Pinda akerwa na mikataba mibovu

Hii serikali ni ya hovyo kuliko zote zilizowahi tawala Tanzania. Rais analalamika kuwa haoni juhudi za kuondoa mgao wa umeme, analalamika wamempa digrii asizostahili, analalama mikataba mibovu. Waziri mkuu naye halikadhalika!

Kwa nini wasijiuzulu tukafanya uchaguzi upya ili tupate viongozi watakaochukua hatua?
 
Kwa kauli yake hiyo, inaonekana alipoteuliwa hakupewa Katiba ya Nchi inayobainisha wajibu na majukumu ya PM aliyonayo kisheria. Kama anayo, basi hajui kutafsri majukumu yake. Afukuzwe kazi. Anatutia kinyaa watanzania kwa kusema anakerwa na mikataba mibovu huku anao uwezo wa kulifanyia kazi. Au akae kimya tu. Alikuwa anajikosha kwa wanafunzi ili asizomewe. Je hiyo inatosha?
 
Hivi ule alioingia kule kwa wazungu kuwamilikisha ardhi yetu mpaka mkataba unapingwa na taasisi nyingine za kimataifa ndio uingiaji mzuri wa mikataba?

Labda kwa uelewa wake anadhani ardhi aliouza kwa mkataba wa Iowa ndioi mkataba bora. Halafu udsm jana wamemtunuku!
Mambo kama haya ndo yanawa encourage viongozi wa hovyo kuendelea kufanya mambo ya hovyo kabisa.

Waziri mkuu wa kulialia na kulalamika, hawezi hata kumuwajibisha mtu aliye ndani ya mamlaka yake.
 
mkuu is not fallacy?

Na pinda juzi kasaini mkataba huko usa ule nao vipi ? Hauna matata hata kidogo ?au ni siasa tu kila mahali ?

Kaka lunyungu, ni FALACY KUBWA TU.
Anaharibu yeye mwenyewe, anashindwa kuwadhibiti waliochini yake walioharibu halafu anakuja kivingine na kujifanya ana huruma kwa wazawa, ndo hiyo appeal to pity ili awakamate wengi hasa wale wanaofikiri kimasaburi kwamba waziri wetu anatupenda, anatuhurumia, anakerwa na madudu yanayofanywa. Huu wote ni uongo, thats why fallacy. Shame on pinda
 
Waziri mkuu Mizengo Peter Pinda amesema anakerwa sana na mikataba mibovu ambayo Taifa letu linaingia

Source: Mzalendo - Jumapili 22/10/2011

Sasa akikerwa ndio kafanya nini...embu acha kulia timiza wajibu wako
 
Waziri mkuu Mizengo Peter Pinda amesema anakerwa sana na mikataba mibovu ambayo Taifa letu linaingia

Source: Mzalendo - Jumapili 22/10/2011
Yeye ni sehemu ya tatizo, shida ya huyu mzee ni kulalamika,,,,, ndio hawa mnaotuandalia 2015, kazi tunayo yeye alie, wananchi walie, usafi peke yake hautoshi kama mamlaka umepewa/tumekupa afu unalalamika badala ya kuchukua hatua,,, du, heri mimi sijasema
 
Hata mimi namzidi pinda kwa utekelezaji...yeye ni kukerwa tu bila kuchukua hatua...bora mimi nikikerwa na utekelezaji na chukua hatua kwenye boksi la kupigia kura..
 
hana lolote analoweza alimshindwa jairo utamuweza nani ,,,yeye ale posho tu muda wak upite
 
Waziri mkuu Mizengo Peter Pinda amesema anakerwa sana na mikataba mibovu ambayo Taifa letu linaingia

Source: Mzalendo - Jumapili 22/10/2011
Viongozi wasio na matumaini hawawezi kuwapa matumaini watanzania!!!!!hopeless
 
Inashangaza kabisa umepewa wajibu hautimizi badala yake unageuka kuwa mlalamikaji!? Kwa mwendo huu itatuchukua miaka mingi(450) kuwa kama South Africa.
 
tehe ataishia kusema tu uwezo wa kuwafuatilia hana, mwenzie sokoine mbona alidili sambamba na wahujumu uchumi, yeye anashindwa nini?
Yeye anakerwa tu unataka achukue action kwani hajui yaliyomtokea puani Mwa maembe?
 
Hapo kitambo kulikuwa na mashindano ya sura Mbaya ambayo hata Remmy aliwahi kushiriki,hivi kwanini yasirudishwe ili tumpeleke Pinda akashiriki nafikiri ni kazi inayomfaa kuliko uwaziri mkuu.
 
Waziri mkuu Mizengo Peter Pinda amesema anakerwa sana na mikataba mibovu ambayo Taifa letu linaingia

Source: Mzalendo - Jumapili 22/10/2011

Kukerwa ni hatua moja,kuchukua hatua nayo ni hatua nyingine Ila kulalamika tu bila vitendo ni unafiki mkubwa kwa kiongozi Kama yeye.Hivi Kama yeye Pinda analalamika na yupo Serikalini sie wananchi wa hali ya chini tutafanyaje wkt tunamtegemea yeye Kama Waziri kututetea?
 
Back
Top Bottom