Pinda akataa shangingi Toyota VX 8 ya Tsh 280 milioni!

Ustaadh

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2009
Messages
413
Likes
7
Points
0

Ustaadh

JF-Expert Member
Joined Oct 25, 2009
413 7 0
  • Gharama yake Sh280milioni, asema nchi yetu ni masikini
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameonyesha kwa vitendo kuwa yeye ni mtoto wa mkulima baada ya kukataa gari jipya ka kifahari alilonunuliwa na wasaidizi wake kwa akisema kwamba alilonalo linamtosha.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana jioni kwa njia ya simu, Pinda alisema kuwa uamuzi huo aliuchukua mwaka huu kabla ya uchaguzi mkuu kuanza baada ya kukataa kulitumia gari jipya aina ya Landcruiser VX 8 lenye thmamani ya sh milioni 280.

Alisema kuwa aliamua kukata kulitumia gari hilo baada ya kungundua kuwa alilonalo ambalo ni la bei ndogo kuliko hiyo bado lina uwezo.

"Ni kweli nimelikataa kulitumia gari hilo kwani niliona hata gari hili ambalo nimeanza nalo kulitumia kama mawaziri mkuu bado halikuwa na matatizo, sasa kwa nini nipewe jingine jipya, hii itakuwa ni matumizi mabaya fedha za serikali," alisema.

Alisema baada ya kulikataa kulitumia gari hilo aliwaagiza watalaam wake kwa sababu tayari walishalinunua kumtafuta mtu mwingine wa kumpa kulitumia, lakini kama angeshirikishwa katika mchakato wa awali hangewakubalia.

Pinda aliteuliwa kuwa Maziri Mkuu mwaka 2008 baada ya aliyekuwa akishika wadhifa huo, Edward Lowassa kujiuzulu kutokana na kuibuka kwa kashfa ya Richmond pamoja na mawaziri wengine ambao Ibrahim Msabaha aliyekuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Nazir Kamaragi aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini.

Pinda ambaye anakuwa Waziri Mkuu wa kwanza kukataa gari jipya alilonunuliwa kwa lengo la kubana matumizi alisema kuwa watu wanatakiwa kujua kuwa Tanzania nchi masikini sana hivyo tunahitaji kutumia vyema kipato chetu badala ya kukitumia kwa matumizi ambayo sio ya lazima.

Alisema kuwa mazoea ambayo Watanzania wajijengea kwamba viongozi wa juu wa serikali wanapenda kila mara vitu vipya na vya gharama kubwa hanapaswa kufutwa kwa vitendo.

"Hii tabia ya kufikiri kwamba gari zuri lazima liendane na hadhi ya mtu ni vyema sasa tukaiacha," alisema na kuongeza:

"Kutokana na tabia hii hata watengenezaji wa magari nao wamejua udhaifu wetu wamekuwa wakijaribu kubadilisha muundo kidogo tu na kuja na magari mpya ambayo wanayauza kwa bei kubwa".

Pinda ambaye ndiye anayetoa kibali cha ununuzi wa magari ya serikali alisema hatakubali kuidhinisha viongozi wa serikali kutaka kununua magari ya kifahari wakati wanaweza kutumia magari ya kawaida.

Hata hivyo,alisema kuwa hawezi kupiga marufuku moja moja ununuzi wa magari ya kifahari kwa vile ni jambo ambalo linahitaji kuchukuliwa kwa hatua, lakini taratibu watedaji wa serikali watahamia katika kutumia magari ya kawaida.

Waziri Mkuu ambaye akiwashukuru wabunge kwa kumwidhisha kuwa waziri mkuu alisema yeye ni mtoto wa mkulima, alisema suala la kudhibiti ununuzi wa magari ya fahari kwa viongozi wa serikali alishaalianza muda mrefu.

Mwaka jana Pinda, aliwaagiza watendaji wa serikali watafute namna ya kupunguza matumizi ya fedha za umma ikiwa ni pamoja na kutonunua magari ya kifahari.

Aliwataka watendaji hao wabadilike, waache ubinafsi na wasijifikirie wao tu, kuna mamilioni ya watanzania wanaohitaji fedha kidogo zilizopo.

Katika Wizara za Serikali kuna magari mengi ya aina ya Toyota Land Cruiser VX yanayouzwa kati ya Sh 160 milioni hadi Mwaka 2008 serikali chini ya uongozi wa Pinda ilifanya marekebisho makubwa ya namna ya udhibiti wa uendeshaji wa magari ya kifahari kwa mawaziri na viongozi wengine ili kuondokana na matumizi mabaya ya mali za umma.

Ripoti ya Mpango wa Serikali kuhusu Orodha ya Magari yake na Kudhibiti Matumizi ambayo ilipendekeza pamoja na mambo mengine magari ya kifahari ya mawaziri maarufu kama mashangingi yanunuliwe kila baada ya miaka saba badala ya miwili ya wakati huo.

Utaratibu uliozoeleka ni kwamba, gari la waziri huweza kununuliwa kila baada ya miaka miwili tangu linunuliwe na kuanza kutumika, kisha hutumiwa na watendaji wa ngazi ya chini, au kuuzwa au waziri 'kujiuzia'.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya serikali ya mwezi Aprili 2008 jumla ya magari yote ya serikali nchini yalibainika ni kati ya 35,000 hadi 40,000.

Kati ya orodha hiyo magari ya kifahari ya Toyota Landcruiser Vx8 na VX, Gx na aina nyingine ya Landcruiser yalikuwa kati ya 10,000 hadi 15,000.

Takwimu za sasa, gari moja aina Toyota VX8 linauzwa kwa sh 280 na kwamba VX la kawaida ni sh 120 milioni, huku gharama za operesheni ikiwa ni pamoja na matengenezo ya kila wiki na mafuta ni kati ya Sh moja hadi 1.5 milioni, kutegemea safari.

Magari hayo 40,000 ni kuanzia Serikali Kuu na Halmashauri za Wilaya, miji, manispaa na majiji, ambayo ni pamoja na yale ya miradi maarufu kama DFP ambayo hutokana na wafadhili.

Orodha hiyo inaonyesha sehemu kubwa ya magari hayo ni Toyota Pickup na Hard Top, ambazo zimekuwa zikitumika zaidi vijijini huku mashangingi ya Vx na Gx yakirandaranda mijini.

Pendekezo la serikali ni kwamba katika ngazi ya Serikali za Mitaa, linataka Mkuu wa Mkoa pekee ndiye atumie Vx ili kuwezesha Rais anapofika aweze kulitumia huku Wakuu wa Wilaya na watendaji wengine wakitakiwa kupatiwa gari za kawaida kama Toyota Landcruiser si Vx.
 
Jay One

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2010
Messages
11,849
Likes
5,879
Points
280

Jay One

JF-Expert Member
Joined Nov 12, 2010
11,849 5,879 280
hana tamko as PM, yy kukataa na kuacha wengine wanunue magari ya kifahari ni kuonyesha how weak as PM he is, angetoa tamko kama PM,
hamna kununua magari ya kifahari, lack of commitment, hana na sitegemei jipya period
 
Mwera

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2010
Messages
967
Likes
1
Points
0

Mwera

JF-Expert Member
Joined Oct 26, 2010
967 1 0

tamko ameshatoa hebu soma vizuri na kwaumakini maeleze hapojuu pinda ameshatoa maagizo yakubana matumizi nakupunguza kwakiasi kikubwa matumizi yakifahari ya pesa zawalalahoi,hongera mkuu pinda kwakuonesha mfano,ila unatakiwa uwemkali kidogo ili agizolako la kubana matumizi lifanyiwe kazi kwavitendo,hakika ukilisimamia hilo kwa umakini nina iman utafanikiwa na utakumbukwa daima nawalalahoi wa nchi hii,na utaandikwa ktk vitabu vya kumbukumbu za histroria ya taifa hili,aluta continua mjomba pinda mimi nakukubalisana,hakika wewe ni muadilifu na usiependa makuu.
 
Mtazamaji

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2008
Messages
5,971
Likes
39
Points
0

Mtazamaji

JF-Expert Member
Joined Feb 29, 2008
5,971 39 0
Hiv gari za viongozi wa serikali zinatakiwa kutembea KM ngapi hadi waseme hazifai ?
Wizara ya Ujenzi imekaa standard na specifaction za kuitambua gari ambayo PM na mawaziri hawatakiwi kutumia.

Hili suala la mashangingi itatakiwa Magufuli na Mwakyembe walifanyie kazi.
 
Anfaal

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2010
Messages
1,157
Likes
6
Points
0

Anfaal

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2010
1,157 6 0
tamko ameshatoa hebu soma vizuri na kwaumakini maeleze hapojuu pinda ameshatoa maagizo yakubana matumizi nakupunguza kwakiasi kikubwa matumizi yakifahari ya pesa zawalalahoi,hongera mkuu pinda kwakuonesha mfano,ila unatakiwa uwemkali kidogo ili agizolako la kubana matumizi lifanyiwe kazi kwavitendo,hakika ukilisimamia hilo kwa umakini nina iman utafanikiwa na utakumbukwa daima nawalalahoi wa nchi hii,na utaandikwa ktk vitabu vya kumbukumbu za histroria ya taifa hili,aluta continua mjomba pinda mimi nakukubalisana,hakika wewe ni muadilifu na usiependa makuu.
Huyu Pinda alitoa tamko kabla ya hata gari hili kununuliwa. Alichotakiwa kufanya ni kuchukua hatua. Hivi akipewa mtendaji mwingine inamaana ndio ameepusha gharama? Kuna haja ya kuwachukulia hatua watumishi wa hivyo hii ya kutafuta umaarufu magazetini haitoshi.
 
Lukolo

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Messages
5,147
Likes
101
Points
145

Lukolo

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2009
5,147 101 145
Mpuuzi tu huyu, inasaidia nini kukataa gari halafu anasema apewe mwingine? Huyo atakayepewa atakuwa anatumia hela ya nani kama si ya serikali? Kama kweli ana nia ya dhati ya kupunguza matumizi mabaya ya pesa za serikali basi angeagiza kwamba iuzwe na pesa zitumike kwa shughuli nyingine. Na zaidi ya yote, hiyo gari aliyoikataa ni ile iliyonunuliwa kwa ajili ya waziri mkuu, je anasemaje kuhusu gari zilizonunuliwa kwa ajili ya wizara nyingine? Amewaambia mawaziri wengine kwamba na wenyewe wazikatae? Huyu Pinda kwa kweli hakustahili kuwa waziri mkuu. Hana bado sifa za kuwa waziri mkuu. Anashindwaje kutoa tamko na agizo kwa taasisi zote za serikali ili zisiendelee kutumia fedha kiholela? Hana lolote huyu.
 
Mtanganyika

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2007
Messages
1,611
Likes
308
Points
180

Mtanganyika

JF-Expert Member
Joined Jul 18, 2007
1,611 308 180
Huyu mzee simuelewi anasema ni matumizi mabaya ya pesa za serikali? Serikali inapesa? au pesa za walipa kodi?

Najiuliza ni kwa nini wawe na magari ya milion zote hizo za pesa?
 
Wacha1

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2009
Messages
12,765
Likes
1,028
Points
280

Wacha1

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2009
12,765 1,028 280
  • Gharama yake Sh280milioni, asema nchi yetu ni masikini
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameonyesha kwa vitendo kuwa yeye ni mtoto wa mkulima baada ya kukataa gari jipya ka kifahari alilonunuliwa na wasaidizi wake kwa akisema kwamba alilonalo linamtosha.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana jioni kwa njia ya simu, Pinda alisema kuwa uamuzi huo aliuchukua mwaka huu kabla ya uchaguzi mkuu kuanza baada ya kukataa kulitumia gari jipya aina ya Landcruiser VX 8 lenye thmamani ya sh milioni 280.

Alisema kuwa aliamua kukata kulitumia gari hilo baada ya kungundua kuwa alilonalo ambalo ni la bei ndogo kuliko hiyo bado lina uwezo.

..........................................

Kwa nini wanunuliwe magari na pesa za walipa kodi si wanunue kutoka kwenye mishahara yao? Wanalipwa pesa nyingi kwa shughuli wanazofanya kutokana na ajira wanapokuwa kazini.

Pinda kama waziri mkuu kama kweli anataka kuhakikisha mpunga wa walipa kodi hautumiwi vibaya apige marufuku mara moja ununuzi wa magari ya kifahari kwa wafanyaazi wa serikali. Haiingii akilini kwa nini bado tunanunua magari huu ni wizi wa mchana kweupe.
 
Mwera

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2010
Messages
967
Likes
1
Points
0

Mwera

JF-Expert Member
Joined Oct 26, 2010
967 1 0
Huyu Pinda alitoa tamko kabla ya hata gari hili kununuliwa. Alichotakiwa kufanya ni kuchukua hatua. Hivi akipewa mtendaji mwingine inamaana ndio ameepusha gharama? Kuna haja ya kuwachukulia hatua watumishi wa hivyo hii ya kutafuta umaarufu magazetini haitoshi.
ndio maana nikasema pinda anatakiwa awe mkali,afatilie maagizo yake kwa vitendo hapo atafanikiwa,nasisitiza tena namkubali pinda mtoto wa mkulima wa kibaoni mpimbwe katavi mweeeh.
 
Ustaadh

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2009
Messages
413
Likes
7
Points
0

Ustaadh

JF-Expert Member
Joined Oct 25, 2009
413 7 0
[FONT=&quot]Baadhi ya kauli za "mtoto wa mkulima":[/FONT]

  • [FONT=&quot]Wanawake kukata viuno kwenye majukwaa ni aibu kwa Mwanamke - Mh. Pinda[/FONT]
  • [FONT=&quot]Waziri Mkuu Mizengo Pinda amenukuliwa akisema watanzania waache kuvaa suti kwani ni gharama kwa wananchi maskini.[/FONT]
  • [FONT=&quot]Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amewaagiza watendaji wa Serikali watafute namna ya kupunguza matumizi ya fedha za umma ikiwa ni pamoja na kutonunua magari ya kifahari.[/FONT]
 
Jay One

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2010
Messages
11,849
Likes
5,879
Points
280

Jay One

JF-Expert Member
Joined Nov 12, 2010
11,849 5,879 280
tamko ameshatoa hebu soma vizuri na kwaumakini maeleze hapojuu pinda ameshatoa maagizo yakubana matumizi nakupunguza kwakiasi kikubwa matumizi yakifahari ya pesa zawalalahoi,hongera mkuu pinda kwakuonesha mfano,ila unatakiwa uwemkali kidogo ili agizolako la kubana matumizi lifanyiwe kazi kwavitendo,hakika ukilisimamia hilo kwa umakini nina iman utafanikiwa na utakumbukwa daima nawalalahoi wa nchi hii,na utaandikwa ktk vitabu vya kumbukumbu za histroria ya taifa hili,aluta continua mjomba pinda mimi nakukubalisana,hakika wewe ni muadilifu na usiependa makuu.
Hivi nini maana ya kutoa tamko hata mm nafaham hilo halafu no one anajali wala kufuatilia, huu ni udhaifu wa PM, hafai, na niseme kwanini angojee hadi limenunuliwa kisha anasema eti apewe mwingine kwani atakuwa ameepusha nini,? gharama ni zile zile so u see again he is too
weak to enforce power to his government, PM anatoa tamko bado magari yananunuliwa tena cha ajabu wanamnunulia yy aliyetoa tamko wanamdharau na shame to him, hafai, kuwa mwaminifu without uajibikaji is useless, period
 
Malafyale

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2008
Messages
11,836
Likes
4,458
Points
280

Malafyale

JF-Expert Member
Joined Aug 11, 2008
11,836 4,458 280
Waziri Mkuu ndiye Mtendaji Mkuu wa Serikali;inakuaje anaruhusu hadi mamilion ya pesa yanatumika kumnunulia gari then anakataa anapokabidhiwa ili hali pesa nyingi za walipa kod maskini wa TZ zimekwisha tumika?

Ningemuona PM Pinda wa maana kama tu angekataza matumizi ya pesa kwenye mashangingi kwa kusistiza kuwa mawaziri magari yao bado yanafaa.Kukataa gari ambalo serikali imekwisha lilipia na hela zetu zimekwisha kwenda na maji hakuna maana yeyote kwa watz

Mtoto wa Mkulima Pinda tunazidi kwenda barabara tofauti na mimi kwenye utendaji wako;kwanza ulinifanya nisikuelewe kwenye majibu ya MEREMETA Bungeni na sasa ni kwenye haya matumizi holela ya pesa za wa TZ kwenye masuala yasiyo na msingi wowote!

Milion 300 za shangingi "ulilo likataa ungezipeleka hata kwenye zahanati ya kijijini kwenu Mlele" ungeokoa maisha ya akina mama wengi sana wanaokufa kwa kukosa huduma siku za kujifungua!
 
babukijana

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2009
Messages
5,220
Likes
1,675
Points
280

babukijana

JF-Expert Member
Joined Jul 21, 2009
5,220 1,675 280
nunueni migali tu sijui VX,GX.V8 shangingi,mkonga,******,whatever,yote sawa.al muradi serekali ya sisemi iko hewani.wacha watuue tu.
 
Ndjabu Da Dude

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2008
Messages
3,921
Likes
616
Points
280

Ndjabu Da Dude

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2008
3,921 616 280
Kwa kiasi fulani hao mawaziri nao ni "watoto wa wakulima" kwani miaka nenda rudi wooote wameng'ang'ania tu Land Cruiser VX badala ya mfano Range Rover Vogue, Porsche Cayenne, Audi Q7 au hata good ol' lambo, wakati tofauti ya bei ya magari haya yote ni almost nil.
 
MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Messages
5,566
Likes
29
Points
135

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2008
5,566 29 135
Usanii ule ule tu. Swali langu ni kwamba kwa nini hilo gari lime nunuliwa in the first place? Na mbona Pinda anavyo ongea ni utazani kanunuliwa zawadi? Matumizi ya serikali lazima yaidhinishwe na Bunge au ofisi husika kwa hiyo haileti picha kusema kwamba Pinda new nothing about it kuanzia lilipo pangwa kununuliwa mpaka likaletwa.

Na hili wazo la yeye hali hitaji basi apewe lingine nalo hali leti picha. Kama utaratibu wake ndiyo huo basi watu wata kuwa wana nunua vitu (pasipo yeye kujua maana na elekea hajui matumizi yana kwendaje) kuji nufaisha wao kisa wanajua waziri mkuu ata vikataa. Nchi yetu bwana saa nyingine ina kera. Hakuna organization kabisa.
 
W. J. Malecela

Tanzanite Member
Joined
Mar 15, 2009
Messages
14,049
Likes
3,401
Points
280

W. J. Malecela

Tanzanite Member
Joined Mar 15, 2009
14,049 3,401 280
- Nimesema mara nyingi sana kwamba Great Thinkers tunatakiwa kujadili taifa kwa kutumia katiba, miongozo na facts, Waziri Mkuu hawezi kutoa amri ya kuzuia kununuliwa kwa magari yanayonunuliwa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri, ambayo ilipitishwa na bunge la pamoja kati ya CCM na Wapinzani, na kuwekewa bajeti yake tayari!

- Mengine ni common sense japo kidogo sana na wala sio politics as usual!

William.
 
MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2008
Messages
5,566
Likes
29
Points
135

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2008
5,566 29 135
- Nimesema mara nyingi sana kwamba Great Thinkers tunatakiwa kujadili taifa kwa kutumia katiba, miongozo na facts, Waziri Mkuu hawezi kutoa amri ya kuzuia kununuliwa kwa magari yanayonunuliwa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri, ambayo ilipitishwa na bunge la pamoja kati ya CCM na Wapinzani, na kuwekewa bajeti yake tayari!

- Mengine ni common sense japo kidogo sana na wala sio politics as usual!

William.
Ni kweli kila kitu kinaenda kikatiba mkuu. Ila kama bajeti ya kumnunulia waziri mkuu gari jipya ilisha pitishwa kwa nini aje kulikataa? Maana bajeti ina specify hela fulani ni ya kitu fulani kwa hiyo ili takiwa awe tayari anajua right? Sasa kama lime nunuliwa na aka likataa it means hiyo pesa haikua kwenye bajeti ya kumnunulia waziri mkuu gari jipya.

Pia kusema waziri mkuu hana say katika hili japo ni kupotosha. Wakati wa bajeti ofisi ya waziri mkuu kama lazima iwasilishe bajeti ya matumizi. Kwenye hiyo bajeti ita sema pesa fulani ni ya vitu fulani kisha Bunge ina idhinisha. Bunge hai tengenezi budget proposals. Sasa wakati ofisi yake inaanda bajeti hiyo yeye hakujua? Au hashughuliki na uundwaji wa bajeti ya ofisi yake?

Otherwise kama kwenye ofisi zetu za umma pesa zina tumika bila kupangiwa matumizi maalumu na bila viongozi wa juu kabisa kujua basi we have a problem.
 
Emma Lukosi

Verified User
Joined
Jul 22, 2009
Messages
931
Likes
8
Points
35

Emma Lukosi

Verified User
Joined Jul 22, 2009
931 8 35
- Nimesema mara nyingi sana kwamba Great Thinkers tunatakiwa kujadili taifa kwa kutumia katiba, miongozo na facts, Waziri Mkuu hawezi kutoa amri ya kuzuia kununuliwa kwa magari yanayonunuliwa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri, ambayo ilipitishwa na bunge la pamoja kati ya CCM na Wapinzani, na kuwekewa bajeti yake tayari!

- Mengine ni common sense japo kidogo sana na wala sio politics as usual!

William.
SiRikAli, KaTibA, MiongOzO vyote hivyo ni UHUNI tu ndani ya Nchi hii.
 
mambomengi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2009
Messages
829
Likes
24
Points
35

mambomengi

JF-Expert Member
Joined May 16, 2009
829 24 35
- Nimesema mara nyingi sana kwamba Great Thinkers tunatakiwa kujadili taifa kwa kutumia katiba, miongozo na facts, Waziri Mkuu hawezi kutoa amri ya kuzuia kununuliwa kwa magari yanayonunuliwa kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri, ambayo ilipitishwa na bunge la pamoja kati ya CCM na Wapinzani, na kuwekewa bajeti yake tayari!

- Mengine ni common sense japo kidogo sana na wala sio politics as usual!

William.
Samahani, hujui unaongea nini!
 
Forum statistics

Threads 1,203,212
Members 456,663
Posts 28,104,846