Pinda akerwa na Kigoma kuendelea kutoza ushuru wachuuzi wadogo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda akerwa na Kigoma kuendelea kutoza ushuru wachuuzi wadogo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sir.JAPHET, Aug 10, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Thursday, 09 August 2012 21:08

  Reginald Miruko, Dodoma
  SERIKALI inachunguza sakata la Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma la kugoma kutekeleza tamko lake la kuitaka kuacha kukusanya ushuru kwa wachuuzi wadogo.Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alilieleza Bunge jana wakati akijibu maswali ya papo kwa hapo, kuwa kodi hizo ni kero na bughudha kwa wananchi wanaotegemea biashara ndogo ndogo na mboga mboga kujipatia mahitaji yao.

  Alisema badala ya kodi hiyo , Serikali ilianzisha ruzuku maalumu ili kufidia pengo lililotokana na kufuta kwa ‘kodi kero’ kwa wananchi.Maelezo ya Waziri Mkuu yalitokana na swali lililoulizwa na Peter Serukamba (Kigoma Mjini-CCM) juu ya meya wa Manispaa wa Kigoma kufunga masoko akilazimisha kodi hizo kutozwa, licha ya kuwapo tamko la Naibu Waziri wa Tamisemi, Agrey Mwanri, na kuzuia kodi hizo.

  Pinda alisema, tamko la Mwanri ni sahihi kwa kuwa wananchi wanaofanya bishara za uchuuzi wanabughudhiwa, hivyo akaahidi kutoa agizo hilo kwa maandishi ili kuona nani anayekataa kutekeleza.
  “Kama Kigoma wameona General Purpose Grant (GPG) haiwafai, sisi tutawithdraw (tutaiondoa) ili tuone kama huo ushuru utaweza kuwasaidia,” alisema Pinda.
  Katika swali lake la msingi, Serukamba alisema Serikali ilianzisha GPG ili wachuuzi wadogo wasitozwe ushuru na maelekezo yametolewa na Mwanri akiwa Kigoma, lakini halmashauri zimekataa zinaendelea kuutoza.
   
 2. kanga

  kanga JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,011
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Pinda hajui chochote hapo, Serikali za Mitaa ni serikali huru na zilizopo kwa mujibu wa sheria,asitafute ummarufu wa kienyeji hapo.Na dawa kama ya akina Pinda kwenye Katiba Mpya tutazidi kuweka hadi mapato yake kwenye katiba mpya ili kuwabana wanasiasa uchwara kama Pinda kupindisha sheria.50% ya bajeti ya serikali ya OC na DEV zinazokusanywa na TRA lazima ziende Serikali za Mitaa maana ndiko kuliko na WATU kuliko ilivyo sasa fedha nyingi zinabaki SERIKALI KUU KWA AJILI YA WATAWALA AKINA KIKWETE NA PINDA KUFANYA UZURURAJI DUNIANI.
   
Loading...