Pinda akunwa miradi ya kimkakati

elivina shambuni

JF-Expert Member
May 31, 2018
461
295
1571910487309.png


WAZIRI Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, amekunwa na miradi ya kimkakati inayotekelezwa na serikali, ikiwamo uboreshaji usafi ri wa anga, huku akishangazwa na watu waliobeza uamuzi wa Rais John Magufuli kununua ndege.

Pinda ambaye amesema binadamu anapotenda mambo mema asitegemee watu wote kumpongeza, alisema zilipotolewa kauli za kuponda, alijisemea moyoni kwamba, wanaobeza watapata majibu polepole na sasa wameshayapata.

Alisema hayo mjini hapa wakati akifunga Maonesho ya Viwanda ya Mkoa wa Pwani katika hotuba ambayo pia alitoa rai kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuangalia uwezekano wa kutoa elimu inayoendana na mahitaji ya soko la ajira na kuishauri serikali kuhusu viwanda vinavyojengwa na kufa akitaka ivifuatilie.

Akizungumzia miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali ya awamu ya tano, alisema ina uhusiano mkubwa na uboreshaji wa maisha ya wananchi. “Jambo jingine ambalo serikali ya awamu ya tano imefanya ni kuboresha Shirika la Ndege la ATCL, mambo haya na mengine ndiyo maana tunakubali.

Mtu unapotenda mambo mema mazuri usitegemee tu kwamba watu watakunyamazai tu, hongera, asante sana.” “Maana nakumbuka bwana mkubwa (Rais) alipofanya uamuzi huu, ulileta mjadala mkali sana.

Nakumbuka siku za mwanzo watu walisema ndege yenyewe haina hata watu. Yanaruka tu matupu tu. Nikajua tu watakuja kupata majibu polepole.” “Ilikuwa inakwenda mara moja sehemu nyingine, sasa tunakwenda mara mbili na bado tutalazimika hata kwenda mara tatu, usafiri nao una mchango mkubwa sana katika maendeleo ya nchi,” alisema.

Pinda alisema kwa kutumia ndege hizo, sasa mfanyabiashara anaweza kutoka Dodoma kwa dakika 50 mpaka Dar es Salaam na kisha akageuza kurudi jambo ambalo lilitakiwa kuwapo tangu awali. “Hivyo lazima tukubali kuwa hii ni miradi ya kimkakati kikwelikweli wala siyo lele mama hata kidogo,” alisema.

Akieleza mchango wa usafiri katika uchumi, alitoa mfano wa Wachina akisema wanapenda kuja nchini kutalii lakini wamekuwa wakihoji kuhusu uwapo wa ndege ya moja kwa moja kutoka nchini kwao. “Sasa nashukuru madege yameingia makubwa na mpango utakapokamilika yataruka kwenda Guangzhou (China) pale utaona sasa Wachina watakavyokuwa wakija kwa wingi kutalii,” alisema.

Pinda pia alitaja Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Nyerere katika Mto Rufiji na kusema ulikuwa na hadithi ndefu na kila aliyejaribu kuutekeleza alirudi nyuma hadi Rais Magufuli alipoingia madarakani. Alisema miongoni mwa sababu zilizotolewa kuhusu kutotekelezwa mradi huo ni gharama na uharibifu wa mazingira.

Akimpongeza Rais Magufuli kwa uamuzi mgumu aliofanya, kwani mradi huo ukikamilika viwanda vitakuwa na uhakika wa umeme. Akizungumzia ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), alisema mradi huo ukikamilika utatoa mchango mkubwa katika ujenzi wa viwanda, kwani utatoa fursa ya kusafirisha malighafi na bidhaa zinazozalishwa.



===
Chanzo: Habari Leo
 
Waliokaa kwenye uongozi wakaona yaliyokuwa yanaendelea wanaelewa nini wanachokisema
 
Back
Top Bottom