Pinda akerwa na ‘ujeuri’ wa Barrick

VIKWAZO

JF-Expert Member
Apr 9, 2011
1,899
580
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ameoneshwa kukerwa na jeuri inayooneshwa na uongozi wa Mgodi wa Dhahabu wa North Mara (Nyamongo) unaomilikiwa na Kampuni ya African Barrick Gold uliopoTarime katika kuwasaidia wananchi wanaozunguka mgodi huo.

Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Mkoa wa Mara baada ya kuwasili hapa, Pinda alisema pamoja na kuzungumza na uongozi wa mgodi huo, atazungumza pia na wananchi wa vijiji vinavyozunguka mgodi huo.

Alisema matatizo na migogoro baina ya uongozi wa mgodi huo na wananchi ni moja ya sababu zilizomfanya kuomba kukutana na uongozi wa Mgodi wa Nyamongo wakati wa ziara
yake mkoani hapa.

“Hili suala la madini lina changamoto kubwa, ndio maana niliomba mwenyewe niende Nyamongo nizungumze na uongozi na wananchi, Serikali itoe tamko kuhusiana na suala hili maana haiwezekani mwekezaji anakuja na jeuri, mgodi upo katikati ya watu, yeye hataki kushirikiana nao na kila anapoelezwa anasingizia uwekezaji.

“Hatuna maana kwamba wawekezaji wawawezeshe wananchi kuwa matajiri, lakini kuna ile misaada ya kijamii ambayo ni lazima wasaidie.

Unakuta mgodi una umeme mwingi unaowatosha na kubakia wa ziada au maji, lakini mwekezaji hataki hata kuwapa kidogo wananchi wa jirani huku ni kutafuta uadui wa bila sababu,” alisema Pinda.

Alisema atakapofika katika Mgodi wa Nyamongo atafanya mazungumzo na uongozi wa mgodi na wananchi wa jirani ili kujifunza kiini cha migogoro inayotokea mara kwa mara kati ya wananchi na mgodi ili kupata ufumbuzi.

Alisema Serikali haitavumilia tena kupokea wawekezaji ambao baada ya kuwasili nchini na kuwekeza wanaanza kutoa kauli za kijeuri dhidi ya Serikali kwa kisingizio kwamba wao ni wawekezaji wanaotafuta faida.

“Hatuwezi kukubali eti kwa vile wanawajibika kwa Wizara ya Nishati na Madini, basi watu wengine wasiwaguse au kuhoji juu ya suala lolote, ni lazima faida wanayoipata isaidie kupunguza matatizo ya kimsingi kwa wananchi wa jirani,” alisema.
 
Wamesahau ile kauli ya UN Juu ya uwekezaji kuwa ni People, profit then planet.
 
Huyu Barrick jeuri yake inatokana na rais wetu kukubali kuhongwa. Hawa walisema mtatufanya nini, hata rais wenu tunamhonga? What do you expect?
 
these big mining companies are less contributing the so called "cooperate social responsibility" but our gv has been blind to see that,Pinda is just playing a hoax to regain his lost popularity in real sense is not one to be expected to take concrete measures to STOP that moving train of downpression
 
Hizo porojo za pinda zisizo na utekelezaji tumeshazizoea.Hawa wanahadaa wananchi akizunguka analipiwa ticket ya kwenda na kurudi ulaya na hao wawekezaji anakunja mkia.Mungu ibariki tz
 
Tatizo Pinda anaga maamuzi yupo yupo 2 hapo ndo namkumbukaga Lowasa ni fisadi lakini anamaamuzi Kama kiongozi

Na wewe usiturudishe nyuma na watu wako wachafu wa maadili. Wewe unataka wakurupukaji? Mimi nadhani hatua ya Pinda ni nzuri na hata siku moja serikali haiendeshwi kwa kukurupuka na kufoka foka kama unvyotaka wewe!
 
Na wewe usiturudishe nyuma na watu wako wachafu wa maadili. Wewe unataka wakurupukaji? Mimi nadhani hatua ya Pinda ni nzuri na hata siku moja serikali haiendeshwi kwa kukurupuka na kufoka foka kama unvyotaka wewe!
HIvi ni uamuzi upi Pinda amewahi kufanya. Tatizo ni unafiki tu hapa!! Pinda JK na viongozi wote wa magamba wako mifukoni mwa wawekezaji. wengine hata C**p** watahongwa!
 
Msanii tu huyu. Vilio vya Watanzania kuhusu wizi unaofanywa na Barrick viko kwa miaka chungu nzima sasa. Wakati Barrick's Management na Shareholders wao wakiendelea kuvuna bilions of dollars kupitia dhahabu yetu Watanzania tunaambulia vimilioni vichache tu halafu Watanzania tukija juu kuhusu wizi wao Barrick, wanakuja na usanii wa kudai kutoa shilingi 16 billioni eti "kusaidia jamii"!!!! na wakati huo huo wanaidai Tanzania U$273 million, kwa maoni yangu ni deni ambalo limejaa ufisadi mtupu.
 
si wale wale tu!unafiki ndo unaomkera na si vinginevyo!km rais hana jeuri yeye anatoa wapi jeuri!damn leaders
 
Kweli kila siku kuna wasanii. Hata hao wanaijiita wawekezaji wakiamua kuwapa hao wananchi umeme anaodai wa ziada Tanesco wako tayari kuuchukua? TPC pale Moshi wana umeme wa ziada kila wakifanya mawasiliano na Tanesco waongeze umeme wanagoma. Mji wa moshi wote unaweza kupewa umeme na TPC bila shida. Hawataki hawa ama hawana taarifa hizo? Waache unafiki wao. Aseme naye anaenda kuchukua kilo zake kadhaa za dhahabu atkomee zake!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom