Pinda akaribisha wawekezaji sekta ya gesi asilia.

KunjyGroup

JF-Expert Member
Dec 7, 2009
352
26
WAZIRI MKUU, Mizengo Pinda, amesema wakati umefika kwa wawekezaji wa kimataifa, kuangalia uwezekano wa kuwekeza rasilimali zao katika miundombinu ya kusafirishia gesi asilia kama njia ya kusaidia kukuza uchumi wa Tanzania.
Hawa wawekaezaji tulionao wa Gold, Diamond, Tanzanite wamekuza uchumi?
 
Kama kweli kashauri hivo, amekosa fikra sahihi kuhusu jambo zima!! Kama alijua kuwa gesi itahitaji kusafirishwa, alipaswa kujua mipango ya muda mfupi, wa kati na mrefu. Na kwa kila mpango, alipaswa kuwa na strategic plan implementation. Kama ni wawekezaji, angejua siku nyingi uwezekano wa wao kuwekeza. Lakini kuja na habari za "tuna mipango ya kusafirisha gesi kwenda Tanga na Mwanza" halafu siku chache baadae anahimiza uwekezaji, inaonesha wazi mambo mengi yanafaywa au kimtazamo, au kisiasa.

Aache siasa, afanye kazi kitaaluma!!
 
Yaani Pinda nawenzake wanaongea bila kufikiria zaidi. Kutoka lini foreign investment imekuza uchumi wakati mikataba ina tax breaks
 
Back
Top Bottom