Maseto
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 944
- 545
Sasa naamini sikio la kufa halisikii dawa kwa CCM.Walianza akina Nape na Kinana kuwataja mawaziri mizigo lakini jina la Pinda halikuwemo.Wabunge wakamtaja Pinda kuwa ndiye mzigo mzito mno kubebeka.
Jana Pinda ndiyo kaiharibia zaidi CCM kwa kusema kazi ya uwaziri mkuu hakuiomba na ni ngumu mno,akasema kama wakiona inafaa wakamtoa atafurahi.
Hapa kimantiki alimaanisha kuwa;
1.yeye hayuko tayari kujiuzuru,
2. Hayuko tayari kujirekebisha ili aongeze ufanisi,
3. Uwezo wake ndiyo umegota hapo,hana ziada ya uwezo wa utendaji.
4. Ameridhika na kiwango chake cha utendaji na anaona wanaosema hafanyi vizuri wanamuonea.
Ieleweke kuwa kwa nchi masikini kama hii,mtu anapopewa cheo maana yake ni kwa ajili ya kujikimu yeye,familia yake na ndugu siyo kwa ajili ya kutumikia wananchi wake.
Hapa ni vema tukakumbuka nadharia ya Abraham Maslow ambayo inaelezea kuwa mahitaji ya binadamu hujipanga kwa muundo wa piramidi,chini huanza mahitaji ya msingi kama vile chakula,mavazi na malazi.Baada ya kukidhi mahitaji ya msingi binadamu huhitaji yasiyo ya lazima sana kama vile ulinzi,starahe na kadharika na hatimaye binadamu hufikia kilele cha mahitaji kwa kuhitaji ufahari wa kujulikana,kuenziwa na kutukuzwa.Hapo ndipo mtu hugombea vyeo vya kisiasa au kutoa misaada kwa watu wenye mahitaji ili atukuzwe.
Kwa maana hiyo Pinda ambaye alikuwa kachero tu ikulu pale anashukuru sana kuwezeshwa kujikimu maisha yake yote ndiyo maana anasema atafurahi akiondolewa kwa kuwa lengo lake litakuwa limetimia.
Swali la kujiuliza CCM watamuondoa?mimi nitashangaa akiondolewa kwa sababu moja kubwa;yeye ni kachero na wanaopendekeza kuondolewa kiongozi ni makachero wenzake ndani ya utawala.
Hata hivyo wasipomuondoa madhara kwa CCM ni makubwa sana kwa sababu amekiri mwenyewe kuwa hana uwezo zaidi wa kutekeleza majukumu ya waziri mkuu.