Pinda akiri kuzomewa Mwanza, afunguka wananchi kusahauliwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda akiri kuzomewa Mwanza, afunguka wananchi kusahauliwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Sep 20, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Sep 20, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Waziri Mkuu Pinda akiwa katika moja ya ziara za kimataifa
  akikagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake

  Pinda aeleza alivyozomewa Mwanza
  SIKU moja baada ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuzomewa kwenye mkutano wa hadhara jijini Mwanza kisha msafara wake kupopolewa mawe, kiongozi huyo amesema kitendo hicho kimemtisha na kusema upo uwezekano mkubwa wa viongozi wengine wa kitaifa kuanza kukumbana na hali hiyo. Alisema hii ni mara yake ya kwanza kukumbana na zomeazomea, hivyo lazima kero zinazowasibu wananchi zitatuliwe kwani hali hiyo siyo nzuri kutokea kwa kiongozi wa taifa kama yeye.

  Pinda aliyasema hayo jana wakati alipokuwa akizungumza kwenye kikao cha majumuisho ya ziara yake ya siku saba mkoani Mwanza, kilichofanyika kwenye ukumbi wa jiji la Mwanza. “Kwa kweli hali ya jana (juzi), ilinitisha sana. Kama mimi nimezomewa, kiongozi gani atakayesalimika kuzomewa akienda uwanjani hapo? “Wakati hali hiyo ikitokea, mbunge wa Jimbo la Nyamagana, jijini Mwanza, Ezekiel Wenje, aliniambia sababu hiyo ni kutokana na vijana kuchukizwa na mienendo ya baadhi ya viongozi wa CCM. “Na akaniambia Wenje kwamba tangu umalizike uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, CCM haijafanya mkutano eneo hilo kuzungumzia kero za wananchi… sasa hii ni hatari sana,” alisema Pinda huku akionekana kusononeshwa na hali hiyo.


  Juzi, Pinda alishindwa kuendelea kuhutubia mkutano wake wa hadhara kwa muda, katika viwanja vya Sahara jijini Mwanza baada ya kuzomewa wakati akitaka kuhutubia. Mbali ya kuzomewa kwa kiongozi huyo, maarufu kwa jina la ‘Mtoto wa Mkulima’, baadhi ya magari yaliyokuwa kwenye msafara wake yalipondwa mawe kwenye uwanja huo wa Sahara wakati msafara wake ukiondoka, jambo lililosababisha taharuki kubwa.

  Hiyo ni mara ya kwanza kwa kiongozi wa kitaifa kama Pinda kuzomewa hadharani mkoani Mwanza na hali hiyo ilionekana pia kumtisha mkuu wa mkoa huo, Evarist Welle Ndikilo, na kamati yote ya ulinzi na usalama ya mkoa.

  Meli za mafuta za Irani Kupeperusha bendera ya Tanzania
  Akijibu swali la mwandishi wa habari hizi, aliyetaka kujua hatua zilizochukuliwa na serikali kuhusiana na tuhuma ya meli za Iran kutumia bendera ya Tanzania kusafirisha mafuta baharini kinyume na sheria, Pinda alikiri kuwepo kwa hali hiyo. Alisema utata huo umeilazimisha serikali kuzifutia usajili meli hizo zilizosajiliwa visiwani Zanzibar, ikiwa ni pamoja na kumchukulia hatua ya kumsimamisha kazi aliyekuwa wakala wa meli wa Zanzibar, huko Dubai. “Ni kweli hili tatizo lilijitokeza kwa meli za Iran kutumia bendera yetu. Lakini tulifanya uchunguzi na tukabaini kuwepo kwa udanganyifu mkubwa kupitia kwa wakala wa meli wa Zanzibar aliyeko huko Dubai. “Baada ya kubaini haya, serikali iliamua kumsimamisha kazi wakala huyo na baadaye kuzifutia usajili meli za Iran,” alibainisha Waziri Pinda wakati akijibu swali hilo.


  Mgongano wa mawaziri Mwakiembe na Hamad Masoud
  Alipotakiwa kufafanua mgongano wa taarifa ya meli hizo zilizotolewa na Waziri wa Uchukuzi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Harrison Mwakyembe, na Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hamad Masoud, Waziri Mkuu Pinda alisema hatua hiyo ilitokana na kuwepo kwa mkanganyiko wa taarifa husika. “Wala si kwamba walitofautiana, hapa kulikuwa na mkanganyiko tu wa taarifa kuhusiana na usajili wa meli hizi. Maana huyu wakala wa meli Zanzibar aliyeko Dubai alifanya udanganyifu mkubwa sana, ndiyo maana sisi tumechukua hatua,” alifafanua Pinda. Alisisitiza ufanyike utekelezwaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Mwanza ili kuharakisha maendeleo kwa wananchi wa mkoa huo.
   
 2. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #2
  Sep 20, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,191
  Trophy Points: 280
  Pinda's humility is disarming. I only wish he was as competent as he is humble.

  Maneno hayo kusemwa na kiongozi Tanzania si jambo rahisi. But is he really that humble?

  Ama anatumia usanii wa hali ya juu ama kazidiwa kweli na hawezi ku manouvre zaidi ya kusema ukweli.

  All in all alichosema kuhusu kuzomewa ni kweli, na kwa hilo kumsema zaidi kutakuja pale tu nitakapoona maneno yake hayafuatiwi na vitendo.

  Kama it takes zomeazomea ili viongozi wapate message, basi wananchi wazidi kuzomea mpaka kieleweke.
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Sep 20, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hapo ni Mwanza, ajaribu kwenda Arusha. Viongozi wamekuwa sooo out of touch na Pinda ni mmojawapo. If I was a betting man ninge-bet kabla ya 2015 wananchi watawarushia mayai viza viongozi.
   
 4. salosalo

  salosalo JF-Expert Member

  #4
  Sep 20, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 579
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  Sababu iko wazi. "Kasungura ni kadogo" ndio utetezi wenu juu ya matatizo yetu wananchi huku kila kiongozi akiondoka na mguu mzima wa Kasungura na kutuacha wananchi tukigawana ngozi na manyoya ya kasungura. Msipojirekebisha tegemeeni zaidi ya hayo maana tumechoka na hatuna namna nyingine. Hata hivyo nakupa pole sana kwa yaliyokukuta
   
 5. james chapacha

  james chapacha JF-Expert Member

  #5
  Sep 20, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 942
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  kwi kwi kwi kwi mtoto wa mkulima kakutana na watoto wenzake,walio mzomea niwatoto wa wakulima vilevile.
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  Sep 20, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160

  [​IMG]
  Martin Luther King Jr. being denied entry
  to the whites only Monson Motor Lodge restaurant
  by owner Jimmy Brock. Current site of Hilton Hotel.

  Nadhani ametafakari kutosha hali inavyozidi kuwa badala ya kuwa nafuu mambo yanazidi kuwa magumu. Mlolongo wa malalamiko ya wananchi kutokana na serikali kuweka kiporo shughuli za kimaendeleo jiji la Mwanza kwa vile linaongozwa na halmashauri ya Chadema ni kitanzi zaidi kwa serikali ya CCM, kwani watu wanajua serikali si ya chama fulani bali ya walipa kodi wote.

  [​IMG]
  View of St. Augustine from the top of the lighthouse on Anastasia Island

  Ni kweli ameonyesha unyenyekevu kiasi fulani, lakini tone la maji ndani ya bahari ni nini? Lakini kama kweli unyenyekevu wake ni wa kweli, tusubiri mwujiza kama ule uliomtikisa ubongo msomi Mtakatifu Augustino wa Hipo huko Khatago kaskazini mwa Afrika alipokuwa akitafakari siri ya utatu wakati wa maditation kando ya bahari ya kati, mara akamkuta mtoto mdogo akichota maji ya bahari kwa kopo kisha kutia kwenye shimo dogo. Alipodadisi mtoto yule alimwambi siri ya anachofikiria kuwa ni ngumu kuelewa katika utawala wa Mungu kuliko kuamini kama anaweza kujaza maji yote ya bahari kwenye kashimo kale.
   
 7. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #7
  Sep 20, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Kama kwa pinda ndo hivo kwa mkuu wa kaya itakwaje
   
 8. B

  Bahati Risiki JF-Expert Member

  #8
  Sep 20, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 531
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tuzomee tu bila kuchoka. Nchi inauzwa, wananchi wanauawa, shule zimekufa, hospitali hoi, kisa ulafi wa CCM na viongozi wake. Tuwazomeeee hadi wakimbie wenyewe!
   
 9. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #9
  Sep 20, 2012
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mwanza hatuna mzaha,kama hawaamini magamba tunawangoja kwenye kimbembe cha udiwani kata ya Kitangiri na Igoma
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Sep 20, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,741
  Likes Received: 82,676
  Trophy Points: 280
  Duh! Anatishika na kuzomewa lakini hatishiki na maisha ya ufukara wa kutisha wanayoishi Watanzania wengi!!! pamoja na kuwa nchi ina utajiri mkubwa wa rasilimali. Hakutishika alipotoa kauli ya kushangaza kuhusiana na mafisadi wa EPA kwamba, "Wezi wa EPA ni matajiri wakubwa sana nchini, kama wakikamatwa nchi itawaka moto."

  Hivi huyu anaishi nchi ipi ambayo hajui kama Watanzania walio wengi hawaridhishwi na utendaji wa Serikali kwenye kila sekta uchumi, uhamiaji, sheria, afya, elimu, huduma muhimu n.k.? Kama alivyosema Mkuu Kiranga naunga mkono kuzomea zomea viongozi wote wa magamba na Serikali ambao kwa njia moja au nyingine ndio wanakuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo nchini.


   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #11
  Sep 20, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Mkuu wa kaya Iringa na Mbeya hakatizi. Walishawahi kumpopoa madongo, wakalala barabarani.
  Pinda ni msanii! Nimekumbuka alipoangua kilio bungeni kuhusu Albino! Aisee, hakulia alipozomewa?
   
 12. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #12
  Sep 20, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Umempa heko, umetuambia Pinda ni humble, sasa iweje tena utuulize sisi kama Pinda ni humble? There we go again na matatizo ya Mtanzania ya kujieleza....

  Wameenda mbali zaidi ya kuzomea, tusifumbie macho vurumai na jinai. Jamii ya watu wasiozoea law and order ndio inaona ni poa kwa kurushiana mawe baada ya kuzomeana. Ukitupa mawe kwenye magari ya Waziri Mkuu walinzi wake wangefanya wanachotakiwa kufanya tungekuwa tunaongea mengine saa hizi...
   
 13. m

  makundi4619 JF-Expert Member

  #13
  Sep 20, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 486
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  BAK: Ulivyosema ni kweli kabisa!Viongozi wa CCM wamezoea kuwazuga wananchi na kuvifanyia hila vyama vya upinzani. Watanzania ni watu wenye subira na ni wapole hii ikawafanya CCM na serikali yake wajisahau. Mtu mpole uvumilivu ukimwisha hashikiki. Wananchi wamechoka. Kinachotakiwa sasa ni elimu ya uraia ipewe kipaumbele na utawala mpya kuzingatia utawala bora na kuyaweka maanani mahitaji ya wananchi kwa kuwashirikisha badala ya kuwaburuza, kuwakejeli na kuwadharau!!!
   
 14. Foum Jnr

  Foum Jnr JF-Expert Member

  #14
  Sep 20, 2012
  Joined: Jul 27, 2012
  Messages: 272
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Alama za wakati, rudini kwa wananchi muwasikilize, jipangeni kwa utawala wa uadilifu na ihsani, rejesheni utawala wa sheria katika nchi, la si hivyo jitayarisheni na dhoruba inayokuwa yenye nguvu ya demokrasia ya kweli.
   
 15. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #15
  Sep 20, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,110
  Trophy Points: 280
  afadhali ametambua chanzo, tuachane na wale CCM addicted, wanajiona wako bora wakati ukweli wameoza.
   
 16. Viol

  Viol JF-Expert Member

  #16
  Sep 20, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 18,982
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  yule huwa anadondosha tu chozi la kisanii ili ahurumiwe
   
 17. M

  Malipo kwamungu JF-Expert Member

  #17
  Sep 20, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 574
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Kwanza unyenyekevu wa Mtoto wa mkulima pekee unaonyesha dhamira ya dhati aliyonayo 'Hapendi uonevu,dhuluma na udhaifu wakila aina unafanywa na watendaji dhaifu wanaomzunguka kila upande" Alichokiri mtu mzima ni mustakabali wa viongozi wataifa hili na hadhali ya kweli ktk matendo yao na utendaji wakila siku hivyo alipo kubali kuwa amezomewa anatoa ANGALIZO kwao!:alien:
   
 18. KXY

  KXY JF-Expert Member

  #18
  Sep 20, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 876
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 60
  Tatizo jingine ni kukosa wepesi wa kuelewa

  Hayo maneno 'bolded' yana ugumu gani kwako ?
   
 19. KXY

  KXY JF-Expert Member

  #19
  Sep 20, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 876
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 60
  Je, hao wananchi wanamuona yeye kama waziri mkuu wao, anawakilisha wanachokiamini?

  whats a god to a non believer?
   
 20. G

  GlorytoGod Senior Member

  #20
  Sep 20, 2012
  Joined: Sep 8, 2012
  Messages: 157
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  LOVING.jpg umoja wa vijana wa ccm mkoa wa mwanza wamemlalamikia na kumlaani mbunge wa chadema wa nyamagana ezekia wenje kuwa aliandaa vijana waliohusika kumzomea waziri mkuu.
  Hivyo wamemtaka amtake waziri mkuu radhi kwa hicho kitendo alichokifanya.

  Source: Magazeti ya leo

  swali: Ni jukumu la waziri mkuu kujiuliza kama serikali yake inayoyafanya kwa wananchi ni mema au ni mabaya yakustahili kuzomewa au la. Ni lazima ajitathmini kwa upya na ninacho amini ni kuwa tatizo siyo wenje tatizo ni ccmajambazi a.k. A. Choo cha makuti.


  Wadau mnasemaje
   
Loading...