Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,896
Nikuulize Waziri Mkuu yafuatayo
Muungano wa Tanzania nini mantiki yake wakati Zanzibar ni nchi inayotambuliwa na OAU, kwa hiyo Rais wa Jamhuri ya muungano hana nguvu Zanzibar. Zanzibar wana Bunge lao na wanashiriki Bunge la Muungano wa Tanzania, hivyo bunge la Tanganyika liko wapi? Wazanzibar wana nafasi ya ajira zaidi katika utumishi wa serikali kuliko wa bara kwa maana kwamba wana serikali ya zanzibar inayowapa ajira na wamo ndani ya serikali ya Muungano wanakopata ajira. Wa bara wamo ndani ya serikali ya Muungano tu kwa kutoundiwa serikali yao ya Tanganyika.
Kuhusu Hospitali ulizoorodhesha nyingi ni zile zilizoanzishwa na taasisi za dini si serikali kama uivyosema. KCMC na Bugando ni za Taasisi za dini si serikali na hivyo serikali haiwezi kujivunia kwamba ni matunda yao. Zahanati, vituo vya afya na hospitali nyingi zimejengwa na taasisi za dini kutokana na mashirika ya dini toka nchi za nje, hivyo ni jambo la aibu kwa serikali kuorodhesha huduma hizo kwamba zimefanya na serikali.
Takwimu za huduma za maji ulizoleta hata mtoto mdogo atakukatalia si kweli, kwani ni pungufu ya asilimia ulizoleta. Waulize tu wa hapo Dodoma wanavyohangaika na maji kama kweli wana 80% ya maji unayosema. Vijijini waziri Mkuu ningekuwa mie ningeona aibu hata kusema afadhali kunyamaa tu.
Elimu ni aibu tupu idadi kubwa ya wanafunzi kushindwa mitihani ambayo kwa Tanzania kiwango cha ufaulu ni chini sana ukilinganisha na mataifa mengine, sasa wanafunzi washindwa hata kupata dalaja la nne, inatisha.
Serikali imeanzisha shule kisiasa kama vile maskini anavyofikiria kuwa na watoto wengi ndio utajiri bila kufikiria malezi bora kwa watoto. Shule hazina maabara, hakuna vyumba vya madarasa, hakuna vitabu vya kiada, hakuna madawati, hakuna walimu, lakini waziri mkuu hukusema hayo. Vyuoni wengi tumesikia mengi yanayolalamikia na wanavyuo.
Huwezi kulinganisha mazingira ya Tanzania ya mwaka 1960 na Tanzania ya 2011, huku ni kuzidi kuwadanganya watanzania. Tanzania ya leo si ile ya kuwaimbia nyimbo za kuwasifu viongozi, bali ni Tanzania ya walioelimika na wenye uhakiki wa hali ya juu.
Hotuba ya Waziri mkuu imekuwa kama kuwapa darasa Watanzania wakati watanzania wanajua wana ufahamu wa hali ya juu sasa katika masuala ya kijamii, kisiasa nk.
Kwa maana hiyo Waziri Mkuu Mizengo Pinda anaendelea kudanganya Bunge na wananchi.