Pinda akataa shangingi Toyota VX 8 ya Tsh 280 milioni!

uzalendo gani?mnajua hizo gari zilinunuliwa oktoba 2010 landcruiser vx na gx idadi yake 65 zote brand new?alikua wapi wakati zinanunuliwa?ccm wanafiki tuu hakuna mwenye uchungu na raia
 
huyu pinda ni hovyo sana... kukaa ikulu miaka mingi kumemuathiri sana .......anafanya kazi kama vle bado yuko TISS......

kwa nini asipendekeze aina za gari za kutumia kwa mawaziri?!! leo anapokataa gari alone tumwelewe?

hakika nawaambia huyu nae hataleta mabadiliko atabaki kulia lia tu.....
 
Kama PM anaweza kushtukizwa katika ishu kama hii ina maana kuna vijisent vingine vingi vinavuja bila yy kujua
 
Hana jipya hao anaotarajia kuwakosoa wana nguvu kuliko yeye mwenyewe ataanzia wp sasa.......Kwa taarifa yako Mafioso wanafurahia sana Utendaji wake wa kazi ndio maana yupo pale ......Maana hawazuuu kufanya chochote ,wakati wowote popote...

Ulitarajia akatae Ununuzi wa hayo magari halafu wenye nchi (mafisadi)warutarudisha vp misaada na fedha walizochangia Chama?

Nchi ishauzwa hii......Soma nyuma ya risiti "Mali iliyouzwa Hairudishwi"
 

- Gari alilolikataa ni gari la ubunge ambalo kila Mbunge anatakiwa kupewa anapoanza ubunge, hizo hela za hayo magari zimo kwenye bajeti tayari kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri, sasa Mbunge anaweza kukataa gari lakini hawezi kusimamisha katiba eti kwa sababu yeye ni Waziri Mkuu na kuzuia wabunge wengine wasipewe magari.

Tuache kupotosha mambo. Wabunge hawepewi magari na serikali na wala hamna bajeti ya namna hiyo. Wala hamna kipengele kwenye katiba kinachosema hivyo. Wabunge wanakopeshwa hela na mabenki kujinunulia magari yao binafsi na wanakatwa moja kwa moja kwenye mishahara yao. Hayo magari yanakuwa ya kwao binafsi. Waziri mkuu amepewa gari kama waziri na sio mbunge.
 
yaani waziri mkuu anaashitukizwa!!!!!

kumbe kuna wizi inafanyika pasipo yeye kujua!!!!
 
- Mkuu hamna jipya hapa, unasema wanakopeshwa! halafu hela za kuyalipia zinalipwa nani? Hebu piga hesabu ya hela za mbunge in five years akiwa bungeni hivi kweli anaweza kuyalipia haya magari akamaliza in five years?

- Pole sana mkuu!

Ndiyo inawezekana kwasababu hawakopeshwi magari ya milioni 300. Tuache kudanganyana. magari wabunge wanaokopa ni kawaida na sio hayo mashangingi ya serikalini.
 
Nimeenda nchi nyingi za Asia, Ulaya, na hapa East Africa. Ili tuweze kusonga mbele bado serikali yetu inatakiwa kuwa na discipline ya matumizi ya pesa. Sehemu nyingi nilizotembea hawana mashangingi kama haya hapa kwetu japo wana pesa kutuzidi. Imeshafikia hatua tunanunua magari kwa ufahari na sio kama kitendea kazi! Land cruiser hard top au 110 ingeweza kutumika kwa ufasaha na kwa bei ya chini. Wanasiasa wasitake kushindana na wafanyabiashara kwani wafanya biashara wanatumia pesa zao na wanasiasa wanatuia pesa zetu na niwajibu wetu kuwahoji. Mimi nakatwa kwenye mshahara wangu kila mwezi million 2 ningependa pesa hiyo iwasomesha maskini au iwatibia maskini wasiojiweza.
 
uwezo wa pinda mi nadhani ni mdogo sana hafai kuwa PM maana iwapo ofisi yake wanaweza kutumia 280 million na yeye ndiye anayetoa kibali cha magari kununuliwa inakuwaje asi?hawajibiki? haendi ofisini muda mwingi ziarani haya ndio matokeo yake.

JK nipe nafasi uone kazi
 
Kwa kweli mtoto wa nyoka ni nyoka. Yaani William unatuambia mbunge wa mahenge hawazi kufika kwake bila ya gari la milioni 300? Hivi mbona nyie watu mliokulia kwenye neema mna matatizo sana? Ni mahali gani hapa tanzania ambako Toyota Hardtop (mkonga) haifiki? Tena mkonga inaweza kuwa ya uhakika zaidi kuliko hata hilo shangingi! kwa uwezo wetu mdogo wa serikali, hakuna sababu yoyote ya msingi ya mtu kutumia gari la milioni 300 wakati kuna VX za milioni 120 ambazo na zenyewe zinaweza kufanya kazi sawasawa na hiyo Vx 8. Jamani, hebu wakati mwingine tuwahurumie na wale watu wa vijijini wanaoishi kwa mlo mmoja.

Ukweli uliyoje! Halafu mazingira wanayotokea hawa watu umaskini umetamalaki. Kwa ambaye ameshafika Dodoma sehemu za vijijini ataelewa nina maana gani! Lakini ndugu yangu hawahurumii agwe wenzake!
 
Hivi mnajua kua hayo magari yananunuliwa kwa gharama kubwa sana lakini baadae wanakuja kuuziana wenyewe kwa bei rahisi sana. Mfano mzuri juzi nilikua ziarani mkoa wa Kigoma nikaikuta toyota Hilux katika chuo cha matabibu amenunua mtu kutoka wizara ya afya kwa sh laki 3.
 
hizo gari zilinunuliwa 65 siku zinahamishwa toka makumbusho usalama wa taifa kwenda ikulu nilitamani kulia.yalikua meupe yote full tank diesel.na zimenunuliwa octoba 2010 swali pinda hakujua kuwa yatanunuliwa?
 
hizo gari zilinunuliwa 65 siku zinahamishwa toka makumbusho usalama wa taifa kwenda ikulu nilitamani kulia.yalikua meupe yote full tank diesel.na zimenunuliwa octoba 2010 swali pinda hakujua kuwa yatanunuliwa?
Kashakwambia hakushirikishwa kwenye mchakato..sasa unataka akuapieje?
 
kichwa cha habari 'pinda akataa shangingi'.......sie wakuda tumeelewa vingine...teh teeeeeeeeh
 
Wana JF, Naomba kuuliza kabla hatujamshambulia pinda, mwenye kampuni inayonunua hayo magari ya serikali ni nani? na anahuusiano gani na JK. Ukipata ilo jibu ndi umshambulie mtoto wa mkulima.
 
tamko ameshatoa hebu soma vizuri na kwaumakini maeleze hapojuu pinda ameshatoa maagizo yakubana matumizi nakupunguza kwakiasi kikubwa matumizi yakifahari ya pesa zawalalahoi,hongera mkuu pinda kwakuonesha mfano,ila unatakiwa uwemkali kidogo ili agizolako la kubana matumizi lifanyiwe kazi kwavitendo,hakika ukilisimamia hilo kwa umakini nina iman utafanikiwa na utakumbukwa daima nawalalahoi wa nchi hii,na utaandikwa ktk vitabu vya kumbukumbu za histroria ya taifa hili,aluta continua mjomba pinda mimi nakukubalisana,hakika wewe ni muadilifu na usiependa makuu.

Kama alishatoa tamko imekuwaje tena watendaji wa serikali wakanunua gari la kifahari? Hii inaonyesha tamko lake lilikuwa ni kufurahisha tu umma au Pinda mwenyewe hayuko serious katika utendaji wake wa kazi. Kama alikuwa ni mtu serious angafuatilia kuhakikisha tamko lake linafuatwa na kinyume na hapo watendaji watakaofanya vinginevyo wanachukuliwa hatua mara moja. Kifupi serikali ya Tanzania imeoza. Watanzania wanahitaji kufanya mabadiliko makubwa kwenye uongozi wa nchi.
 
Kama kawaida, paukwa pakaya nyingine ndani ya Tz. Masikini, sina uhakika kama yule mama aliyepoteza mwanaye pale hospitali kwa ukosefu wa vifaa vya kumsaidia aweze kujifungua, hili akilipata likamea ndani ya bongo yake anaweza kumsamehe hy PM, analalama wakati yy ndiye kiranja anategemea huruma kutoka wapi. Pinda tandika kazi, acha kutafuta huruma toka kwa wananchi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom