. Uki chukulia mfano wa raisi wetu wa sasa. JK baada ya kushindwa kuukwa ugombea wa CCM kwa mwaka 1995 alionyesha dhahiri nia yake ya kuja kugombea tena. Hatma hiyo ili timia 2005 ambapo safari hii ali pitishwa na CCM na kushinda uchaguzi mkuu.

  Kwa upande mwingine kuna wale ambao bahati ina wakuta na kuji kuta wana pata nafasi ambazo labda hawa kuwa wakizi myemelea au kuzi tafuta. Mfano mmoja wapo hapa inaelekea kuwa waziri mkuu Pinda. Pinda alikuwa mtumishi wa umma kabla ya kuji bwaga kwenye siasa na hatumae 2007 kupewa uwaziri mkuu. Maswali ninayo jiuliza na je Pinda alikua na ndoto ya kuja kushika wadhifa mkubwa kama huo au alikua ame tosheka na ubunge? Je Lowasa asinge anguka ange kuja kushika nafasi ya juu kama hiyo? Je alikuwa chaguo la kwanza la JK kumridhi Lowasa au ali chaguliwa ili kuridhisha pande zote? Katika mjadala wa kumrithi Lowasa ni majina gani yaliji tokeza na Pinda alikua na nafasi gani ya kushinda? Political capital na ushawishi wa Pinda ndani ya CCM ulikuaje kabla ya kuteuliwa kuwa waziri mkuu?

  Kwa mujibu wa maswali hapo juu na kwa ninavyo fahamu mimi(kumbuka haya ni maoni yangu kama kuna ana ona vingine ruhusa kusema) ni kwamba mheshimiwa Pinda ali pata kwa msemo wa mitaani "zali la mentali". Hakuwa mtu anaye tarajia kuja kuwa kiongozi wa juu. Hakua chagua la kwanza la JK kumrithi Lowasa bali alimpa asionekani kupendelea wanamtandao. Jk alimpa kwa kuwa Pinda hakuwa na skendo za huku nyuma zinazo weza kuja kuleta matatizo baadae. JK alimpa Pinda uwaziri mkuu kwa kuwa alijua Pinda siyo tishiyo kwa mamlaka yake kutokana na ushawishi mdogo na kukosa nguvu kubwa ndani ya chama.

  Baada ya hapa pia najiuliza je kama nafasi hiyo ali pata kibahati ana mpango wa kui tumia hiyo bahati na kutafuta nafasi ya juu zaidi? Ana nguvu gani sasa ndani ya CCM na serikali au ni kiongozi wa mpito tu? Ana nafasi gani ya kushangaza wengi na kuja kuukwa uraisi baadae? Pinda ana ushawishi gani sasa ndani ya CCM?

  Kwa kifupi haya ni maoni yangu tu na ni jinsi ninavyo ona mambo. Maswali ninayo jiuliza hapo juu ndiyo naya tafutia majibu. Kuna sehemu nime jijibu kutokana na ninavyo ona lakini ina wezekana nime kosea. Je kuna mwenye kujua majibu ya maswali haya JF? Je kuna mwenye maoni tofauti?
   
Loading...